Wednesday, January 22, 2014

Kutoka Kongo

Je, bado unaikumbuka ndoa hii ya kihistoria iliyofungwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ya mwanaume mmoja kufunga ndoa na wanawake watatu. Jamaa anaonekana kufurahim, wanawake je? Hebu waangalie vizuri.

Wote wanatafuta riziki!

Mwenye mkokoteni, dereva wa daladala na mwenda kwa miguu wote wanatafuta riziki!

Mafuta ya ubuyu yanatoka katika mti huu

Huu ni mbuyu.Miaka ya nyuma mti wa mbuyu ulikuwa unaonekana hauna faida yoyote zaidi ya ubuyu. Ukubwa wake hauwezi hata kutoa mbao nzuri, haufai pia hata kuchoma mkaa! Lakini katika miaka ya hivi karibuni hapa  Tanzania, mbuyu umewanufaisha watu wengi. Mafuta ya ubuyu yamekuwa yakiaminika kuwa tiba ya magonjwa mbalimbali hivyo kuwa biashara ya maana. Baadaye ilibainika kuwa mafuta hayo si salama. Hadi hivi sasa taarifa kamili haijatolewa kuhusu mafuta ya ubuyu. Tunasubiri taarifa rasmi.

Tuesday, January 21, 2014

Usafiri wa 'Bodaboda'

Niseme ukweli mimi binafsi sipendi kupanda pikipiki au maarufu kwa jina la bodaboda

Friday, January 10, 2014

Fenesi - sura inatisha manufaa ni makubwa

Ukiliona tunda la fenesi kabla halijakatwa kwa kweli halivutiii. Lina sura ya kutisha lenye nundunundu nyingi lakini likishakatwa ni tamu kulila. Licha ya utamu wake, fenesi lina faida zifuatazo kwa afya zetu.
i. Lina vitamini C ambayo huongeza kinga ya mwili
ii Hupunguza mafua
iii.Husaidia kupunguza maumivu ya kifua na homa
iv. Huupa mwili nguvu kwani yana madini ya wanga na sukari
v.Huondoa sumu mwilini hivyo kuwa na kinga ya saratani  k.m. mapafu, midomo, kinywa na tumbo
vi.Tiba ya shinikizo la damu kwani lina madini ya potasium
vii.Hurahisisha mmeng'enyo wa chakula (digestion)
viii. Linasaidia kuzuia kuvimbiwa
ix.Kwa wenye matatizo ya macho husaidia uoni (Kwa mujibu wa Dr. Deepark Kevat wa Shree Hindu Mandal Hospital - Dar Es Salaam)

(Kwa hisani ya gazeti la Mwananchi 10/01/2014- Ijumaa)

Thursday, January 9, 2014

Kisiwa cha Chumbe

Kisiwa cha Chumbe kilichopo Tanzania. Fanya utalii hapo kha! Ubahiri wa nini na fedha unazo?

UIsinichokoze

Ukimchezea chui katika raha zake atakurarua. Fahari ya Tanzania

Jay Z na Beyonce

Unakumbuka wanamuziki nguli wa Amerika wameshawahi kutua Tanzania? Hao ni Jay Z na Beyonce

Filebert Bayi enzi zake

Filbert Bayi wa ukweli, enzi zake. Wanariadha wa sasa chokest!

Nyerere na Karume

Hayati Mwl. J.K.Nyerere (kushoto) na Sheikh Abeid Amani Karume.Waasisi wa Muungano wa Tanganyika na Unguja iliyozaa TANZANIA. Wote walikuwa na nia njema na walifanikiwa. Tunakwenda wapi?

Atamchoma tu

Hii ni michezo ya baharini nyumbani Tanzania. Kuvua samaki kwa mkuki!

Unapoingia Lindi mjini

Kusini raha barabara ya lami hadi Mtwara. Hapa unaingia Lindi mjini. Hebu tupia jicho bahari ya Hindi.

Afrika imetengenezwa na Mungu


    Angalia Taswira hii. Mungu anaipenda Afrika!

Adili na Nduguze

Je ulibahatika kusoma kitabu hiki cha Shaabani Robert? Adili na Ndugu zake. Kitafute.

Friday, January 3, 2014

Lazima utafunga tu

Kama futuru yenyewe ndiyo mazagazaga haya, lazima ufunge!- Picha kwa hisani ya kurasa za fb za Mibavu

Anajifunza kusonga ugali

Mama wa kesho anajifunza kusonga ugali-Picha kutoka kurasa za fb ya Mibavu.

Kumbe Mibavu Gungu ni Simba!

Sikujua kuwa rafiki yangu Mibavu Gungu ni Simba damu. Picha hii nimiipata kupitia ukurasa wake wa fb

Msafiri kafiri

Kweli kuna sehemu nyingine barani Afrika usafiri ni wa taabu kweli kweli.

Mwaka 2014 nimeanza na matunda

Wengi wetu hupenda matunda. Tunaambiwa matunda yana vitamin aina nyingi ambayo huipa miili yetu kinga. Kwenye picha kuna ndizi,mananasi,machungwa, zabibu,peyas na pichis. Tanzania tumebahatika ya kuwa na matunda ya tropiki na matunda ya kutoka sehemu za baridi kama Mgeta mkoani Morogoro, Njombe, Tukuyu, Lushoto na sehemu nyingine. Lakini matunda kama vile ndizi, mananasi na machungwa hupatikana kwa wingi kijijini kwangu Matombo mkoa wa Morogoro. Kilimo cha matunda  ni Biashara. Kwenye mazingira yanakostawi matunda tujikite na kilimo hicho na tufuate ushauri kutoka kwa wataalamu tulime kwa faida. Wakulima tubadilike. Fedha ziku shambani.Karibu Morogoro tule matunda!

Thursday, January 2, 2014

Karibu mwaka 2014- Moro Oyee!

Mwaka 2013 ulikuwa na changamoto nyingi kwa Banzi wa Moro. Misiba mingi. Nimepoteza mjomba mdogo wangu na ndugu wengine. Hata hivyo kulikuwa wakati wa furaha pia. Harusi nyingi, watoto wamezaliwa na shughuli nyingi tu za kikazi. Namshukuru Mungu kwa kufanikiwa kuingiza posts 602 ambapo mwaka 2012  niliingiza posts 573.




Hata nikiwa mbali na Moro nakumbuka Moro Oyee.....
Nawashukuru wadau wa Banzi wa Moro, wengi wamepitia Blog yangu mwaka 2013 lakini ni wachache sana waliotoa comments. Nawaomba mwaka huu mchangie zaidi katika matukio mbalimbali yatakayoonekana kwenye Blog hii.Kwa kuanza  mwaka huu nawaletea waburudishaji wa Mji Kasoro Bahari (Moro) wakikumbushia enzi za  Marehemu Mbaraka Mwinshehe, Salumu Abdallah na wanamuziki wengine mahiri wazamani wa Morogoro.