Ukiliona tunda la fenesi kabla halijakatwa kwa kweli halivutiii. Lina sura ya kutisha lenye nundunundu nyingi lakini likishakatwa ni tamu kulila. Licha ya utamu wake, fenesi lina faida zifuatazo kwa afya zetu.
i. Lina vitamini C ambayo huongeza kinga ya mwili
ii Hupunguza mafua
iii.Husaidia kupunguza maumivu ya kifua na homa
iv. Huupa mwili nguvu kwani yana madini ya wanga na sukari
v.Huondoa sumu mwilini hivyo kuwa na kinga ya saratani k.m. mapafu, midomo, kinywa na tumbo
vi.Tiba ya shinikizo la damu kwani lina madini ya potasium
vii.Hurahisisha mmeng'enyo wa chakula (digestion)
viii. Linasaidia kuzuia kuvimbiwa
ix.Kwa wenye matatizo ya macho husaidia uoni (Kwa mujibu wa Dr. Deepark Kevat wa Shree Hindu Mandal Hospital - Dar Es Salaam)
(Kwa hisani ya gazeti la Mwananchi 10/01/2014- Ijumaa)
No comments:
Post a Comment