Monday, February 23, 2015

Kuongeza thamani ya mazao yetu isiishie mdomoni




Maabara zina vifaa vya kawaida kabisa na visivyo na gharama kubwa, hata hivyo taasisi za utafiti wa kilimo nchini India zinafanya utafiti wa uhakika kuhusu uongezaji thamani ya mazao na teknolojia baada ya mavuno (post-harvest technologies). Timu ya wataalamu wa kilimo na Mifugo iliyofanya ziara ya mafunzo nchini India mwaka 2014 iliweza kutembelea maabara hizo na kujionea wenyewe jinsi utafiti wa kuongeza ubora wa mazao unavyofanyika kuanzia mpunga hadi matunda. Tulipata bahati ya kuonja juisi iliyo kwenye utafiti. Mambo yakienda sawa kampuni mmoja itazalisha kwa wingi juisi aina hiyo hivyo mtafiti,kiwanda,wafanyabiashara na walaji kunufaika. Wadau hao wanaweza kuchangia utafiti wa uzalishaji na usindikaji wa matunda hayo.

Tuache siasa tufanye utafiti





Sayansi lazima itumike na utafiti lazima ufanyike ili kuweza kukabiliana na matatizo katika nyanja mbalimbali. Katika kilimo matumizi ya bioteknolojia hasa ya Genetic Modified Organisms nchi nyingine imekuwa vigumu kukubalika. Tulipokuwa India tulitembelea Taasisi inayoshughulikia masuala ya bioteknolojia. Binafsi nilishangaa kuwakuta watafiti wengi vijana wakijihusisha na fani hiyo na wengi wao ni wanawake. Maabara zao zimejaa vifaa na madawa ya kufanyia utafiti ndiyo maana vijana wanavutiwa na fani hii. Hata hapa Tanzania, maabara yetu ya bioteknolojia iliyopo Mikocheni  watafiti waliowengi ni vijana. Tuache siasa tufanye utafiti na kuwekeza katika utafiti.

Utafiti unaofanywa kwenye mradi wa EAAPP

'Eastern Africa Agricultural Production and Productivity Project.' unatekelezwa na nchi nne zilizoko Mashariki ya Afrika nazo ni Tanzania, Uganda, Kenya na Ethiopia. Watanzania tumejikita zaidi katika zao la mpunga ingawa mazao ya muhogo, ngano na ng'ombe wa maziwa nao unafanyiwa  kazi. Katika mradi huo moja ya shughuli zinazofanyika ni Utafiti. Wakati mradi huu unafikia ukingoni mwaka huu 2015, watafiti wameandaa kijitabu chenye muhtasari wa tafiti zilizofanyika chini ya mradi huu. Moja ya mradi ambao umeandikiwa muhtasari huo ni huu hapa.'Genetic variability of improved and traditional rice (oryza sativa L.) varieties from Eastern Africa for Phosphorus deficiency tolerance. Watafiti wanaoshughulika na utafiti huu ni Atugonza Bilaro (ARI-Tumbi, Tabora, Tanzania);Ahura Luzi-Kihupi (Sokoine University of Agriculture, Morogoro,Tanzania); na Khady Nani Drame (Africa Rice Centre-Dar Es Salaam, Tanzania).
Hebu tuone kwa kifupi kuhusu mradi huo:-

"Low soil phosphorus is one of the limiting mineral nutrients in rice production. In Tanzania, available soil P in some rice producing area is as low as 2.7 mg/kg soil. This is aggravated by the fact that the majority of Tanzanian rice farmers do not apply fertilizers or apply only urea probably because of associated high costs. Therefore, developing P-efficient varieties will ensure relatively high yields in P-decifient areas and at reduced costs for smallholders. This study aimed at improving P-deficiency tolerance of local rice varieties grown widely in the East and Southern Africa (ESA) region. The specific objectives are (i) to identify tolerant and susceptible widely grown rice genotypes under phosphorus deficient soil conditions, and (ii) to study the distribution of Phosphorus starvation tolerance (PSTOLI) gene as a basis for selecting recipients in the biparental crosses."

....can biosciences contribute?

Sipendi kutafsiri 'Title' ya kitabu hiki naweza nikaondoa maana yake. Nimepokea kitabu hiki hapa ofisini tarehe 20/02/2015, Ijumaa. Ilikuwa ni zawadi ya kwanza ya asubuhi na mapema. Kurasa za mwanzo kabisa za kitabu hiki zimeanza na 'quotations' za watu maarufu. Hebu ni nukuu hii iliyopo ukurasa wa 5. "we can feed the world but it will not be easy. There are no magic bullets. The answer lies in seeking win-win-solutions where there are economic, social and environmental benefits."  Gordon Conway
One Billion Hungry:Can We Feed the World?
Comstock Publishing Associates, 2012

Ukipata fursa ya kukisoma kitabu hiki basi fanya hivyo. Kinafaa kusomwa na watu wote.

Mizengo anapofurahi

Nimeshawahi kumuona Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda 'live' au kupitia vyombo vya habari. Mara nyingi namuona yuko 'serious.' Picha hii inamuonyesha Pinda akiwa ametabasamu na kuwa na furaha ya pekee sijui alikuwa anaongelea jambo lipi.

Wataalamu wa Halmashauri na sekta ya Kilimo wanapokutana

Tunasoma kwenye taarifa nyingi kuwa bado kuna mapungufu ya kimahusiano kati ya ugani,wakulima na watafiti katika kuwafikishia teknolojia bora za kilimo walengwa hapa nchini. Tatizo ni nini? Hatupangi kwa pamoja? Je, raslimali ni chache au tatizo ni kwa wataalamu wenyewe? Mnasemaje wadau wa kilimo hapa Tanzania. Pichani timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi wakiwa ofisini kwa Afisa Kilimo wa Wilaya  ya Mtwara wakijadiliana kuhusu utekelezaji wa mradi wa EAAPP katika Halmashauri hiyo.

Fanya yako- Ujumbe mzito

Leo asubuhi wakati nikija kazini nakumbana na ujumbe  mzito  'fanya yako' ulioandikwa kwenye gari  la miguu mitatu  aina ya PIAGGIO. Nilitafakari. Ni ujumbe mzito.Nikakumbuka kuwa kwenye mkoba wangu kuna Camera nikaipiga picha.Muwasilishaji anaweza kuwa sahihi au hapana. Ndiyo usipofanya yako nani atakufanyia. Lakini upande mwingine je furaha unayoipata au karaha unayoipata ni kwa kufanya yaliyo yako peke yake? Tafakari.

Thursday, February 19, 2015

Mbwembwe za maharusi

Hizi zinaitwa mbwembwe za maharusi. Gari ni jeep, mavazi ya gharama na mapambo ya kiufundi

Iko siku atakuwa Mhasibu wa Dar Young Africans

Mhasibu Pouline Mlekani amechaguliwa kwa kishindo kushika nafasi ya Uhazini ndani ya Tawi la Yanga Tabata. Pouline ni mwanachama na mpenzi wa YANGA. Iko siku atakuwa mhasibu wa kwanza wa kike wa Klabu ya YANGA.HONGERA!

Hata mbuyu ni kivutio cha watalii

Mbuyu waweza pia kuwa kivutio cha watalii (Picha kwa hisani ya fb ya TANAPA)

Wazungu Mikumi sisi nyumbani

Wazungu hutembelea Hifadhi zetu za Taifa kwa utalii sisi tuko nyumbani wala hatuna habari tukisingizia gharama wakati si kweli. Umeona eh, ndiyo maana wageni wanaweze kuandika na kuelezea vizuri hifadhi zetu kuliko Watanzania Wazalendo. Si shangai kuona kwenye fb ya TANAPA habari nyingi zimeandikwa kwa lugha ya Kiingereza!

Tembo aweza kung'oa miti

Ni kweli kuwa Simba ni mfalme wa nyika, lakini Tembo kwa ukubwa wake anaweza kung'oa miti

Ndege huyu anaitwaje?

Ndege huyu anapatikana kwenye  Hifadhi Zetu za Taifa picha nimepata kwenye postings za fb ya TANAPA.Wanaofahamu jina la ndege huyu kwa kiswahili naomba wanifahamishe.

Mnyama anatisha!





Umeshawahi kumuona simba wa kweli (siyo kwenye picha au video).Huyu ndiye Simba au 'mnyama' ni mfalme wa  msituni, binadamu pia humuogopa. Ndiyo maana hapa Tanzania kuna club moja ya michezo inaitwa 'Simba Sports Club.' Hii si Klabu ya kuchezea mwaka huu tayari imeshanyakua vikombe viwili muhimu (Mtani Jembe na Mapinduzi).Kweli  Mnyama anatisha. Hifadhi zetu za Taifa  zilizo nyingi SIMBA hupatikana tuwe na mazoea ya kuzitembelea. Inakuwaje wageni hasa wazungu wanafahamu mengi kuhusu Hifadhi za Taifa kuliko sisi?

Maua Simba majani Yanga

Maua Simba majani Yanga. Hivi ni moja ya vivutio katika Hifadhi zetu za Taifa

Wednesday, February 11, 2015

Mwanasheria akiwa na miaka 74

Mzee Ole Kipeyan kutoka Arusha, tarehe 24 Januari 2015 alitunukiwa  shahada ya sheria kutoka Chuo Kikuu Huria Tanzania akiwa na umri wa miaka 74.

Tuesday, February 10, 2015

Ni Kawaida Kijiji cha Kisemvule kukutana



    Kijiji changu cha Kisemvule, Mkuranga kina utaratibu mzuri wa kufanya mkutano mkuu wa kijiji wa mwaka ambapo wanakijiji wote hualikwa kujadili maendeleo ya kijiji kwa mwaka uliopita na kupanga mipango ya mwaka ujao. Hoja hutolewa na kujadiliwa na maazimio kufikiwa. Huu ni utaratibu mzuri. Pichani wanakijiji waume kwa wake na vijana wakiwa katika mkutano wa kijiji ulifanyika Januari 2015.

Hii ndiyo NASHERA HOTEL iliyopo Morogoro

NASHERA HOTEL.Kwa sasa hii hii inaongoza kwenye hadhi ya kimataifa mjini Morogoro. Anayemfahamu mmliki wa Hotel hii anifahamishe.

Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika




Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika lilikutana mjini Morogoro kuanzia tarehe 26-27 Januari 2015 ni kikao cha pili tangu Baraza jipya liundwe, lakini ni kikao cha kwanza kwa mwaka 2015. Masuala mengi yalijadiliwa pamoja na Mada mbalimbali kuwasilishwa zikiwemo zile zilizohusu masuala ya Mifuko ya Jamii, Bajeti ya Wizara, Majukumu ya Wajumbe wa Baraza, UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa  na Maadili ya Utumishi wa Umma. Wajumbe walikuwa na hoja kemkem kutokana na mada zilizowasilishwa, ufafanuzi ulitolewa na maazimio ya kutekelezwa yaliainishwa.

Wako wapi akina baba kwenye Jumuiya Ndogondogo?



Jumuiya Ndogondogo ya Mt. Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Vikindu ni Jumuiya kongwe Parokiani na yenye wanajumuiya wengi. Jumuiya inajitahidi kukutana karibu kila Jumamosi na kushiriki shughuli za parokia inapohitajika. Hata hivyo, parokia hii ina udhaifu mmoja, wanaume wachache wanaonekana kwenye Jumuiya ingawa wapo wengi. Haingii akilini watoto wote hawa na akina mama hawa wanaishi bila akina baba. Hii ni changamoto kubwa kwenye Jumuiya zetu.

Safari kuelekea Jumuiya Ndogondogo

Kila siku ya Jumamosi asubuhi, Jumuiya yetu Ndogo ya Mt.Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Vikindu hukutana kwenye moja ya nyumba ya mwanajumuiya kwa kuzingatia ratiba kwa lengo la kusali pamoja na kujadili masuala ya Jumuiya. Jumuiya inahimiza watoto kushiriki kwenye Jumuiya ili kujenga Kanisa endelevu. Pichani kijana  wa Jumuiya anakata mbuga kwenda kwenye Jumuiya huku akiwa amebeba vitabu na kumbukumbu mbalimbali.

Vijarida visisubiri NANENANE



Nilichojifunza nikiwa India. Kwanza vijarida vya teknolojia za kilimo vinavyotolewa kwa wakati vinapatikana katika vituo vyote vya utafiti tulivyotembelea. Vituo hivyo vina sehemu maalumu ya kuhifadhi vijarida (museum)na maelezo mbalimbali ya utafiti havisubiri siku ya maonyesho. Fedha za kutosha  zinatumika kwa shughuli hii. Watafiti wote wanafahamu kinachoendelea kituoni. Lakini kizuri zaidi siku zote katika vijarida vyao wanatanguliza lugha yao na hasa kihindi, kiingereza baadaye (kwa wageni tu). Vijarada visisubiri NANENANE!

Tuwekeze kwenye utafiti





Kutatua matatizo ya kilimo shambani hatuna budi kuwekeza kwenye utafiti. Hivi ni vifaa vichache kwenye maabara ya udongo nchini India ambavyo vinatumika katika uchunguzi wa udongo.

Kabla ya kuwekeza kwenye uzalishaji wa mazao lazima hali ya udongo ifahamike ili kuweza kutambua aina ya zao linalotakiwa kustawishwa. Hapa Tanzania maabara za udongo ziko chache sana. Ile ya Kitaifa iko Mlingano, Tanga nyingine Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine-Morogoro, Ukiriguru-Mwanza, Selian-Arusha na Uyole-Mbeya.Vifaa vya maabara ya udongo kama ilivyo kwa maabara ya magonjwa ya binadamu, ni ghali mno! Hata hivyo ni muhimu kuwa navyo kama kweli tunataka kuwekeza kwenye kilimo cha kisasa. Hali ilivyo kwenye maabara zetu nyingi si nzuri. Tunao watafiti waliobobea lakini wanakosa vifaa vya kisasa vya kuendesha utafiti wao, ndiyo maana wakati mwingine wadau wanalalamika kuwa ukipeleka sampuli yako ya udongo pale Mlingano-Tanga inachukua muda mrefu kupata majibu.

Hakuna ardhi isiyofaa

Hakuna ardhi isiyofaa. Ukishindwa kustawisha mpunga,mahindi,mtama na mbogamboga unaweza kustawisha miti ya aina mbalimbali inayoweza kukupatia kipato cha kuweza kununua mahitaji mengine kama vile chakula, mavazi na makazi.

Huko India wanafanya tafiti mbalimbali ya matumizi mbadala ya ardhi kama vile kupanda miti. Tayari wameshapata matokeo mazuri ya aina ya miti inayoweza kustawishwa kwenye aina hizo za udongo kama vile udongo wenye tindikali nyingi kupitia kituo kilichopewa jukumu la kufanya tafiti za udongo. Kituo chetu cha utafiti wa kilimo Tumbi-Tabora kimepewa majukumu ya kuendesha tafiti hizo. Tukae mezani kukiwezesha kituo hiki kiendelee kufanya tafiti hizo kwa manufaa ya taifa.

David Kafulila

Mhe. David Kafulila. Mbunge kijana mweledi anayeibua mengi Bungeni anachozungumza ana uhakika nacho. Wabunge kama hawa ndiyo wakuwapigia kura. Mbunge gani miaka mitano inapita hata hujaonekana kwenye Hansard! (kumbukumbu za bunge).

Anna Kilango amefika?


Simba anapomlenga Yanga

   Simba anapomlenga Yanga ujue kesha!