Tuesday, February 3, 2015

Tulichojifunza kutoka kwa wafugaji wa Amani - Muheza




Amani-Muheza ni sehemu nzuri ya milimani. Wananchi wa Amani wanategemea kilimo na ufugaji kwa maisha yao ya kila siku. Mazao ya chai na ndizi yanalimwa kwa wingi. Miti ya mdalasini,pilipili manga na hata karafuu inaoteshwa pia. Kikubwa kilichotupeleka Amani ni kuongea na kuona shughuli za ufugaji wa ng'ombe wa maziwa. Ni kweli, ufugaji wa ng'ombe wa maziwa unaendelea na baadhi ya wafugaji wamebahatika kupata mafunzo mbalimbali ya ufugaji bora wa ng'ombe  wa maziwa kupitia miradi mbalimbali ukiwemo wa EAAPP. Manung'uniko ya wafugaji hawa ni soko la maziwa si la uhakika na bei yake ni ya chini mno. Lita moja ya maziwa huuzwa kwa bei ya shilingi 600. Vituo vya kukusanya maziwa viko mbali sana hivyo kumfanya mfugaji kutembea umbali mrefu kabla ya kuuza maziwa yake. Wakati mwingine maziwa huharibika na kumwagwa.

Ili kuwaandeleza wafugaji wa ng'ombe wa maziwa wa Amani, kuna haja ya kuboresha miundo mbinu ya barabara na kuongeza vituo vya kukusanyia maziwa. Ni vyema wafugaji wakapata bei nzuri ya maziwa yao. Timu yetu ilitoa ushauri kwa wafugaji wa kuboresha malisho ili kuongeza uzalishaji wa maziwa. Miradi mingine ya ufugaji itakayoanzishwa kuwasaidia wafugaji hao iangalie mambo hayo.

No comments: