Ni mazao machache sana yanayostawi vizuri kwenye udongo wa chumvichumvi.
Kama ilivyo kwa Tanzania, sehemu kubwa ya ardhi nchini India ina udongo wa chumvichumvi. Sehemu hii ingeweza kuzalisha mpunga kwa wingi kama tatizo hili lingetatuliwa. Njia nyingi zinatumika kutatua tatizo hilo kama vile kuweka chokaa ardhini ili kupunguza makali ya chumvi lakini njia hii ni ya gharama kubwa hasa inapotumika kwa eneo kubwa. Watafiti nchini India na hata hapa kwetu Tanzania kituo cha Utafiti KATRIN wanajaribu kuzalisha aina ya mpunga ambao utaweza kuhimili udongo wa chumvi chumvi. Mwaka jana (2014) timu ya wataalamu wa Kilimo waliokuwa kwenye ziara ya mafunzo nchini India, walibahatika kutembelea moja ya taasisi inayoshughulikia utafiti huo. Watafiti hao tayari wameshakuja na aina mbalimbali za mpunga zinazostahimili udongo huo. Ushauri wangu ni kuwapeleka watafiti wetu huko India ili wajifunze zaidi ya jinsi ya kuzalisha mazao mbalimbali katika udongo wa chumvichumvi.
No comments:
Post a Comment