Tunasoma kwenye taarifa nyingi kuwa bado kuna mapungufu ya kimahusiano kati ya ugani,wakulima na watafiti katika kuwafikishia teknolojia bora za kilimo walengwa hapa nchini. Tatizo ni nini? Hatupangi kwa pamoja? Je, raslimali ni chache au tatizo ni kwa wataalamu wenyewe? Mnasemaje wadau wa kilimo hapa Tanzania. Pichani timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi wakiwa ofisini kwa Afisa Kilimo wa Wilaya ya Mtwara wakijadiliana kuhusu utekelezaji wa mradi wa EAAPP katika Halmashauri hiyo.
No comments:
Post a Comment