Tuesday, January 28, 2014
Adha ya ujenzi wa barabara ya mabus yaendayo kasi DAR
Mpaka itakapokuwa imekamilika. Ujenzi wa barabara ya mabus yaendayo kasi jijini Dar utakuwa umewatesa wengi na kwa kweli wachumi tunaweza kukokotoa gharama ya matumizi ya mafuta na kuchelewa kazini wakati wote wa ujenzi wa barabara hiyo/hizo. Tutashangaa!
Mbegu ya mpunga TXD 306 a.k.a SARO 5
Mbegu ya mpunga TXD 306 iliyozalishwa na watafiti wa kilimo Tanzania maarufu kwa jina maarufu la SARO 5 kwenye maonyesho ya kilimo kitaifa huko Dodoma ikipigiwa debe.
Wednesday, January 22, 2014
Vipando vya mahindi
Maonyesho ya vipando vya mahindi kwenye maonyesho ya kilimo Kitaifa viwanja vya Nzuguni, Dodoma mwaka 2013
Zana za Kilimo
Miaka 10 iliyopita Taifa imefanya jitahada za makusudi ya kuongeza zana za kilimo nchini kwa kuboresha sera na kuwafanya wakulima kuweza kutumia zana mbalimbali za kilimo kwa lengo la kuongeza uzalishaji na kuleta tija katika kilimo.
Kwetu pazuri!
Inawezekana picha hii haina uhalisia. Lakini kuna baadhi yetu tunaomiliki magari ya kifahari lakini hatuna makazi mazuri huko tunakofanyia kazi wale kule vijijini tulikotoka.Tubadilike.(Picha kwa hisani ya fb- George Mandepo)
Mahindi mabichi
Biashara ya mahindi mabichi imeenea sehemu nyingi za nchi. Watu wengi hupenda kula mahindi mabichi yaliyochomwa
Madhara ya mvua Iringa
Mvua zinaendelea kunyesha sehemu nyingi za nchi hii kwa sasa. Pichani ni mafuriko yaliyotokea huko Iringa kutokana na mvua iliyonyesha tarehe 7 Januari 2014
Kibanda cha mamalishe
Inasadikiwa kuwa hiki ni kibanda cha mamalishe. Tusicheke. Inabidimmiliki aweze kushauriwa ili aweze kuboresha kibanda hiki kwa lengo la kuvuitia wateja na kulinda afya zao. (picha kwa hisani ya Bw. George Mandepo)
Chai maharage bado zipo Zanzibar
Usafiri wa mjini kisiwani Zanzibar kwa kutumia magari yajulikanayo 'chai maharage" bado unatumika. Hebu angalia jinsi watalii walivyofurahi!
Subscribe to:
Posts (Atom)



















