Mafanikio haya yamepatikana kutokana na kuwa na vitendea kazi bora vya IT,safari za kikazi mikoani, shughuli za kanisa na familia pia. Wasomaji wa Blog hii wamekuwa wakinitia moyo sana kwa kuandika comments zao na wengine kunipigia simu baadhi yao ni Bi. Sophia Kizito, Bw. Charles John Arbogasty wa Botswana, Dada Appia Mkoba wa Norway, Dada Eddy Daulinge wa COSTECH aliyetoa maoni ya kutengeneza pesa kupitia blog hii (Nakungoja Sister), Dogo Fredy Mloka wa TTCL, Dr. Doreen Mloka wa Muhimbili University,Sister Ceasar Mloka a.k.a 'Mzungu' mjisiriamali, Sister Slyvia Daulinge na mumewe Gaitan ambao walikuwa wananipa ujumbe-tumeona vitu vyako! Dada Meab, Dogo Frank Mdimi, Dogo Sily Jakka wa Dadaz Dar (a.k.a. Paroko), Bw.Philemon Kabandwa wa MAFC,Dadaz Ishika na Vidah wa DRD, Dr. Louis Kasuga wa ARI-Naliendele, Bw. Andrew Rabson Kwayu na vijana wake wa IT pale MAFC na wengine wengi.Asanteni sana.
Mategemeo yangu kwa mwakani ni kuboresha zaidi blog hii ili ipendeze na kuvutia wasomaji wengi na pengine kuifanya ya kibashara (kama itawezekana). Yeyote mwenye wazo la kuiboresha namkaribisha. NAWATAKIA MWAKA MPYA WENYE BARAKA ZA MUNGU.