Mwanzoni mwa mwezi Desemba watafiti wakilimo walikutana mjini Morogoro kutathmini utekelezaji wa mradi wa PHRD katika masuala yanayohusu utafiti wa zao la mpunga. Katika kikao hicho cha kazi, ilibainika kuwa, utafiti wa mbegu bora za mpunga, matumizi ya mbolea pamoja na maji unalekea kutoa matunda yaliyotarajiwa na kuna uwezekano mkubwa wa kuongeza tija katika kilimo cha mpunga mara tafiti hizo zitakapokamilika na kuanza kutumiwa na wakulima.
No comments:
Post a Comment