Hapa ndipo mahali nilipozaliwa miaka zaidi ya 50 iliyopita. Sikuzaliwa ndani ya nyumba hiyo ya kisasa ila naambiwa (nimeiona) ndani ya nyumba ya msonge ilioezekwa kwa nyasi na kukandikwa udongo. Kisiki nilichokikanyaga hapo juu ni shina la mwenmbe bongwa. Huu ni mwembe maarufu wa siku nyingi lakini sasa umekwata kupisha ujenzi wa nyumba unayoiona. Tuliobaki ni wajukuu na vitukuu wa familia ya Bw na Bibi Ephrem Lugongo Kobelo maarufu kwa jina la Babu Vibaya. Namshukuru Mungu nimeweza kurudi kijijini na kukutana na ndugu zangu na watoto. Wengine pichani hawajui kijiji kilivyokuwa miaka ya nyuma lakini hapa kwa namna moja au nyingine ndiyo asili yao tulipotoka babu zao na babu,bibi.wajomba, kaka,dada, mama, waume, wake na shangazi zao. Hapa ni NIGE-KARIAKOO, MATOMBO,MOROGORO kwa WAMBIKI wanapotoka akina BANZI
Tuesday, December 30, 2014
Kijiji Nige-Kariakoo nilikozaliwa

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment