Friday, December 5, 2014

Unga safi wa muhogo- Mtwara vijijini


 



 
 
 Chakula cha unga wa muhogo ni cha asili mkoani Mtwara. Lakini miaka ya zamani unga huo ulikuwa hautayarishwi katika mazingira mazuri. Makopa ya muhogo yalikuwa yakiachwa hadi kushika ukungu na kuwa mieusi hivyo unga wake kwa kweli ulikuwa ni mchungu na hauvutii hata kwa macho hivyo kuufanya ukose thamani ni zao lenyewe kukosa thamani na kuitwa zao la njaa. Hali imebadilika kabisa kwa sasa. Baada ya wakulima kufundishwa teknolojia bora za kusindika muhogo. Unga wa muhogo sasa umepanda thamani. Mjini Mtwara kilo moja ya unga huo sasa inapatikana kwa bei ya Tzs 1000-1500/=. Muhogo si zao la njaa tena bali limekuwa la chakula na biashara limeboresha hali ya maisha ya wakulima wengi mkoani Mtwara. Pichani pamoja na kutumia zana za asili za kutayarisha unga huo, kikundi hicho pia kina mashine za kuchakata mihogo mibichi na kuindaa kabla ya kutumia vifaa hivyo vya asili (kinu na mchi) kwa utayarishaji wa unga. Hapa ni Mtwara Vijijini kijiji cha Mbawala-Kikundi cha JITEGEMEE B

No comments: