Tuesday, December 30, 2014

Jay Shanidev-Usafiri wa Dutumi-Mngazi-Dar

Shanidev ni moja ya kampuni za mabus yanayosafirisha abiria kutoka  DAR-Matombo-Mngazi-Dutumi. Huduma hii imeanza hivi karibuni. Kwa kawaida mabus haya hayafiki Morogoro mjini hukatiza barabara ya Mikese. Nilipotoka Matombo kurudi Dar nilitumia bus la Shanidev. Kutoka Matombo hadi Dar ni Tshs 12,000/=. Kituo chake kiko Buguruni karibu kabisa na ofisi ya Jay Hambe. Kwa wakazi wa Buguruni, Ilala, Kigogo, Tabata, Ukonga, Temeke, Mbagala, Kurasini, Tandika na hata wa kutoka wilaya ya Mkuranga. Si Shanidev pekee linalotoa huduma hiyo, yapo pia mabus yanayoitwa BINTI FOROGO!

No comments: