Tuesday, January 31, 2012
Mazinde- Stesheni bila gari moshi
Hivi ndivyo ilivyo stesheni ya Mazinde Mkoani Tanga. Reli ya Kaskazini 'kwishne' kama reli hii ingekarabatiwa ingeweza kutumika kusafirisha abiria na mizigo,hivyo kusaidia kutunza barabara ya Chalinze Arusha kwani mizigo mizito ingesafirishwa kwa gari moshi. Vijiji inamopita reli hiyo vingenufaika sana kiuchumi. Hivi kweli tumeshindwa kuifufua reli ya Kaskazini au ubinafsi. Pichani Stesheni ya gari Moshi ya Mazinde, kibao kinaning'inia lakini gari moshi hakuna na nyasi zimeota kwenye reli na kuta za reli kuporomoka
Napenda kurudi ESAMI
Wahitimu wa mafunzo ya Jinsia katika Bajeti kutoka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika
Maktaba ya Chuo cha Uhasibu Arusha
Nikiwa Jijini Arusha jengo hili lilinisisimua. Lakini nilipoambiwa kuwa ni maktaba ya chuo nilifurahishwa sana. Unapokuwa na jengo zuri la Maktaba kama hili chuoni jua kwamba waliobuni chuo hicho walikuwa wanauelewa mpana kuhusu Elimu. Chuo kisichokuwa na maktaba iliyokamalika basi kina dosari. Maktaba hii ni ya kisasa huenda ikawa ni moja kati ya maktaba bora zaidi hapa nchini. Nimeshatembelea vyuo vingi, taasisi nyingi za serikali na zisizo za kiserikali sijaona maktaba nzuri kama hii. Hata lile jengo la Maktaba Kuu ya Taifa- Barabara ya Bibi Titi jijini Dar Es Salaam haifui dafu na hili! Kwenye blog hii niliwahi pia kupost Maktaba ya Mkoa wa Arusha bure kabisa! Tuamke kila mkoa, taasisi mbalimbali hasa shule kuanzia nursery hadi vyuo vikuu vianze kuboresha au kujenga maktaba za kisasa ambazo zitakuwa visima vya maarifa.
Monday, January 30, 2012
Prof. Apollonia Kerenge
Professor Apollonia Kerenge ni mmoja ya wahadhiri waandamizi na wazoefu katika Chuo cha ESAMI kilichoko jijini Arusha nchini Tanzania. Yeye ni Mchumi kitaaluma na amefanya kazi sehemu nyingi ndani na nje ya nchi. Zaidi amebobea katika masuala ya jinsia na Watanzania wachchache ninaowafahamu ambao wanaweza kutoa uchambuzi wa kina kuhusu masuala ya jinsia na kuweza kukuelekeza inavyoweza kufanyika ili yatumike kwenye sera zetu, mipango yetu ya maendeleo, miradi na bajeti.
Banzi wa Moro wilayani Meru
Na huu ndiyo Mlima Meru
Mlima Meru ni mmoja kati ya milima mirefu nchini Tanzania. Nakumbuka nilipokuwa shule ya msingi tulifundishwa wimbo mmoja kuhusu milima ya Tanzania "Milima ya Tanzania, Kilimanjaro na Meru, Rungwe hata Livingstone, Usambara, Uluruguru na ..... milima ya Iringa! (Pengine hii ndiyo iliyokuwa chachu ya mimi kulipenda somo la Jiografia na hatimaye kusoma combination ya CBG - a.k.a cabbage).
Chuo cha Nelson Mandela
Hiki ni Chuo kipya cha Kimataifa cha Sayansi na Teknolojia kilichopo mkoani Arusha. Chuo hiki kimejengwa pale ilipokuwa CARMATEC.Madhumuni ya Chuo hiki ni kutoa Elimu ya Juu ya Sayansi viwango vya shahada za uzamili na Uzamivu. Uwekezaji unaoendelea katika Chuo hiki ni wa kiwango cha Kimataifa na endapo kitaendeshwa na kutunzwa vizuri kitatisha kwa viwango vya utaalamu.
Matombo Msalabani
Hii ni moja ya alama kuu ya Tarafa ya Matombo-Matombo msalabani. Ukifika Msalabani ni rahisi kwenda Mtamba (Makao makuu ya tarafa ya Matombo), Matombo Mission/Matombo Secondary School, vijiji vya Kibungo, Tawa, Lukenge, Dimilo, Konde, Kitungwa, Lusangalala, Mlono n.k. (hiyo barabara inayoonekana pichani). Picha hii ni zawadi kutoka kwa Bw. Gaitan Banzi aliyekuwa huko nyumbani Matombo kwa likizo. Nami nasema asante kwa zawadi nzuri. Wengi wetu hufikiri zawadi zinazoshikika kama vile maembe, ndizi, kuku, mchele,mashelisheli, mafenesi n.k.Kumbukumbu kama hii ni zawadi ya kudumu . Embe, kuku, 'ubwabwa' utakula utasahau! Tulipokuwa wadogo mimi na kaka yangu marehemu George Banzi tulikuwa tunajiuliza maswali mengi kuhusu msalaba huu. Kaka George alikwenda mbali zaidi akifikiri kuwa huenda Wajerumani wameficha fedha humo ndani! Nangojea zawadi nyingine kutoka Matombo pamoja na ile ya picha ya jiwe la Matombo!
Friday, January 20, 2012
Arusha maarufu kwa ndizi
Thursday, January 19, 2012
Mashamba ya maua Arusha
Tuesday, January 17, 2012
Hajasahau kutengeneza vyombo vya elekroniki
Himili Mbawala ni Mhasibu kitaalamu lakini kabla ya hapo kwa utundu wake tangu alipokuwa mwanafunzi wa shule ya msingi alikuwasambamba na baba yake marehemu Ireneus Mbawala kujifunza ufundi hasa wa redio na baadaye Televisheni. Juzi jumapili aliweza kutengeneza Tv ya mama yake huku mwanae Vanesa akiwa sambamba naye. Je naye atakuwa fundi? Mtoto kama baba kama babu?
Reli bila gari moshi
Mafuriko ya Desemba 2012- Dar Es Salaam
Sunday, January 15, 2012
Hotel 88 Moro
Tofauti na hotel nyingi za ghorofa zilizopo Arusha, mji wa Morogoro una safari ndefu ya kuwa na hotel za hadhi ya kimataifa. Hotel za kwenda juu (ghorofa) ni za kuhesabu. Wakati wa sherehe za kitaifa au kanda si rahisi kwa wageni kupata nafasi ya kulala. moja hotel nzuri karibu kabisa na viwanja vya nanenane morogoro ni Hotel 88
Familia nyingi zitaongeza matumizi ya mkaa
Mtoto anapokuwa pekee
Subscribe to:
Posts (Atom)