Friday, January 31, 2014
Kikundi cha Kuigiza Moro
Nikiwa Morogoro kwenye sherehe za harusi, mara nyingi hukutana na kikundi hiki kinachoigiza muziki wa dansi uliokuwa ukipigwa na magwiji wa muziki huo mjini Moro ambao wote kwa sasa ni marehemu. Nao ni Mbaraka Mwinshehe Mwaruka, Juma Kilaza na Salum Abadallah. Kwa kweli ukiwaona waigizaji hao (pichani) utafurahi hasa kwa wale wenye umri wa miaka 50 na zaidi ya hapo kwani wanaweza kukumbuka enzi zao.
Namezea mate ndafu hii
Jinsi ilivyochomwa. Ndafu hii ilichomwa na mtaalamu kutoka Kilimanjaro anaitwa Joseph. Wachagga kwa kutengeneza ndafu ndo wenyewe. Na ni wakali pia katika kudhibiti matumizi ya fedha. Lakini wanajua jinsi ya kzitafuta. Hii ndafu ilitafumnwa siku ya Boxinga day ya mwaka 2013 huko Mbezi Beach nyumbani kwa mjomba Dr. G.Mluge
Ustaarabu wa Pwani
Ni kuvua viatu. Pwani mchanga ni mwingi kwa hiyo mtu mstaarabu haingia ndani huku akiwa amevaa viatu. Ustaarabu wa watu wa Pwani.
Dada zetu ukumbini Moro
Akina Kimbiki na watoto wao wakijimwaga wakati wa sherehe za kumpongeza kaka yao Richard Banzi mwishoni mwaka jana huko Morogoro
Thursday, January 30, 2014
Waliofanikisha harusi ya Richard Banzi
Kutoka kushoto Faustini Mizambwa, Mrs Mizambwa, Mrs. Kobelo, Mr. Aniani Kobelo (Mwl. Thomas). Anayetambulisha Mama P.Mloka wakati sherehe ya kumpongeza Bw. Richard Banzi kwa kufunga ndoa huko Morogoro Desemba, 2013. Kazi nzuri ndugu zangu HONGERENI.
Whisky inapogeuzwa maji ya kunawa
Kama starehe ndiyo hivi basi laana. Wakati wengine wanatafuta fedha ya chakula, huyu ananawa mikono yake kwa kutumia pombe kali - Whisky!
Uokovu wa kula nyasi
Inasemekana hawa wameokoka na wanasali kwa kula nyasi. Ukiangalia vizuri picha hii wote ni vijana. Hivi kuna nini kinaendelea? Je, ni kukata tamaa ya maisha?
Tuesday, January 28, 2014
WAWATA DEKANIA YA KIGAMBONI
Happy Birth Day Norbert !
Tarehe 26/01/2014 Norbert Macarios Banzi ametimiza mwaka mmoja. Happy birthday Norb. Je, atakuwa dereva?
Ujasiri wa kuchezea nyoka
Wengine wanaogopa nyoka. Lakini kuna dada majasiri wa kucheza ngoma na nyoka hapa nchini Tanzania huu ni utamaduni wetu tuuenzi.
Mama Kikwete hotuba kwa wake wa Mabalozi
Mama Salma Kikwete akitoa hotuba ya kuukaribisha mwaka mpya kwa wake wa Mabalozi nchini Tanzania hivi karibuni.
Kikwete na Ruto
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Ruto Makamu wa Rais wa Kenya hivi karibuni
Magufuli ndani ya mtambo kwenye eneo la darala la Dumila
Waziri wa Ujenzi Mhe. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya mtambo wa kujaza kifusi kwenye daraja lililoharibiwa na mafriko huko Dumila, Kilosa, Morogoro.
Hivi ndivyo daraja la Dumila lilivyochimbika
Daraja lilichimbwa mwanzo na mwisho hivyo kulifanya lisipitike baada ya mvua kubwa kunyesha wilayani Kilosa mkoani Morogoro hivi karibuni.
Ibrahimu Masoud akimhoji Sumaye
Mtangazaji maarufu wa michezo wa Clouds alipata fursa ya kumhoji Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Sumaye wakati alipotembelea studio za kituo hicho hivi karibuni. Masoud alimuuliza swali la kizushi Mhe. Sumaye mapenzi yake kwa Club ya Simba ya mtaa wa Msimbazi maaelezo zaidi sina.
Kikwete ashangiliwa Switzerland
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akishangiliwa baada ya kutoa hotuba yake mjini Davoos, Switzerland.
Pokea hati ya kuboresha jeshi la Polisi
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mathias Chikawe akipokea hati ya kuboresha Jeshi la Polisi nchini Tanzania.
Nasikia 'Lulu' amepata mchumba
Huyu ndiye Elizabeth Michael a.k.a Lulu aliyepata kashikashi ya kifo cha Kanumba. Ni mcheza filamu maarufu hapa Tanzania. Tetesi ni kwamba Lulu amepata mchumba
Hiyo ndiyo bodaboda bwana
Waw! Bodaboda abiria 8! Hata gari ndogo aina ya Toyota haiwezi kubebe abiria wengi kiasi hicho. Lakini abiria wameufurahia usafiri huo!
Adha ya ujenzi wa barabara ya mabus yaendayo kasi DAR
Mpaka itakapokuwa imekamilika. Ujenzi wa barabara ya mabus yaendayo kasi jijini Dar utakuwa umewatesa wengi na kwa kweli wachumi tunaweza kukokotoa gharama ya matumizi ya mafuta na kuchelewa kazini wakati wote wa ujenzi wa barabara hiyo/hizo. Tutashangaa!
Subscribe to:
Posts (Atom)