Tuesday, October 3, 2017

Masista wanafunzi (Novisti) wa Shirika la  Carmel,Vikindu, Jimbo Kuu la Dar Es Salaam wakicheza ngoma siku ya mahafali ya wanafunzi wa darasa la saba wa  shule ya Msingi ya Carmel ya Vikindu.

Shukrani iliyoniliza

Ilikuwa zaidi ya shukrani. Pale Dada Slyvia Daulinge, mtoto kitinda mimba wa Bw & Bi. Nestory Daulinge alipotoa shukrani kwa wote waliomhangaikia marehemu Baba yao Mzee Nestory Daulinge hadi kuzikwa kwake. Ilituliza wengi hata kama ni kimyakimya. Hii ilikuwa kabla ya mazishi tarehe 5 Septemba 2017 kule Matombo, Morogoro

Hapa ndipo alipopumzika Mzee Nestory Augustino Daulinge

Dada watatu kutoka Kushoto Slyvia Daulinge,Edditruda Daulinge na Restituta Daulinge wakiwa na mtoto wao baada ya tendo la kumzika baba yao Mzee Nestory Augustino Daulinge tarehe 5 Septemba 2017 nyumbani Matombo, Morogoro.
Wamasai wanapendeza wakiwa na vazi lao la asili wakimlaki Rais wetu Mhe. John Pombe Magufuli. Hivi mchakato wakuwa na vazi la taifa imefikia wapi? Tusiangalie rangi, tutakwama.Tuangalie design.