Wednesday, September 28, 2016

Hili ni group langu nililosoma nalo nchini Urusi

Hili ni group langu la masomo nilipokuwa nchini Urusi kwa masomo yangu.Katika Group hili nawakumbuka wachache kwa majina hasa hao waafrika kutoka kushoto Mamadu (Mali) Mohamed Barrie (Sierra Leone), Mansary (Sierra Leone) na Alex Konte (Siera Leone). Mimi niko mkono wa kushoto wa Mamadu. Hapa ilikuwa ni Crimea, Simferopol mwaka 1989. Nadhani wa kwanza kushoto ni Kutryova na kushoto kwangu ni Svetlana.

Huyu ndiye Ibrahim Ajibu wa Simba

Ibrahim Ajibu wa Simba Sports Club (Nyekundu) akiruka kiunzi wakati wa mpamboa wa klabu yake na AFC-Leopards kutoka Kenya-Tarehe 8/8/2016 katika uwanja wa Taifa, Dar Es Salam. Leopards ilala 4-0. Ni katika kuadhimisha miaka 80 tangu kuanzishwa kwa klabu ya Simba ninayoipenda mimi!

Bright Angels-High School ziara ya mafunzo-Mafia

Wanafunzi wa Bright Angels High School iliyopo wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani wakiwa katika ziara ya mafunzo huko Mafia wakiangalia mabwawa ya kutengeneza chumvi.

Miaka 80 ya Simba Sports Club nilikuwepo uwanjani

Nilikuwepo uwanjani pamoja na mashabiki lukuki wa Simba nikimshuhudia mnyama akimrarua AFC Leopards ya Kenya mabao 4-0 kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar Es Salaam. Wote tukiimba kila mtu 'Mavugooo'. Mchezaji huyu wa Kimataifa kutoka Burundi,  Laudit Mavugo alitupia bao katika mechi yake ya kwanza akiichezea SSC. Ilikuwa raha sana. Nimeweka kumbukumbu ya kuhudhuria mechi ndani ya uwanja wa Taifa wakati Simba inatimiza miaka 80 tangu ianzishwe.

Thursday, September 22, 2016

Milima ya Nyingwa-Matombo-Morogoro

Hii ni milima ya Nyingwa, Matombo-Morogoro

Matombo-Lanzi

Mandhari mazuri ya kijiji cha Lanzi,Kibungo, Matombo, Morogoro. Angalia mgahawa kando ya barabara. Kwetu kuzuri.

Hii ndiyo Kamati ya Harusi

Ukisikia kamati ndiyo hii. Hongera!

Maharusi wamechagua kibanda wazi

Hawa ni wadogo zetu Waluguru kutoka Matombo Kiswira waliofunga ndoa hivi karibuni. MC alikuwa Richie Paschal. Kwa mujibu wa Richie harusi ilifana sana.

MC. Mluguru Richie Paschal Solaga

Kwa Waluguru wanaotaka shughuli zao ziendeshwe kwa lugha ya Kiluguru basi itabidi umtafute MC. Richie Paschal Solaga. Ana  kipaji cha hali juu na anajua kuchangamsha shughuli. Hata kama si kwa Kiluguru yupo vizuri sana kwani anajua vikorombwezo. 

Kunywa maziwa kutoka Meatu

Nadhani somo limeeleweka na limekubalika. Mkuu wa Mkoa wa Shimiyu Mhe. Anthony Mtaka akionyesha  maziwa ya Meatu. Hakika inafurahisha na inapendeza. Cha kufurahisha Maziwa hayo yanatengenezwa na mradi wa vijana. Hivyo ni moja ya vyanzo vya ajira na mapato kwa vijana.(Picha kwa hisani ya Michuzi Blog)

Tutumie vya kwetu- Chaki kutoka Maswa

Mkoa wa Simiyu umeanza kutengeneza chaki kutoka Maswa. Tupende na kutumia vya kwetu. Inakuwawaje hata chaki tuagize kutoka nje? Pichani Mkuu wa Mkoa wa Simiyu  Mhe. Anthony Mtakwa akishangaa Chaki kutoka Maswa mali ya Tanzania.

Thursday, September 15, 2016

Unapoitaja Matombo unagusa matunda na machenza

Machungwa na machenza ya Matombo, Morogoro ni matamu sana. Tatizo wafanyabiashara wameingilia kati biashara hii na kuyauza machenza na machungwa wakati bado hayajafikia kukomaa kibailojia (Yanakomaa yakiwa mtini). Kibaya zaidi huchanganya machungwa au machenza mazuri na mabaya. Mlaji akibahatika hula chenza tamu na ikiwa hana bahati unaweza kula chenza chungu. Hii ni kuharibu biashara na umaarufu wa machungwa au machenza ya nyumbani Matombo. Kwa kawaida machungwa huanza kuvunwa kuanzia mwezi machi hadi Juni.

Athari ya Tetemeko la Ardhi Bukoba

Tetemeko la Ardhi lililotokea Bukoba.Baadhi ya nyumba za Ibada zimeathirika.Kanisa Katoliki Ihungo limeharibiwa vibaya. Poleni sana wenzetu wa Bukoba.(Picha kwa hisani ya ukurasa wa fb. Askofu Method Kilaini).

Tuangalie ugonjwa wa nyanya kuoza kitako (Blossom endrot)


Baadhi ya wakulima wa nyanya wamekuwa wakipata tatizo la nyanya zao kuungua chini ya kitako na kuharibu kabisa ubora wa nyanya hizo. Wanataalamu wanatueleza kuwa ugonjwa huo unaitwa kuoza kitako (Blossom endrot). Hii husababishwa na mmea kukosa maji ya kutosha au kutofuata ratiba ya umwagiliaji kwa zao hilo.Unakuta siku nyingine unamwagilia asubuhi siku nyingine mchana au unamwagilia Jumamosi halafu unarudia tena kumwagilia siku ya Jumanne huko ndiko kutozingatia ratiba ya umwagiliaji. Hiki ndicho chanzo kikuu cha ugonjwa huo wa kuoza kitako.
 
 TIBA

Ondoa matunda yote yaliyo athirika halafu anza kufuata na kuzingatia ratiba ya umwagiliaji wa shamba lako.
(Hii nimeinyaka kutoka fb wafanyakazi wa kilimo Mifugo na uvuvi na kuikarabati kidogo na kuirusha kwani ni wengi wanalima nyanya na hasa na kuwaona wanamwagilia maji kiubabaishaji tu).

Wednesday, September 14, 2016

Bus la Yutong la Wachina

Hili ni bus la Yutong la kutoka Uchina. Utawapenda tu. Wachina ni wazuri kwa teknolojia.  Hutengeza kuteka matakwa ya mdau. Hapa Tanzania kwa sasa naweza kusema kuwa asilimia 80 ya mabus ni  ya Kichina. Inasemekana ni bei poa ukilinganisha na mabus aina ya Scania au Marcopolo. Kingine wanachofanya  Wachina ni kuongeza thamani ya bidhaa. Ukipanda mabus yao yalivyorembwa na kuwekewa vikorombwezo vingine hakika hutoacha kulipanda tena. Sisi tutaanza lini kuunda mabus yetu?

Nani Zaidi?


Haya ni machenza kutoka Matombo - Morogoro

Machungwa na machenza ya Matombo, Morogoro ni matamu sana. Tatizo wafanyabiashara wameingilia kati biashara hii na kuyauza machenza na machungwa wakati bado hayajafikia kukomaa kibailojia (Yanakomaa yakiwa mtini). Kibaya zaidi huchanganya machungwa au machenza mazuri na mabaya. Mlaji akibahatika hula chenza tamu na ikiwa hana bahati unaweza kula chenza chungu. Hii ni kuharibu biashara na umaarufu wa machungwa au machenza ya nyumbani Matombo. Kwa kawaida machungwa huanza kuvunwa kuanzia mwezi wa Machi hadi Mei.

Kumbukumbu harusi ya uncle Sophy Mluge

Ushiriki wa madada na makaka kwenye harusi hii iliyofanyika mjini Morogoro  ulikuwa wa hali ya juu. Hii ni kumbukumbu ya zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Nimeikumbuka shule yangu ya Msingi Matombo

Nimeikumbuka shule yangu ya Msingi Matombo. Hivi sasa ni shule ya Sekondari Matombo. Kuna mchakato unaoendelea kuifanya iwe High School (Form I-VI) haya ni mabadiliko makubwa.Kitu kimoja nakumbuka nilikuwa mpiga kengele.

Friday, July 1, 2016

Mc POLD wa Ukweli

MC  Leopold ni mshehereheshaji anayechipukia katika Jiji la Dar Es Salaam. Anapatikana zaidi maeneo ya Magomeni. MC asiyekuwa na Makuu, Kijana na anayeitendea vyema kazi yake. Mawasiliano hayo hapo. Na mweleze umemuona kwenye Banzi wa Moro. Hahaha.

Mji kasoro Bahari- Moro - 2016

Hiki ndicho keepleft cha Msamvu, Morogoro

Utafiti wa mbolea unaofanyika ARI-Mlingano

 Ukitaka kuingiza mbolea mpya nchini lazima ifanyiwe utafiti kuona kama inafaa na haina madhara. Huu ni utafiti wa mbolea angalia tofauto. Mkono wa kushoto wameweka mbolea inayofanyiwa utafiti. Kati kati hakuna mbolea.

Je, ukipata mlo huu asubuhi utajisikiaje?

Nimevutiwa na mlo huu, chips, mishkaki, juice saladi. Aah lazima afakamie tu.

Yanga Vs TPMazembe- Tulishangilia lakini Yanga ilipoteza pointi 3

Mechi ya Yanga na TP Mazembe Uwanja wa Taifa  tarehe 28/6/2016. Tulishangilia wote hata hivyo yanga ilipoteza pointi tatu kwa kufungwa bao 1-0
Picha zote kwa hisani ya Michuzi Blog

Tuesday, June 21, 2016

Kilimo cha bamia kama ufugaji wa kuku wa mayai!

Kitu ambacho nilikuwa sifahamu ni jinsi unavyoweza kuvuna bamia. Bamia linaweza kuvunwa mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni. Kuna mtu ameninong'oneza. Bamia wakati wowote hukua, tena kwa haraka ukichelewa linakomaa na hivyo kuwa gumu na kutofaa kuliwa kama mboga labda kulitunza kwa mbegu.Hivi sasa navuna bamia katika sehemu ndogo niliyolima pale nyumbani kwangu Kisemvule. Kweli kilimo cha bamia ni kama ufugaji wa kuku wa mayai.


Thursday, May 19, 2016

Tanzania imepania kuongeza uzalishaji wa mpunga

Mpunga ni zao linalostawi vizuri katika sehemu nyingi za nchi yetu hasa ukanda wa pwani na mabonde yanayozunguka maziwa yetu na inakopita mito mikubwa. Wakulima wengi huzalisha wastani wa tani 2 kwa hekta ambapo ni kidogo sana. Utafiti uliokwishafanyika hapa nchini unaonyesha kuwa kwa kutumia teknolojia bora za kilimo cha mpunga, uzalishaji unaweza kufikia tani 8
kwa hekta. Hivi sasa serikali inaboresha kilimo hicho kupitia miradi mbalimbali hasa kwenye skimu za umwagiliaji.

Ni changamoto

Wapenzi wa Banzi wa Moro nimerudi kuwajuza.
Inapotokea kuwa na njia mbalimbali za kupeana habari na msambazaji habari ni huyohuyo ni changamoto kwa kweli. Kuingia kwa facebook na whatsapp kwa kweli kumeimomonyoa blog yangu. Inakuwa vigumu kupost kwenye blog. Naweza kupost kutoka whatsapp kwenda facebook tukio hilohilo lakini siwezi kufanya hivyo kwenda kwenye blog. Uzuri wa whatsapp na facebook ni rahisi kupata feedback hivyo kukufanya kuandika na kupost. Hata hivyo nimerudi, nitaanza kuning'iniza kadri ninavyoweza nipatapo wasaa.
Dereva Mwandamizi wa Idara ya Utafiti na Maendeleo Ndg.Shushu Kondowe akiwasilisha taarifa ya mafunzo kwa mratibu wa mafunzo Bw. John Banzi

Wednesday, March 2, 2016

Wataalamu wa ERPP ofisini Mvomero

Mradi wa kuongeza uzalishaji wa Mpunga (ERPP) umeshaanza. Mradi huu utatekelezwa katika wilaya tatu za mkoa wa Morogoro (Mvomero,Kilosa na Kilombero). Skimu za umwagiliaji zitahusika nazo ni  Kigugu, Mbogo-Kamtonga, Mvumi, Njage na Msolwa. Pichani wataalamu wakielezea jinsi mradi huo utakavyotekelezwa ndani ya ofisi ya Mkurugenzi wa Maendeleo Halamshauri ya Mvomero (Haonekani).

Ifakara ya 2016 inang'ara

Hii ni moja nyumba ya kulala wageni iliyopo mjini Ifakara.m Miaka 10 iliyopita mji wa Ifakara ulikuwa na nyumba chache za kulala lakini hivi sasa nyumba za aina hii ni nyingi tu. Hebu fikiria pango la chumba kwa usiku mmoja ni Tsh 15,000/= huku ukila raha ya TV ya bapa!

Padri Abdoni Antipas Nzegesela akisoma Injili

Padri Abdoni Antipas Nzegesela ni Paroko wa Parokia ya Ilonga iliyoko Kilosa- Kanisa Katoliki jimbo la Morogoro. Pichani anaonekana akisoma Injili ndani ya Kanisa Katoliki Vikindu, Jimbo Kuu la Dar Es Salaam. Ndiye aliyefungisha ndoa ya Bw. Macarios Banzi na Bi. Martina Jeremias siku ya tarehe 6/02/2016

Bango bora la Shule ya Msingi Kisemvule

Huenda likawa bango bora kabisa kwa shule za msingi za wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani. Ni shule ya msingi Kisemvule. Kila kitu kiko wazi.Huu ni ubunifu wa mwalimu mku wa shule hiyo ambaye amehamishiwa hapo shule hivi karibuni. Nilipouliza gharama ni Tshs 150,000/= na kiasi kikubwa cha fedha kimetolewa na Serikali ya Kijiji cha Kisemvule. Hongera Mwenyekiti na Kamati yako ya Kijiji. Kujitangaza ni maendeleo pia!

Skimu ya umwagiliaji ya Msolwa kuboreshwa

Wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakikagua skimu ya umwagiliaji ya Msolwa iliyoko wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro ambayo kupitia Mradi mpya wa " Expanded Rice Production Project" ulioanza kutekelezwa mwaka 2015/16  ni moja ya skimu zilizo kwenye mpango wa kuziboresha ili ziweze kuongeza uzalishaji wa mpunga nchini.

Samaki-Faida inayoweza kupatikana kwenye skimu za umwagiliaji

Hivi karibuni nilitembelea skimu ya umwagiliaji ya kijiji cha Msolwa kilichoko wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro. Nilishangaa kuwaona watoto hawa wakivua samaki kwenye skimu hiyo. Hii ina maana kuwa kwenye skimu za umwagiliaji, wakulima wanaweza kutenga sehemu na kuwa na mabwawa ya kufuga samaki  na kujipatia kitoweo pamoja na mapato kwa kuuza samaki hao.

Saturday, February 27, 2016

Sh2-Mdundo bila umeme












Wote hawa wanafurahi mdundo wa ngoma ya Kiluguru iitwayo shilingi 2. Hii ngoma ilitumbuiza siku ya harusi ya Bw na Bibi  Macarios  Banzi. Kikundi hiki ni cha watu sita na kila mmoja hupiga,huimba na kucheza. Kwa kawaida hupiga ngoma kwa muda mrefu na hubadilisha midundo mumo kwa mumo. Unacheza upendavyo. Hiyo ndiyo shilingi 2 mdundo bila umeme wala amplifier!