Thursday, February 14, 2013

Msongamano wa magari Dar

Jijini Dar msongamano wa magari ni mkubwa na ni kero. Hii inasababishwa na mambo mengi moja ni ujenzi wa barabara unaofanyika hasa barabara ya mabasi yaendayo kwa kasi!

Kanisa la Magomeni -Sura Mpya

Jengo la Kanisa Katoliki Parokia ya Magomeni, Jimbo Kuu la Dar Es Salaam linakarabatiwa upya. Kwa sasa paa lake limeezekwa katika mtindo wa kisasa kabisa. Ukarabati unaendelea. Familia yetu ina historia nzuri katika kanisa hili.Hapa ndipo nilipopata skaramenti yangu ya ndoa mwaka 1997.

Ilipo Wizara ya Maendelo ya Mifugo na Uvuvi

Kama ilivyo kwa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika. Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi nayo iko wilaya ya Temeke eneo la Veterinary karibu na Stesheni ya TAZARA.

Makao Makuu ya Mamlaka ya Bandari Tanzania

Hapa ndipo yalipo Makao Makuu ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),Kurasini, Dar Es Salaam. Bandari ni moja ya chanzo kikubwa cha mapato ya serikali hapa nchini.

Ujuzi popote

Kijana huyu anahamu ya kufahamu kutumia kompyuta. Banzi wa Moro alimkuta akijifunza kompyuta pale Magomeni karibu kabisa na Kanisa Katoliki. Ndivyo inatakiwa,ujuzi popote.

Wednesday, February 13, 2013

Uchaguzi wa Kamati Kuu ya CCM

Mambo yanavyokwenda kwenye mkutano wa kuwachagua wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM huko Dodoma ni ajabu na kweli.Waliotegemewa sana hawamo!(Picha kwa hisani ya gazeti la DailNews-Tanzania 13/02/2013)

Huenda akawa Baba Mtakatifu

Huenda Kadinali Peter Tukson (alisimama) kutoka Ghana akawa mwafrika wa kwanza kuwa Baba Mtakatifu kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani baada ya Baba Mtakatifu Benedict XVI kutangaza kujiuzulu jana.

Tuesday, February 12, 2013

Mlima Meru

Mlima Meru unavyoonekana ukiwa pale Soweto Club jijini Arusha.

Vyoo vya Highway hotel Korogwe

Hili ni jengo la vyoo vya Highway hotel Korogwe. Vyoo hivi ni visafi sana na huduma ya maji hupatikana wakati wowote inapotakiwa na wasafiri. Ni moja ya hotel zinazotoa huduma bora za vyoo kwa wasafiri hapa nchini.

Hawa ni ndugu

Ali Mhanndo na Abdallah Mhando ni ndugu wanaoishi Arusha lakini ni Wazaramo. Ndugu hawa wamejaliwa kipaji cha kunyoa (Barbers) kwa sasa Bw. Abdallah anafanya kazi katika Barber shop moja ijulikanayo kwa jina la Big L jijini Arusha karibu kabisa na Hospitali ya KKT pale Selian.

Napenda kusoma magazeti

Kama kuna kitu ninachopenda basi ni kusoma magazeti.

Sehemu sehemu za Jiji la Arusha

Waliokwisha tembelea Jiji la Arusha nielezeni hapo ni wapi?

Kutoka kwenye Jumuiya Ndogondogo

Wakati mwingine inabidi utembee kando kando ya kuta kuzifikia Jumuiya Ndogondogo

Papa Benedict XVI ajiuzulu

Tarehe 11 Februari, 2013, Pope Benedict XVI kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani ametangaza kujiuzulu wadhifa huo kuanzia tarehe 28/02/2013.
(Picha kwa hisani ya Reuters)

Monday, February 11, 2013

Nje ya uwanja wa TAIFA-Dar Es Salaam

Uwanja wetu mzuri wa Taifa umeanza kutuletea mafanikio, ndani ya uwanja huo ulipo kwenye Manispaa ya Temeke Jijini Dar, Zambia na Cameroon zimechinjwa!

Twiga yake majani ya nchani

Urefu wa twiga humsaidia sana kula majani ya nchani ambayo ni machanga.

Nyamachoma ya ukweli

Hii ndiyo nyamachoma 'original.'

Nigeria Bingwa 2013

Bingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2013 ni Nigeria. Imetwaa ubingwa baada ya kuilaza Burkinafaso bao 1-0 lililofungwa na mchezaji Sunday Mba katika kipindi cha Kwanza. Kocha mzawa Stephen Keshi aliyewahi kuichezea Super Eagles mwaka 1994 na kutwaa ubingwa wa Afrika ndiye aliyeiongoza Nigeria katika michuano hiyo.

Wakulima wafuatwe shambani

Bi. Mary Ndomba (kulia) ni mtafiti wa kituo cha Utafiti wa Kilimo Tumbi, Tabora. Wakati wa mafunzo yake ya shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Ndomba alifanya utafiti shambani mwa wakulima.

Tatizo la muhindi huu ni nini?

Wataalamu wa kilimo tuambieni tatizo la mmea huu wa mahindi.

Kitambulisho cha Taifa hiki hapa

Kitambulisho nambari 1 ni cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete

Vyama vya Siasa vyenye sauti Tanzania

CCM na CHADEMA ni vyama vyenye sauti kubwa na mvuto nchini Tanzania.Lolote au chochote wakifanyacho hupewa nafasi kubwa na vyombo vya habari. Jana CHADEMA walikuwa jijini Dar pale TEMEKE mwisho wakati CCM wao wako DODOMA ni katika harakati za kuchukua DOLA!

Thursday, February 7, 2013

Maria yuko Darasa la pili

Maria Banzi mwaka huu ameingia darasa la pili. Kweli ana safari ndefu.

Tutumie makazi yetu kuotesha mboga

Tukitumia makazi yetu vizuri tunaweza kuotesha mboga mboga kwa ajili ya chakula na kuongeza kipato pia ni njia nzuri ya kuwafanya watoto wetu wapende kazi hasa za kilimo.

Aliyeiua Cameroon

Huyu ndiye Mbwana Samata (aliyemiliki mpira) aliyeiua Cameroon jana kwenye uwanja wa Taifa. Siku zote ninasema hakuna kisichowezekana na si kweli kuwa nchi nyingine za Kiafrika hata dunia zinatupita sana kiuchezaji. Tatizo tulikuwa hatujajipanga, hatujitambui na hatujiamini. Sasa tumeanza kujipanga, tunajitambua,tunajiamini. Na ndiyo maana katika kipindi kifupi tumeweza kuzifunga Zambia na Cameroon zinazosemekana kuwa ni vigogo wa soka barani Afrika. Ndiyo, tuanze sasa kuvaa sare za akina Mbwana Samata, Frank Dumayo, Juma Kaseja na wengine. T
uwatangaze wachezaji wetu na kutangaza soka la Tanzania.

Adha ya kuendesha gari jijini Dar

Hakuna kinachokera jijini Dar kama kuendesha gari kwenye msururu mrefu wa magari. Inachosha, inasababisha mafuta kutumika kwa wingi, inasababishwa kuchelewa sehemu uliyokusudia kwenda, wakati mwingine wezi hupata fursa ya kuiba ndani ya magari endapo ukijisahau.

Limetoka bandarini

Malori haya yametoka bandarini yakiwa yamebeba shehena ya bidhaa zinazosafirishwa kwenda nchi za nje. Bandari yetu ikitumika vizuri na kufanya kazi kwa tija itaongeza pato la Taifa na kuinua uchumi wa nchi.

Kuna mategemeo ya kula nazi

Iko siku nitakula nazi kutoka mnazi huu. Hivi sasa bei ya nazi jijini Dar haikamatiki, ni kati ya Tshs 600/= hadi Tshs 1000/= kwa nazi moja. Wali na maharagwe yaliyoungwa kwa nazi ni mtamu sana hasa kipolo chake ambacho ndugu zangu Waluguru wanakiita 'bandula!'

Hospitali ya Mbagala Rangi3

Hospitali hii ya kisasa imezunduliwa rasmi mwaka jana baada ya kuboreshwa kwa msaada Kutoka Serikali ya Korea Kusini. Hospitali hii iko kando ya barabara ya Kilwa maeneo ya Zakhem.

Ni hili ndilo bamia

Nimejitosheleza kwa kustawisha bamia.

Nimejaribu kupanda mboga za maboga

Hapa Kisemvule nimejaribu kupanda mboga za maboga ingawa si eneo kubwa kwa sababu mimi ni mpenzi sana wa mboga ya maboga iliyochangwa na bamia.Waswahili wanasema raha jipe mwenyewe!

Mboga kutoka bonde la Chang'ombe

Kwa miaka mingi bonde la Chang'ombe limekuwa likistawisha aina mbalimbali za mboga zikiwemo bamia, mboga za mabgoa, na mchicha. Wakazi wengi wa Jiji la Dar Es Salaam hutegemea bonde la Chang'ombe kwa mboga. Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ikiandaa Mpango Mkakati wa Kilimo mzuri wa jinsi ya kulitumia bonde hilo kwa shughuli za bustani mabadiliko makubwa ya uzalishaji wa mboga zilizo na ubora na uwingi wa kutosha kwa matumizi ya wakazi wa jiji la Dar utapatikana. Hii pia itawaongezea kipato wazalishaji wa mazao ya bustani katika bonde hilo.

Mbagala R3

Acha kabisa. Mbagala ya sasa siyo ile ya zamani. Ghorofa zimeanza kuchipuka na barabara iboreshwa, foleni za magari hutokea kwa nadra sana.Tunaweza kusema kuwa Mbagala Rangi 3 ni kichocheo cha maendeleo ya mikoa ya kusini.

Hapa ndipo 'Kempski'

Siku za kazi wakati wa mchana ukinipigia na nikakujibu kuwa niko 'Kempsiki' basi ni hapa.Ukiwa 'Kempsiki' unapata vyakula vya leoleo. Kuanzia samaki aina ya changu,kibua pamoja na mboga za maboga, tembele, kisamvu, bamia na maharage, nyama za kukaanga, wali kwa nazi na ugali wa kuviringwa. Huduma zake ni poa pia hapa hakuna daraja! Bei zake pia ni kivutio cha wateja. 'Kempsiki' inapatikana karibu kabisa na yalipo Makao Makuu ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika wailaya ya Temeke, maeneo ya Veterinary ni jirani pia na ofisi za usafirishaji ya Kampuni ya DANDHO.

Bahari yetu ya Hindi

Tanzania tumebahatika kuwa na bahari ya Hindi (Indian Ocean). Bahari hii hutumika kusafirisha abiria pia bidhaa ndani na nje ya nchi.Bahari ni makazi ya viumbe wa majini kama vile samaki ambao hutupatia kitoweo pamoja na kuingiza kipato. Bahari ni kivutio cha watalii. Maji ya bahari hutumika pia kutengeneza chumvi. Faida tuzipatazo kutokana na bahari ni nyingi hizi ni baadhi tu.

Wednesday, February 6, 2013

Bakhresa anavyotangaza bidhaa zake

Hivi ndivyo Mohamed Bakhresa anavyotangaza bidhaa zake. Bango hili linaonekana pale TAZARA - Traffic lights

Nyumba za TAZARA

Hivi ndivyo Banzi wa Moro alivyozikuta nyumba za TAZARA pale Temeke Veterinary jijini Dar. Zimechoka ile mbaya. Hakuna kupaka rangi wala nini. Lakini enzi zake walipokuwa wanakaa Wachina zilikuwa babukubwa. Nasikia nyingi kama si zote zimeshauzwa kwa wafanyakazi wa TAZARA.

Bei ya mafuta jijini Dar - Leo

Hivi ndivyo bango la Oil com lilivyosomeka kuhusu bei ya mafuta jijini Dar hii leo.

Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika

Wizara ya Kilimo inapatikana jijini Dar, wilaya ya Temeke kandokando ya Barabara ya Mandela karibu kabisa na Stesheni ya Tazara.

Friday, February 1, 2013

Hatufuatilii mijadala

Pamoja na kuwa na luninga zenye ving'amuzi majumbani kwetu lakini nibaini kuwa tulio wengi hatufuatilii mijadala inayoendeshwa luningani.

Tunachambua mbaazi

Mbaazi mbichi ni mboga nzuri sana hasa ikipikwa na nazi na kisha ukala na wali ni utamu mpaka kisogoni. Lakini mbaazi zikikumaa halafu ukala na ugali wa mtama hapo shughuli ni pevu na kwakweli chakula hiki mimi sikipendi!

Dar kweupe

Kuna mitaa katika jiji la Dar Es Salaam, Tanzania haina msongamano wa watu hasa siku za mapumziko kama Banzi alivyoukuta mtaa huu maeneo ya posta tofauti kabisa na hali ilivyo kwenye mtaa wa Kongo pale Kariakoo.

Alipokuwa 'Form One'

Mwaka huu 2013 Catherine Banzi ameingia 'Form II' Pichani Cathy alipokuwa 'Form I' Kweli miaka inakwenda. Mwezi Januari umekuwa mchungu kwa wazazi wengi kwa ajili ya kulipia gharama za watoto wao wanaosoma. Hata hivyo tusisikitike sana kwani ni muhimu kuhakikisha kuwa watoto mtoto wako anapata elimu nzuri itakayomsaidia kumudu maisha yake.

Gari yahitaji kukaguliwa

Baadhi yetu wanamiliki na kuendesha magari lakini ni wangapi wanapata muda wa kukagua magari yao ili kuhakikisha kuwa ni salama? Mara nyingi ajali nyingi hutokea kwa kuwa magari ya hitilafu fulani. Ni vyema kukagua, tairi,mafuta, oil, maji, na betri kabla ya kuanza kuendesha gari.

Wapi hapa?

Shughuli hii ilifanyika takribani miaka 3 iliyopita. Hii ndiyo raha ya shughuli za kijijini.