Tuesday, April 30, 2013

Mtoto makini

Yusra ni mtoto wa Kitanzania ni mjanja na makini kama anavyoonekana pichani.

Mmea unaotegemea majani kama mizizi

Unaweza kuuona mmea huu ukibahatika kutembelea kituo cha Utafiti wa Kilimo Kibaha kilichopo mkoa wa Pwani. Mmea huu una physical features za kushangaza. Kile kinachoonekana kama majani kimejichimbia ardhini kama mizizi. Ni mmea wa ajabu na aina yake.

Hospitali ya Muhimbili-Watoto

Watoto wanapendwa na tunawajali pia. Hili ndilo jengo jipya la wodi ya watoto hospitali ya Muhimbili. Jengo hili kwa kweli ni safi. Ndani ya jengo kuna facilities mbalimbali kama vile vyumba vya kucheza, kula n.k.

Kuelekea SRI-Kibaha

Barabara hii inaelekea kwenye kituo cha Utafiti wa kilimo Kibaha, Pwani kinachojulikana kama SRI-Kibaha.

Tunahesabu kura hadharani

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Walei Parokia ya Vikindu Bw. Faustini Onyango (mwenye shati jeusi) pamoja na msimamizi wa uchaguzi kutoka Parokia ya Mbagala wakihesabu kura hadharni wakati wa uchaguzi wa viongozi wa Parokia ya Vikindu uliofanyika hivi karibuni.

Toto tundu!

Mtoto huyu ametoka kanisani ili achezee baiskeli. Hebu fikiria kama itatokea baskeli kumwangukia si itakuwa balaa? Kweli ni toto tundu.

Mtoto kanisani

Ni kweli mtoto huyu yumo ndani ya kanisa lakini ni vigumu kuamini kama anafuatilia ibada. Angalia jinsi anavyocheza na tawi kanisani.Tuwafundishe watoto wetu kufuatilia ibada kwa makini wawapo kwenye nyumba za ibada.

Kwa waliokwishafika Dodoma

Saturnight Bar!

Vivalo vya vijana

Haya ndiyo mavazi wayapendayo vijana.

Mr & Mrs Mangengesa Mdimi-Miaka 40 iliyopita

Bw. na Bibi Mangengesa Mdimi siku ya kufunga ndoa kwenye kanisa Katoliki Mt.Paul - Matombo Morogoro. Miaka 40 imeshapita tangu kutokea kwa tukio hilo. Kweli miaka imepita wakati huo picha za rangi hazikuwepo, hakukuwepo na video pia! Lakini mambo yalikuwa mazuri sana na tabasamu mdomoni.Hivi sasa wana watoto na wajukuu.Tarehe 21/04/2013 Mama Dolorose Mdimi ametimiza miaka 60 tangu azaliwe. Mzee Mangengesa Mdimi ni Mwandishi Habari veteran.Hongera sana baba na Mama. Mungu awajalie maisha marefu.


Tuesday, April 23, 2013

Kilima cha Mawasiliano Dodoma

Kilima hiki kinapendwa na wamiliki wa kampuni za simu. Minara ya Voda, Airtel, Zantel na Tigo ipo hapa.

Medical Centre of Excellence-Dodoma

Kituo Mahiri cha Tiba kinaendelea kujengwa mjini Dodoma pembezoni mwa reli ya kati karibu kabisa na Kanisa Katoliki Mt. Paul wa Msalaba.

Elimu haina mwisho

Dr. Kafiriti (Zonal Director)na Dr.Masawe (Cashew Research Programme Coordinator) wa kituo cha utafiti Kilimo Naliendele kanda ya kusini wakifuatilia kwa makini mafunzo ya kuandaa Bajeti yaliyofanyika kituoni hapo hivi karibuni.

Daladala -Maelezo mlangoni

Kabla ya kupanda daladala za mjini Dodoma soma maelezo mlangoni. Moja ya maelekezo-Abiria anatakiwa kukaa katika mstari wakati wa kupanda gari.

School Bus - Dodoma

Hata Dodoma kuna 'minibuses'safi za kusafirisha wanafunzi.

Dodoma mambo safiiiii

Barabara ya Mwanza inavyoonekana sasa mjini Dodoma.

Watoto wa Utatu Parokia ya Vikindu

Watoto wa Utatu mbele ya Altare.

Monday, April 22, 2013

Wanawake na Utafiti Uhandisi Jeni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kutoka kwa mtafiti mwanamama wa kituo cha Utafiti wa Kilimo Mikocheni-Dar Es Salaam.

Kikwete na utafiti katika kilimo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia kwa makini mimea inayozalishwa kwa njia ya 'tissue culture' katika maabara ya Uhandisi Jeni iliyoko katika kituo cha Utafiti Mikocheni- Dar Es Salaam.

Mfugaji akitoa maelezo kwa wataalamu

Mfugaji Mama Kileo akitoa maelezo kwa timu ya wataalamu wa kilimo na mifugo wakati walipomtembelea kuona jinsi anavyoendesha shughuli zake za ufugaji.

Ofisi za Azam Ferries - Dar es Salaam

Hii ndiyo ofisi ya Boti ziendazo kwa kasi za Azam iliyopo jijini Dar Es Salaam kanda kabisa ya Bahari ya Hindi.

Mikoba na masanduku ya safari uwanjani Mtwara

Na langu lipo likisubiri kuwekwa ndani ya ndege ya Precision kusafirishwa kwenda Dar.

Bango la Pepsi-Dodoma

Hivi ndivyo linavyoonekana Bango la kinywaji cha Pepsi-mjini Dodoma karibu kabisa na Makao Makuu ya Kanisa la Anglikana - Dayosisi ya Kati.

Makao Makuu ya CCM-Dodoma


Hili ndilo jengo la Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.

Karibuni Wajumbe

Ndivyo Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anavyowakaribisha wajumbe wa CCM mjini Dodoma Makao Makuu ya Chama

Fr. Mathayo altareni

Fr. Mathayo ni Paroko wa Parokia ya Vikindu (St. Vicent de Paolo)

Maduka ya nguo yashamiri Dodoma

Maduka ya nguo yameanza kushamiri mjini Dodoma. Wenyewe wanaita 'designer' ambacho hakinifurahishi ni vinyago vinavyovalishwa hizo nguo mbona ni wazungu?

Simba na Yanga-Dodoma

Nani Mbabe?

Sunday, April 21, 2013

Bango la Kanisa Katoliki Mt.Paulo wa Msalaba-Dodoma

Nje ya Kanisa la Mt.Paulo wa Msalaba kuna Bango linaloonyesha Siku za Ibada na muda wa Ibada.Hakika ni mfano wa kuigwa. Nje ya Kanisa VIWAWA wanaouza nakala za masomo ya misa, picha,hata vitenge kwa lengo la kutunisha mfuko wa chama.

Kanisa Kuu la Mt. Paulo wa Msalaba-Dodoma

Leo kwa mara ya kwanza nimesali katika kanisa hili la Mt.Paulo wa Msalaba-mjini Dodoma.Ni kanisa kubwa na zuri. Ibada iliendeshwa kwa lugha ya Kiingereza. Kwaya iliongozwa na Wasichana wa Shule ya Sekondari (Sikuuliza jina la shule). Baada ya misa Masista wa kutoka Parokia ya Kristu Mfalme jimbo Kuu la Dar Es Salaam walipata fursa ya kujitangaza na kuwaomba wasichana wenye sifa kujiunga na shirika lao la kitawa. Sifa ni msichana aliyemaliza kuanzia darasa la saba na kuendelea. Shirika hilo limejikita zaidi katika masuala ya elimu na tiba.

Milestone- Singida 244

Leo nimegundua kijiwe hiki (milestone) mjini Dodoma kinachoonesha km 244 kwenda Singida kutoka Dodoma.Neno 'Milestone' linatumika sana na wataalamu katika kupima malengo tunayojiwekea.

'Hotel' yangu Dodoma

Nimegundua mahali pazuri pakupata chakula cha mchana wakati nikiwa Dodoma. Ni hapa. Usiulize maswali mengi. Siri yangu.

Hoteli mjini Dodoma

Hoteli nyingi zinazidi kujengwa mjini Dodoma kwa lengo la kuwapatia wageni mahali safi pa kuishi

Barabara za mji wa Dodoma zimeboreshwa

Barabara nyingi za katikati ya mji wa Dodoma zimeboreshwa kwa kiwango cha lami. Dodoma inazidi kung'ara!

Msikiti wa Dodoma

Huenda ukawa Msikiti Mkubwa nchini Tanzania. Msikiti huu upo mjini Dodoma karibu kabisa na Sekondari ya Dodoma Central. Nimefahamishwa kuwa msikiti huu umejengwa kwa hisani ya aliyekuwa Rais wa Libya Muamar Gaddafi.

Uwanja wa Dodoma Central Sec.

Huu ni uwanja wa soka wa Dodoma Central Secondary School uliopo katikati ya mji wa Dodoma. Uwanja huu umekuza vipaji vingi vya wachezaji maarufu nchini Tanzania.

Dodoma Central Secondary School

Hiyo ndiyo Dodoma Central. Enzi zake acha kabisa.Sasa iko hoi bin taaban. Banzi wa Moro ameshuhudia jinsi shule hiyo ilivyochakaa licha ya kupakwa rangi!

Africana April 2013

Mwezi April mwaka huu kikundi cha Africana a.k.a. Kibanda Kimoja kilikutana nyumbani kwa Bw & Bi G.Banzi huko Temboni, Dar.

Mtoto yake soda!

Uncle Elvis akifurahi kinywaji chake nyumbani kwao Temboni, Dar Es Salaam.

Viongozi wa Baraza la Walei Kanisa Katoliki Parokia ya Vikindu

Parokia ya Kanisa Katoliki Parokia ya Vikindu (Mt. Visent wa Paulo)imepata viongozi wa Baraza la Walei litakaloongoza Parokia hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu wakiongozwa na Mwenyekiti Bw. Eric Mwambeleko. a href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgoTYJNl5iFl6y_UEwyfB2ujZLqsZmM2u4pPuSsh5E8xbJcRtUvj7msajllsC3qZiWMBvwuEKmJPL0gK44bGZiDyhfT6gUCJH3OZkWLWGJ1IuPhLyWUg5nfIp5bBRubVHFTddpLPM6uBDet/s1600/MWAMBE+APA+2013.JPG" imageanchor="1">

Wanajengewa uwezo

Watafiti wa kituo cha Utafiti Naliendele, Mtwara wakijengewa uwezo wa kuandaa bajeti