Thursday, April 11, 2013

Operesheni fufua Kariakoo

Hapa ndipo nilipozaliwa. Kisemu, Nige Kariakoo, Matombo, Morogoro. Nyumbani kwa baba zangu Wambiki. Naelezwa kuwa nimezaliwa katika nyumba ya msonge. Na kwa kweli nyumba hiyo hata mimi niliiona. Baadaye baba zangu kwa pamoja walijenga nyumba kubwa ya kwanza ya bati nafikiri ilikuwa mwaka 1965! Nyumba hii ilianguka mwisho mwa miaka ya 90. Kwa kushirikiana na Shangazi Mama Paulina Mloka Kariakoo inaanza kufufuliwa. Inawezekana! Kumbuka ulikotoka.

No comments: