Monday, May 18, 2015

Eti huyu naye ni samaki

Baharini kuna mambo. Huyu naye ni samaki! Hayo mazaga zaga yote ni kwa kujilinda. Ni misumari yenye sumu kali. Ukikanyaga tu lazima udhurike. Samaki wa aina hii anapatikana  Australia anaitwa 'the reef stonefish.' Pamoja ya kuwa ni samaki lakini sijui kama analiwa. Kwanza utamkamataje samaki wa aina hii?

Unaweza kusafiri na nyoka ndani ya ndege

Hebu angalia vizuri nadhani kwenye picha hii unaweza kuona nyoka. Unaposafiri na nyoka ndani ya ndege na ghafla akatokea ndani ya mkoba wako, kwa akili za kawaida utadhani kuwa umerogwa na hasa kama unakwenda majuu kusoma tena majuu yenyewe ni USA! Kwa Australia ni kitu cha kawaida kwa nyoka kuingia ndani ya ndege. Picha kwa hisani ya mtandao.

Chatu anapambana na mwavuli?

Utadhani kuwa chatu huyu anataka kuumeza mwavuli,hapana! Chatu amemmeza popo. Hapa ni Australia ambapo chatu na popo wakubwa wanapatikana.

Pweza huyu ni hatari

Pweza huyu anajulikana kwa jina la 'blue ringed octopus' ana sumu kali sana. Inasemekana kuwa akikuuma basi huchukui masaa mawili umeshaisha! Pweza wa aina hii wanapatikana Australia. Sijui kama kwenye bahari yetu ya Hindi wapo. Kwa kawaida samaki aina ya Pweza hupatikana baharini tu (maji chumvi). Pamoja na kupenda kula Pweza huyu anatisha!

People do ride Kangaroo!

Nimeinyaka hii kwenye mtandao na kunifurahisha.Huko Australia, kuna watu wanawaendesha Kangaroo kama pikipiki au farasi!

Wednesday, May 13, 2015

Ng'ombe wenye nundu bado lulu India

Wahindi hawajatelekeza ng'ombe wao wa asili, isipokuwa wanazidi kuendelea na utafiti ili waweze kuleta tija, kwani ng'ombe hao wapo siku nyingi wanastahimili mazingira ya sehemu hizo. Wako wapi ng'ombe wetu wenye nundu? Wako wapi Zebu wetu wenye nyama tamu. Wako wapi? Watafiti tuambieni, utafiti unaendelea? Je, tumewekeza vya kutosha katika utafiti wa mifugo? Jibu sina uhakika kwa hilo.

Teknolijia zinavyosambazwa na Taasisi zinavyojitangaza India





Mwaka jana nilibahatika kuwa katika msafara wa mafunzo nchini India. Madhumuni ya msafara huo ni kujifunza jinsi wenzetu wa India wanavyoendesha Taasisi za Utafiti. Moja ya kitu ambacho nimevutiwa nacho ni jinsi wanavyotunza kumbukumbu na jinsi wanavyosambaza teknolojia za kilimo na jinsi taasisi zinavyojitangaza. Kikubwa wenzetu ni wazalendo. Hata katika lugha, mabango yote yanatanguliwa na lugha yao na kufuata Kiingereza hii haidhoofishi sayansi, badala yake inakuza sayansi kwani mtu anafanya kitu anachokielewa na pia wadau wanafaida nacho.

Unapopokelewa katika taasisi kabla ya kupata maelezo ya shughuli za kituo hicho, unawekewa clip yenye nyimbo ya Taasisi na wote wanajivunia. Nyimbo inapoimbwa unajionea na kusoma historia ya taasisi, shughuli wanazofanya na mafanikio waliyoyapata. Na hiki ndicho tumekishauri kwa Taasisi zetu za Utafiti kuiga, kwani gharama yake si kubwa kama inavyodhaniwa. Angalia mabango hayo hapo juu yanajitosheleza. Kwa njia hii teknolojia inasambazwa kwa haraka na Taasisi inajitangaza.

Karibu kwa msosi

Siku moja andaa msosi namna hii na kaa pamoja na familia yako na ufurahie maisha. Inawezekana. Usingojee mpaka wakati wa mwaliko wa 'sendoff ' au Reception!

Aliyoyaona Kipanya wakati wa mazishi ya marehemu Komba

Si wote walienda kwa nia moja ya kumzika marehemu Komba huko Mbinga. Wengine walikwenda kujiandaa kukamata jimbo kwenye uchaguzi ujao!

Ninapomkumbuka Uncle Dr. G.Mluge

Dr. Gregory Paul Mluge (R.I.P.)  na mkewe Restituta Mluge wakiwa na mjukuu wao katika picha ya pamoja mwaka 2011. Baada ya kuipata picha hii nimeamua kuining'iniza kwenye blog hii ya Banzi wa Moro kwa kumbukumbu. Nitakukumbuka daima unlce Dr. Mluge ulikuwa nguzo ya familia na utaendelea kuwa nguzo ya familia kwa msingi uliouweka katika maisha yako. Dr. Mluge alifariki mwaka 2013 na kuzikwa nyumbani Matombo (Kiswira), Morogoro. Amina.

Anaweza kuwa sangara

Inawezekana amemvua sangara. Tuna maziwa,bahari na mito pamoja na mabwawa. Je, samaki wameweza kuinua uchumi wa nchi yetu? Magufuli alipojaribu, waliofuata hatusikii chochote kuhusu uimarishaji wa sekta ndogo ya uvuvi.

Kama wewe ungekubaliana na ushauri huu wa mwanao!

Inabidi kuvumilia. Yanga hawana uzoefu wa mashindano ya Kimataifa!

Mtafiti wa mpunga shambani

Pamoja na juhudi zake katika utafiti wa zao la mpunga. Mtafiti Owekisha Kwezigile kutoka kituo cha Utafiti wa Kilimo Uyole, Mbeya anakosa mavazi maalumu akiwa shambani.

Nimembamba Mwekahazina wa Tawi la Yanga

Ndipo nilipombamba live na handbag ya SSC. Huyu ni Yanga damu!

Wenzetu zinawatajirisha na kuinua uchumi wa nchi

   Sisi tunazifanyia maonyesho (Ngozi za wanyama). Wanyama tuliopewa na Mwenyezi Mungu watusaidie kuishi maisha bora. Mungu alimuumba mwandamu kwa mfano wake!

Jangwani Port Authority

   Samahani- Napita tu

St. Francis Secondary School ya Mbeya yakabidhiwa Tuzo

Wengi tunaisikia St. Francis Secondary School  ya Mbeya. Ni shule inayofanya vizuri kitaaluma. Imekuwa ikishikilia nafasi 10 za juu za ufaulu hapa nchini karibu kila mwaka. Shule hii iko makini sana katika kudahiri wanafunzi wanaojiunga na shule hiyo. Si rahisi kupata nafasi kama kijana hana uwezo. Na anapojiunga na shule hiyo pamoja na ukweli kuwa iko vizuri kitaaluma lakini wanaangalia sana nidhamu ya mwanafunzi.Wanafunzi wanatakiwa kuchapa kazi wakiwa shuleni, kutambua kuwa MUNGU yupo na kumwabudu. Nimeambiwa kuwa hakuna kujidai ukiwa shuleni hapo kama baba au mama yako ni Waziri, Mbunge,Mkurugenzi, Profesa au Meneja hiyo ni kwenu. Hakuna kuleta majidai ukiwa shuleni hapo. Pichani Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akikabidhi Tuzo kwa mwakilishi wa shule hiyo mjini Dodoma hivi karibuni.

Pole Mama Maria Nyerere

Mama Salma Kikwete akimpa pole Mama Maria Nyerere kwa msiba wa kufiwa na mtoto wake John Nyerere.R.I.P. John.

Thursday, May 7, 2015

Kiongozi wa Korea ya Kaskazini asiye na masihara

Anaonekana ni kijana na mnyoa punk. Lakini hana masihara huyu. Ni rahisi KIM JUG II wa Korea ya Kaskazini. Ukiingia katika anga zake asivyotaka yeye na kukushuku vibaya unanyongwa tu. Inasemekana kwamba tayari ameshanyonga watu 15  katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Friday, May 1, 2015

Si unachotaka mafuta

Shida yako ni mafuta. Mbwembwe za nini? Unachotakiwa ni kuwa na tank lenye mafuta, pump, kibanda na mhudumu wa kutoa huduma ya mafuta - period! Nashangaa unaposafiri kutoka Morogoro hadi Matombo hakuna hata kituo kimoja rasmi cha mafuta.

Samaki wa baharini


Huyu ni samaki aliyevalishwa kofia nyekundu. Ni viumbe vilivyoko baharini. Haya ni maajabu ya Mungu. Kuna vitu vingi ambavyo MUNGU ameviumba ambavyo wewe hujaviona. Vingine vinatisha na kushangaza.

Siku moja nitajenga kitu kama hiki Kisemvule

  Kitu kama hiki kitajengwa Kisemvule hivi karibuni na nitakimiliki mwenyewe. Subirini muone.

Wajenzi wakipata lunch yao juu kabisa ya ghorofa

Nimeipenda picha hii ingawa ni black and white. Imeandikwa wajenzi wakipata  chakula juu kabisa ya jumba la ghorofa walililokuwa wanalijenga.

Ukisikia maghorofa ndiyo haya


Nyuki anathamini alizeti sisi je?

Ona jinsi nyuki anavyothamini alizeti na kulifuata. Je, sisi tunathamini zao la alizeti linalotupatia mafuta na kuongeza kipato? Pamoja na kuwa na maeneo mengi yanayoweza kustawisha alizeti hapa nchini, sijaona mkakati wa kuliendeleza zao hilo, tunagusagusa tu.

Mlipuko wa volcano

Volcano ikilipuka hutoa moto na huyeyusha hata mwamba

Bonge la theluji baharini

Barafu inaweza kujijenga baharini na kutengeneza mwamba. Hii ni hatari kwa vyombo vya baharini.

Tunaweza kujenga nyumba miambani

Tunaweza kujenga nyumba miambani hapa Tanzania. Tatizo ni miundo mbinu. Umeme na maji vitafikaje? Barababara je. Nyumbani kwetu Morogoro hasa Mgeta na Matombo watu wanajenga milimani. Ukiwa huko na raha mustarehe na unapata ulinzi wa uhakika!

Nimepata picha za ajali ya Mafisango

Mafisango aliipenda Simba na sisi tulimpenda. Wakati wa uhai wake ameifanyia makubwa Simba. Hii ndiyo ajali mbaya iliyomtokea Mafisango barabara ya Chang'ombe karibu na VETA iliyosababisha kifo chake.