Wednesday, December 31, 2014

Nakushukuru Mungu kwa yote uliyonitendea kwa mwaka 2014


Shukrani kwa  Mungu kwa yote uliyonitendea mwaka 2014. Wapenzi wa Banzi wa Moro, mwaka huu nimeweza kufikisha posts 955, posts 353 zaidi ya mwaka jana (602). Nakushukuru sana Bw.Bello kwa changamoto yako wakati ule nilipokuwa niliponing'iniza posts 16 kwa mwaka, miaka miwili mfululizo!

Mafanikio haya yamepatikana kutokana na kuwa na vitendea kazi bora vya IT,safari za kikazi mikoani, shughuli za kanisa na familia pia. Wasomaji wa Blog hii wamekuwa wakinitia moyo sana kwa kuandika comments zao na wengine kunipigia simu baadhi yao ni Bi. Sophia Kizito, Bw. Charles John Arbogasty wa Botswana, Dada Appia Mkoba wa Norway, Dada Eddy Daulinge wa COSTECH aliyetoa maoni ya kutengeneza pesa kupitia blog hii (Nakungoja Sister), Dogo Fredy Mloka wa TTCL, Dr. Doreen Mloka wa Muhimbili University,Sister Ceasar Mloka a.k.a 'Mzungu'  mjisiriamali, Sister Slyvia Daulinge na mumewe Gaitan ambao walikuwa wananipa ujumbe-tumeona vitu vyako! Dada Meab, Dogo Frank Mdimi, Dogo Sily Jakka wa Dadaz Dar (a.k.a. Paroko), Bw.Philemon Kabandwa wa MAFC,Dadaz Ishika na Vidah wa DRD, Dr. Louis Kasuga wa ARI-Naliendele, Bw. Andrew Rabson Kwayu na vijana wake wa IT pale MAFC na wengine wengi.Asanteni sana.

Mategemeo yangu kwa mwakani ni kuboresha zaidi blog hii ili ipendeze na kuvutia wasomaji wengi na pengine kuifanya ya kibashara (kama itawezekana). Yeyote mwenye wazo la kuiboresha namkaribisha. NAWATAKIA MWAKA MPYA WENYE BARAKA ZA MUNGU.

Matombo Msalabani

Ukifika hapa, kushoto ni barabara inayoelekea makao makuu ya tarafa ya Matombo ambako ni Mtamba, barabara hiyo inakufikisha  hadi Kisaki ambako unaweza kupanda gari moshi kwenda Zambia au Dar Es Salaam! Kulia ni baraba kuelekea Matombo Mission, Tawa, Kibungo Juu,  Kibogwa, Nyachiro, Lusangalala, Konde,Mlono,Lanzi,Lukenge, na Kitungwa.

Kwenye bango la Matombo Secondary sijafurahishwa na jinsi Mission yao ilivyoandikwa- 'Always Forward.' Kwa kweli haileti maana hata kidogo.Tutashauriana na uongozi wa shule ili kuiboresha.

Tunauvuka mto Ruvu x 2



Tunaposafiri kutoka Dar kwenda Matombo lazima tuvuke mto wa Ruvu mara mbili. Hapa ni daraja la mto Ruvu unapokaribia Matombo. Mto wa Ruvu unaonywesha jiji la Dar chanzo chake ni Matombo.

Mlima wa Pangawe a.k.a Ng'alo





 Mlima wa Pangawe a.k.a Ng'alo njia ya kwenda Matombo ni mlima mkali una makona machache lakini hatari. Nilipokuwa mdogo nikisafiri na mama na bibi zangu walikuwa wanauogopa sana. Gari lilipokuwa likipanda au kushuka mlima huo wote walikaa kimya kabisa na wengine wakisali. Siku hizi mlima huo umechongwa na kuwekwa lami nyepesi.


Kanisa Katoliki- Mt. Patrick Morogoro

Hili ndilo Kanisa la Mt. Patrick lililoko Morogoro mjini, karibu kabisa na Hospitali ya Mkoa

Hapa ni Chalinze

Huu ni msimu wa mananasi. Angalia jinsi yalivyorundikana. Check pia vijana wanavyotembeza biashara kwa wasafiri. Usipoangalia kwa haraka unaweza kununua bidhaa duni na kwa bei ya juu.

Tusisahau kusoma mabango

Unapofika Kibaha ukitokea Dar umbali wa sehemu unakotaka kwenda zinasomeka hivyo.

Wakati nikielekea Morogoro

Traffic police huyu alikuwa kwenye kazi nzito ya kuongoza magari pale Ubungo

The Banzis walikuwa Matombo kwa Xmass

Linus Banzi (kushoto) na Renatus Banzi - wadogo zangu hawa machachari  ambao wengine wanawaita the twins (lakini si mapacha) niliwakuta Matombo wakila Xmass. Hapa wapo nyumbani kwa uncle Nestory Daulinge

The peace of mind


Jamani nauza nyumba 'yangu!'


A real relationship!


Wambagala tunavyotaniwa

Zamani walikuwa wanatutania kuhusu tunavyogombea mabus sasa wamekuja huku. Tuacheni na Mbagala yetu na nyinyi na Sinza Kijiweni yenu 'period.'

Anaweza kumpiga hata mbwa


How to burn fat

Kupunguza mafuta huyu kaamua kukoka moto kabisaaaa! Kimeeleweka kweli?

Habari ndiyo hiyo

Atajifunza tu kukwea mnazi hata kama bado anatambaa. House Girl anaweza kuchukua uamuzi kama huu na kisha kuondoka.

Don't worry about tomorrow!


Smartphone inauwezo wa kutoa picha jinsi utakavyo

Na ndivyo binti huyu alivyoitengeneza picha yake kutoka umbo flat na kuwa na umbo lenye wowowo balaaa!

Mtoto anaweza kuanikwa kama nguo

Ukimchezea 'house girl' naye anaweza kukuchezea zaidi. Usishangae kukuta mtoto wako ameanikwa kama nguo!

Hata 'house gir'l wa porini naye anajua kutesa


To fool a fool....


Tutumie busara kabla hatujafanya maamuzi ya kuachana

                       Haya ndiyo kina baba yanayotusibu baada ya kuachana na wake zetu

Definition of stupid


Majibu ya kichaa

Ukipata jibu kama hilo huna wasiwasi wasi huyo  akili zake zimepungua (kichaa).

Haijalishi umetayarishwa kwa unga gani

Uwe ugali wa muhogo, dona au mtama kwa vyovyote vile chakula hiki ni kingi mno. Lakini kila mmoja ana bakuli yake ya mboga. Utakwisha tu!

Wanarudi shuleni

Ni hekaheka kwa wazazi walezi na watoto wenyewe. Januari ni wakati wa kuanza mwaka mpya wa masomo hasa kwa shule za msingi na sekondari. Mwezi huu ukipata shida ni yako ni vigumu mtu kukuksaidia. Utasikia "nashughulikia ada ya wanangu."

Tuesday, December 30, 2014

Nyumba ya zamani Nige-Matombo

Hii ni moja ya nyumba ya bati ya zamani sana kijijini Nige- Kariakoo, ipo kando ya barabara ya kutoka Morogoro kwenda Matombo. Ni nyumba ya Mwl. Yuda.

Mtani anapotaniwa

Aliyekaa ni mtani wetu dada wa Fransic Salehe. Ukoo wao ni wa Mgera ni watani na ukoo wa akina baba -Wambiki. Hapa mdogo wangu Tizo Banzi anamtania kuwa tutamnyonya damu! dada zetu wanaangua kicheko!

Alihangaika kupata tawi la furaha



Na alipolipata kugeuka tu alikutana na Banzi wa Moro! Huyu ni dada yetu Helmina Mwenda akiwa na furaha ya mtoto wake Edwin Peter Machemba Banzi kufunga ndoa ndani ya Kanisa Katoliki la Mt. Paul, Matombo, Morogoro tarehe 27/12/2014

Haki sawa kwa wote!

Tulipokuwa nyumbani nilishuhudia hii. Binti yetu Tizo Banzi hakutaka kumpisha Bw. Mrema mtoto wa mpwa wetu Heri Mrema. Miaka ile Binti asingethubutu kukalia kiti cha babu haku mtoto wa kiume akikosa nafasi. Kweli Haki Sawa kwa Wote!

Tufungue 'Barber's shop' Nige Kariakoo

Mdogo wetu Godfrey Banzi aliyeko kijijini Nige-Karikoo, Matombo, Morogoro ni kinyozi mzuri tu. Pichani God akimnyoa kaka yake Renatus Banzi. Hakika ninafikiria kufungua 'Barber's shop' hapa nyumbani Nige-Kariakoo!

Unaamini?


Gari nyota ya punda

Nyota nyingine hazina faida. Kama nyota yako ni ya punda basi usikasirike kubeba mizigo!

Too much can hurt you........................


Utathubutu kugusa?


Shughuli haikosi sare

Ulifika wakati wa kurusha roho basi hapo ndipo kila kitu kilionekana. Sare za vikundi mbalimbali kutoka Dar, Moro na kijijini Nige-Matombo. Angalia nyweli zilivyotengenezwa angalia mavazi yalivyoshonwa, kweli shughuli haikosi sare hata kijijini!

Nyama tamu sana

Nilipewa nyama hii ya mfupa ambayo ni sawa na kupata vipande 10 vya nyama. Ulikuwa ni mfupa mtamu sana. Yote haya ni katika kusheherekea harusi ya Bw & Bi.Edwin Banzi wa Nige, Matombo -Morogoro siku ya tarehe 27/12/2014

Analindwa na waume zake

Dada Helmina Mwenda (katikati) akilindwa na waume zake Linus Banzi(kulia) na Tizo Banzi (kushoto).Hapa ni nyumbani Nige Matombo, Morogoro wakati wa sherehe ya harusi ya Bw & Bibi Edwin Banzi

Harusi ya Edwin Peter Banzi







Hivi ndivyo tulivyosheherekea harusi ya Bw & Bibi Edwin Banzi, kuanzia kanisani hadi nje. Ndoa hii ilifungwa tarehe 27/12/2014 katika Kanisa la Mt. Paul, Matombo, Morogoro. Edwin ni mtoto wa baba yetu mdogo Peter Anthony Machemba. Nilibahatika kuhudhuria tukio hili. Angalia Banzi wa Moro anavyonengua kanisani.