Thursday, May 31, 2012

Hivi ndivyo chai inavyooteshwa

Wengi wetu tumeshakunywa chai lakini ni wachache sana wameshauona mmea halisi wa chai. Pichani ni kitalu cha kuotesha mchai kilichopo kijijini Kidabaga, wilaya ya Kilolo, mkoa wa Iringa.

Tunapata taarifa ya miradi ya kilimo kijijini

Unapoingia kwenye ofisi ya kijiji cha Msosa unakuta matangazo mbalimbali ukutani ambayo yanatosha kukupa hali halisi ya kijiji hicho. Hata hivyo ilibidi tuzungumze na baadhi ya wakulima wa kijiji cha Msosa wakiongozwa na mwenyekiti wao.

Kilimo cha Vitunguu kijijini Msosa

Tulipotembelea kijiji cha Masosa kilichopo katika wilaya ya Kilolo tulishuhudia bonde kubwa linalolimwa vitungu aaina ya Red Bombay kwa njia ya umwagiliaji. Kilimo cha vitunguu kimeboresha maisha ya wakazi wa Msosa.Nyumba za kisasa zimeanza kujengwa na vijana zaidi ya 10 wamerudi kijijini kutoka mijini kushiriki katika shughuli za kilimo kwa muda wa miezi 3 mkulima ana uhakika wa kupata shilingi 350,000 kwa eneo la robo eka tu.
Shamba la vitunguu kijijini Msosa.
Baada ya mazungumzo na wanavikundi kijijini ilibidi tufike shambani

Mradi wa Ufugaji wa Kuku wa asili-Msosa

Moja ya vijiji vinavyopiga hatua ya kasi katika kilimo ni kijiji cha Msosa kilichoko wilaya ya Kilolo, mkoa Iringa. Kijiji hiki kiko karibu sana na barabara kuu ya Tanzania - Zambia sehemu maarufu ya Ruaha Mbuyuni. Licha ya wakazi wake kujikita katika kilimo cha vitunguu, sasa wameanzisha mradi mwingine wa ufugaji wa kuku wa asili. Mwaka 2010 kikundi kijulikacha JIPE MOYO kiliwezeshwa jumla ya shilingi 1,900,000 ambazo ziliwezesha kikundi kujenga banda la kuku na kuku wa kufuga na wanakikundi walichangia jumla ya shilingi 180,000/=. Kikundi kina jumla ya wanachama 21 wengi wao ni wanawake (17). Mradi huu kwa sasa hutumika kama shamba darasa la ufugaji bora wa kuku. Lengo ni kuboresha kuku wa asili. Wakulima hufundishwa lishe ya kuku, tiba, ujenzi wa banda bora na jinsi kuweka kumbukumbu za ufugaji ili kuweza kufuga kwa faida.

Wednesday, May 30, 2012

Skimu ya umwagiliaji kijiji cha Mkungugu

Ujenzi wa Bwawa la Mkungugu, lilipo katika kijiji cha Mkungugu wilaya ya Iringa Vijijini lilianza kujengwa msimu wa mwaka 2009/10 chini ya Progamu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP) lengo ni kukusanya maji ya mvua kwa lengo la kuendesha kilimo cha umwagiliaji.Litakapokamilika, bwawa hili litakuwa na uwezo wa kumwagilia hekta zipatazo 80.Mazao yanayatarajiwa kumwagiliwa ni yale ya bustani pamoja na mahindi. Banzi wa Moro imeshuhudia sehemu kubwa ya bwawa hilo likiwa limekamilika isipokuwa miundo muhimu ya umwagiliaji haijatengmeaa kama vile matanki, pump na mifereji ya umwagiliaji.

Shule ya Sekondari ya Kata - Magozi, Iringa vijijini

Kuongezeka kwa kipato cha wanakijiji wa Magozi kumewezesha kuchangia shule ya Sekondari ya Kata ya Magozi. Shule hii ina kisima cha maji, umeme wa solar, na mabweni ya kulala wanafunzi.

ASDP imeleta mabadiliko kijiji cha Magozi

Kijiji kina 'powertillers' zipatazo 10, vijana wameanza kurudi kijijini kutoka mjini na kushughulika na kilimo cha umwagiliaji
Nyumba bora za kisasa zimeanza kujengwa

Skimu ya umwagiliaji kijiji cha Magozi-Iringa Vijijini

Miaka 21 iliyopita kijiji cha Magozi, wilaya ya Iringa vijijini kila mwaka kilikuwa kikipata msaada wa chakula kutoka na hali ya ukame wa maeneo hayo. Kupitia 'Disitrict Agricultural Develpment Plan (DADP) kijiji kimejenga mfereji wa umwagiliaji kuanzia mwaka 2007 na sasa wanazalisha mpunga kwa wingi. Kwa wastani mkulima sasa anaweza kuvuna magunia 20 ya mpunga kwa eka moja.

Mbwa wetu 'Kijenge'

Mbwa wetu aitwaye 'Kijenge' tunampenda sana. Hubaka kwa nguvu kuashiria tukio hasa nyakati za usiku, anatulinda. Kijenge hula ugali na dagaa la kuchemsha, huogeshwa mara moja kwa wiki kujikinga na kupe. Hunywesha dawa za minyoo angalau mara moja kila baada ya miezi mitatu. Hivi ndivyo tunavyomtunza 'Kijenge.'Lakini kuna kundi la watu wanaiba mbwa kijini kwetu Kisemvule. Wengine wanasema wanawauzia Wachina kwa bei ya shilingi 40,000 kwa mbwa mmoja. Sina uhakika na hilo.

SHEREHE YA KUMPONGEZA DOLORES

MC alikuwa ni Maria 'Bonge' kutoka DADAZ
Dolorose Kamsopi a.k.a EKA akilishwa keki na shangazi yake Hellena Mdimi
Ni zamu ya Baba Joseph Kamsopi Mdimi kulishwa keki na bintiye
Mama akilishwa keki na mwanawe
Babu (Mzee C.M.Mdimi)alilishwa keki
Tulisakata miondoko ya 'gospel songs'
Mjomba Msechu alifungua champaigne
Keki ilikatwa

Dolorose apata Kipaimara

Siku ya tarehe 25/5/2012 itakuwa ya ukumbusho mkubwa kwa Bi Dolorose J.Kamsopi Mdimi a.k.a EKA kwa kupata kipaimara ambayo ni moja ya Skaramenti muhimu katika Kanisa Katoliki. Kipaimara kinakupa ujasiri kupitia Roho Mtakatifu kuweza kueneza neno la Mungu. HONGERA SANA DOLOROSE.

Keki jamvini

Na hii ndiyo keki ya Catherine ya miaka 14

Binti yetu atimiza miaka 14

Jana tarehe 29/5/2012 binti yetu Catherine Banzi (kulia) ametimiza umri wa miaka 14. Hongera sana Catherine Mungu akubariki sana uwe na maisha marefu.

Tuesday, May 29, 2012

Anatambua umuhimu wa mifugo

Pichani kijana Jack Makishe akichanganya chakula cha mifugo.

Zawadi ya kaka George

Na hii ndiyo zawadi ya Kaka kwa dada. Furaha iliyoje!

Furaha ya ndugu

Mdogo wake Adela akicheza kwa furaha siku ya Send OFF

MC alimuona mtoto huyu

Kati ya watoto walioshughulika sana katika kupiga picha za send off ya Adela alikuwa ni huyu mwenye T-shirt ya pink na suruali ya jeans ilibidi MC amtambulishe mbele ya wageni waalikwa na kumpongeza.

Ni wakati wa Kwaito!

Kama umepata msosi na vinywaji bwelele hakuna wa kukukataza kuyarudi magoma kwa raha zako. Hapa ni Moro,Magadu Leaders Club siku ya Send off ya Adela, mzee wetu huyu akionyesha umahiri wake katika kuirudi miondoko ya 'Kwaito'. Kwa kweli Moro oyee!

'Vikuku vinanukia ahaa."

Enzi zangu niliipenda sana nyimbo tuliyoibatiza 'vikuku vinanukia ....' Lakini hii ni picha hali ya msosi tulioukamata siku ya send off ya dada yetu Adela Ng'atigwa (kuku wa kienyeji kutoka Nyandila-mgeta, bamia, njegere, kisamvu, derega, vhimoka, magimbi, samaki, mbumundu, bwasali, ng'udende, uhunga, ng'andulo....). Kilikuwa kitamu sana!

Fuga nguruwe ujiongezee kipato

Nguruwe ni mnyama rahisi kumfuga kwani hashambuliwi sana na maradhi na pia hutumia aina mbalimbali za vyakula ambavyo hupatikana kirahisi katika mazingira yoyote.Jijini Dar Es Salaam nguruwe wa uzito wa kilo 80 anaweza kukupata kiasi cha Tshs 400,000/=. Nilipotembbelea mikoa ya Iringa na Mbeya nilikuta wakulima wengi wakifuga nguruwe hasa wilaya ya Kilolo kijiji cha Kidabaga.

Radio pembeni

Inawezekana vijana hawapendi tena kusikiliza radio. Lakini wazee wengi hupenda kusikiliza radio kama inavyoonekana pichani Mama Hasbon Makishe akiwa karibu sana na radio wakati alipowatembelea wajukuu zake nyumbani kwao Kisemvule mkoa wa Pwani.

Mtu na wifi yake

Dada Julieth Madenge kushoto akiwa na wifi yake Nancy Banzi kwenye bustani za Magadu Leaders' Club-Morogoro

Tuchague miti ya kupanda karibu na nyumba zetu

Tunashauriwa kupanda miti yenye manufaa kama vile ya matunda kando ya nyumba zetu kamavile mpera (pichani)

Monday, May 28, 2012

Na huyu nae ameanza

Iko siku atapaua na ataishi kwenye nyumba yake.

Mjengo wa Masaki

Pitapita zangu jijini Dar kando ya bahari ya Hindi nilinyaka mjengo huu wa Masaki.Nikwambie kitu, Masaki mwanangu asikwambie mtu kuna mijengo ya nguvu na kumetulia, na kusafi!

Bw na Bibi Kavia

Watu wengi wamnekuwa wakiniomba nining'inize picha ya Bw.na Bibi Kavia. Pichani MC.akiwatambulisha maharusi watarajiwa Bw.na Bibi Kavia
Kilimo cha umwagiliaji cha mpunga huko Igurusi Mbeya. Umwagiliaji ni sharti uzingatie kanuni za kilimo bora kama vile kupanda kwa nafasi, kutumia mbegu bora, kuweka mbolea inayostahili, kupambana na wadudu waharibifu pamoja na magonjwa. Ukifuata haya unaweza kuvuna zaidi ya gunia 40 kwa eka moja.

Sunday, May 13, 2012

Kilimo kinavyobadili maisha ya wakulima

Niko kikazi mikoa ya Iringa na Mbeya kwa madhumuni ya kukagua miradi inayotekelezwa na Programu ya kuendeleza Sekta ya Kilimo Tanzania (ASDP).Mpaka sasa nilichokiona kinatia moyo pale miradi ilipotekelezwa vizuri.Vijiji ambavyo havikutekeleza vizuri mambo ni 'business as usual' Wakulima wetu wanafanya kazi katika mazingira magumu. Wanazalisha ili kutulisha sisi. Kuna wengine kilimo kimebadilisha maisha yao. Kwa mfano wakulima wa kijiji cha Magozi Iringa vijijini kutokana na kilimo cha mpunga sasa wana uhakika wa chakula mwaka mzima, wengi wameweza kujenga nyumba bora pia wamejinunulia jenereta ya kufua umeme! Mpunga ndani ya viroba
'Satelitte dish' kijijini Magozi wilaya ya Iringa Vijijini
Nyumba bora za kisasa.

Saturday, May 5, 2012

Meza zilifurika vinywaji

Hakuna aliyelalamika kukosa kinywaji, kila meza ilifurika kinywaji siku ya Sendoff ya Da Adela Ng'atigwa. Waluguru wanasema 'lusona na mbwali' - Sherehe na pombe (tafsiri yangu).

Familia ya Madenge

Kama ilivyokawaida ya Waluguru.Familia ya Madenge kutoka Mgeta hawakukosa 'gubiko'

Meza ya akina Kobelo

Familia ya Kobelo kutoka Dar Es Salaam na Morogoro ilikuwa na meza yao kwenye sendoff ya Adela. Waluguru wanamsemo wao 'Lusona lwao'

Ndugu na marafiki walikutana

Sendoff ya Adela imekutanisha wengi
Dada Rest wa Kilakala-Morogoro
Dada Mbiki wa Morogoro
Dada Kibena wa Morogoro
Wafanyakazi wa MAFC-Dar