Thursday, May 19, 2016

Tanzania imepania kuongeza uzalishaji wa mpunga

Mpunga ni zao linalostawi vizuri katika sehemu nyingi za nchi yetu hasa ukanda wa pwani na mabonde yanayozunguka maziwa yetu na inakopita mito mikubwa. Wakulima wengi huzalisha wastani wa tani 2 kwa hekta ambapo ni kidogo sana. Utafiti uliokwishafanyika hapa nchini unaonyesha kuwa kwa kutumia teknolojia bora za kilimo cha mpunga, uzalishaji unaweza kufikia tani 8
kwa hekta. Hivi sasa serikali inaboresha kilimo hicho kupitia miradi mbalimbali hasa kwenye skimu za umwagiliaji.

Ni changamoto

Wapenzi wa Banzi wa Moro nimerudi kuwajuza.
Inapotokea kuwa na njia mbalimbali za kupeana habari na msambazaji habari ni huyohuyo ni changamoto kwa kweli. Kuingia kwa facebook na whatsapp kwa kweli kumeimomonyoa blog yangu. Inakuwa vigumu kupost kwenye blog. Naweza kupost kutoka whatsapp kwenda facebook tukio hilohilo lakini siwezi kufanya hivyo kwenda kwenye blog. Uzuri wa whatsapp na facebook ni rahisi kupata feedback hivyo kukufanya kuandika na kupost. Hata hivyo nimerudi, nitaanza kuning'iniza kadri ninavyoweza nipatapo wasaa.
Dereva Mwandamizi wa Idara ya Utafiti na Maendeleo Ndg.Shushu Kondowe akiwasilisha taarifa ya mafunzo kwa mratibu wa mafunzo Bw. John Banzi