Tuesday, September 30, 2014

Waseminari ya Vikindu -Siku ya St. Vincent wa Paulo Parokia ya Vikindu





Waseminari ya Parokia ya Vikindu ni moja ya familia hiyo. Hivyo hawakubaki nyuma katika kusherehekea sikukuu wa somo wa Parokia. Mt. Vinsent wa Paulo iliyofanyika siku ya tarehe 28/09/2014-Jumapili

Kwaya ya Mt.Vinsenti wa Paulo ilitumbuiza


Kwaya Vinsenti wa Paulo na Somo ni Vinsenti wa Paulo. Hapa wanawatumbuiza wageni waalikwa. Kwaya hii imeshatoa Album mbili  (Audio na Video) -  'Inabidi Nikeshe'

Utoto Mtakatifu-Wanajengwa Kiimani






Watoto wa Utatu Mtakatifu wakiwatumbuiza wageni waalikwa siku ya kuadhimisha sikukuu ya Mt. Vinsenti wa Paulo somo wa Parokia. Watoto hawa ni nguzo ya Kanisa. Bila watoto hakuna kanisa endelevu.

Ngongoti kutoka Kigango cha Malela- Siku ya sherehe ya Somo wa Parokia ya Vikindu

Ngongoti akiingia uwanjani akiwa na picha ya familia akiashiria kuwa huu ni mwaka wa familia



Ngongoti akiwa na picha ya familia


Ngongoti akijimwaga uwanjani

Ngongoti akicheza 'zunguzunguka'

Anaokota 'michuzi' aliyotunzwa ngongoti


Huyu mwenye koti alishindwa kuvumilia na kuanza kuserebeka na ngongoti

Ngongoti akionyesha picha ya familia wageni walioketi meza kuu
Kama kuna burudani ambayo huwa inatia fora kwenye sherehe zote za Mt. Vinsenti wa Paulo  somo wa Parokia ya Vikindu, basi ni Ngongoti. Mwaka huu Ngongoti alikuwa na mambo mawili mapya. Kwanza aliingia uwanjani akiwa ameshikilia picha ya familia akiwakumbusha waalikwa kuwa huu ni mwaka wa familia. Pili Ngongoti aliserebuka wimbo wa 'Zungukazunguka.' Hii ndiyo turufu yetu wana Vikindu. Tukiitwa popote kwenye tafrija  kama kuna mashindano, ngongoti hakosi kikombe!

Siku ya Somo wa Parokia ya Vikindu - St.Vincent de Paulo












Parokia ya Vikindu Jimbo Kuu la Dar Es Salaam, tarehe 28/09/2014 iliadhimisha sikukuu wa somo- Mt. Vinsenti wa Paulo. Sikukuu ilianza kwa misa takatifu iliyoongozwa na Paroko Fr. Stephen na kisha kwenye burudani ambako waumni kutoka Vigango tisa vya Parokia walishirki na kula pamoja.

Friday, September 26, 2014

Stahili hii ya kunywa maji ni kama kugema ulanzi


Unajifunza nini kutoka kwa Baba Mtakatifu Francis wa sasa?


Jumba analoishi Papa Francis

Hili ndilo jumba amnaloishi Papa Francis wa Kanisa Katoliki

Tanzania iliwakilishwa

                   Uteuzi wa Papa Francis- Tanzania iliwakilishwa ona bendera. Nimeambiwa   huyu             alibeba    bendera alikuwa ni Padri kutoka Tanzania aliyekuweko Vatican wakati huo

Je,unawatambua hawa?


Pope John Paul II

     Katika sura na wakati tofauti

Filosofia ya Eistein


Mpangilio na uzuri wa mahesabu


Ni teknolojia tu


Vatican City


Njiwa wa Vatican

                        Je, unaweza kuwachezea njiwa wetu namna hii?

Wote ni viungo washambuliaji


Kipi kinauma zaidi kati ya hivi??



1. Kusoma miaka 7 chuo na kukaa nyumbani miaka 10 bila kupata kazi....
2. Kulea mtoto kwa miaka 20 halafu unakuja kuambiwa sio wako...
3. Kuibiwa mshahara wako wote baada ya kutoka kwenye ATM