Monday, December 31, 2012

Arnold na Aneth Mdete walipokaribishwa Golden Tulip

Bw na Bibi Arnold Mdete waliandaliwa tafrija ya aina yake iliyoandaliwa kwenye hoteli ya Golden Tulip iliyopo Oysterbay, jijini Dar ndani ya hema! Fuatilia matukio kwenye reception hiyo ya tarehe 29/12/2012 ambayo Waluguru wameibatiza kuwa ni ya funga mwaka !
Huyu ndiye aliyekuwa supervisor!
Wazee wa Itifaki!
Meza ya wazee wa Kiluguru!
Meza ya akina baba Mkude!
Mzee Romanus Mdete akipokea keki kutoka kwa mkwewe Aneth
Nyama choma
Kinywaji maalum (punch)
Kilichofuata ni dance zilipigwa za Moro, bakurutu,taarab hadi Kwaito!
Mandhari ya Golden Tulip, Oysterbay, Dar Es Salaam, Tanzania.

Inapatikana Vikindu

Mikaangizo hii inapatikana Vikindu, Mkuranga!

X-MASS yetu chini ya Mkorosho

XMASS ywa mwaka 2012 mimi na familia yangu tulisherehekea nyumbani Kisemvule chini ya Mkorosho! Mimi sikununua nguo mpya na wala mke wangu sikumnunulia nguo mpya! Lakini pilau ilipikwa!

Ubunifu-Zahanati ya Mimea

Mimea huugua kama binadamu kwani ni viumbe hai. Wataalamu wa kilimo kupitia Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika wakishirikiana na mradi wa 'Plantwise' wamebuni njia ya kuwasaidia wakulima kwa kuanzisha zahanati za mimea mashambani.

Matunda ya Utafiti

Watafiti wa Selian wana aina ya mbegu za mahindi zinazobeba mahindi mawili mawili kwa shina ukitaka kufahamu zaidi wasiliana na kituo cha utafiti wa Kilimo Selian, Arusha(Picha na Livingstone Mwedipando wa ARI-Selian, Arusha)

Monday, December 24, 2012

Wamekuja kuwaona Mgambo

Yule pale Baba Sele! Ndivyo alivyosema Mama Sele baada ya kumuona mmewe baba Sele akiwa katika gwaride rasmi la kuhitimu mafunzo ya mgambo kijijini Kisemvule.

Moja mbili tatu moja mwili legeza!

Ndivyo walivyoimba wanamgambo wa Kisemvule wakati wa 'pass-out' yao iliyofanyika kwenye kiwanja cha shule ya Msingi Kisemvule.Hakika, moja, mbili tatu moja inani kumbusha wakati nilipokuwa JKT Ruvu kuhudhuria mafunzo ya kujenga taifa kwa mujibu wa sheria mwaka 1980!

Askari aliyeiva

Mgambo Maulidi Pembe akionyesha ukomavu wake baada ya kupata mafunzo ya mgambo kijijini Kisemvule.

Brass Band ilirindima Kisemvule

Brass Band ya Jeshi la Wananchi ililirindama kijijini Kisemvule wakati wa 'pass-out' ya wanamgambo wa Kisemvule iliyofanyika kwenye kiwanja cha Shule ya Msingi Kisemvule tarehe 22/12/2012.

Askari wa Mgambo aliyehitimu

Bwana Maulidi Pembe ni mmoja wa askari wa mgambo wa kijiji cha Kisemvule aliyehitimu mafunzo hayo tarehe 22/12/2012 akiwa na mkewe Nyangonga aliyefika kiwanjani kumpongeza.

Jeshi la Mgambo Kisemvule

Tarehe 22/12/2012 kijiji cha Kisemvule kimeweka historia mpya ya kuwa na jeshi lake la ulinzi la Mgambo. Ikumbukwe kuwa kijiji cha Kisemvule kinakua kwa haraka kutokana na viwanda vingi vinavyojengwa katika kijiji hicho kikiwemo kiwanda cha saruji cha Rhino. Kutokana na hali hiyo wakazi wanaongezeka kwa kasi ya ajabu. Hivyo basi kijiji kimetekeleza azimio walilojiwekea kwenye mkutano mkuu wa mwaka kuwa na jeshi la mgambo. Hongera sana Kisemvule.

Friday, December 21, 2012

Mizaha ya watoto

Nimejaribu kupanda karanga

Kuna dhana imejengeka kuwa karanga hazistawi mkoa wa Pwani. Mimi nimejaribu kupanda kidogo mwaka huu. Nitawajulisha matokeo yake

Raha jipe mwenyewe

Wachezaji wa Kise Kids wa baadaye

Banzi wa Moro aliwakuta watoto hawa wa Kisemvule wakiangalia mazoezi ya kaka zao wa Kise Kids.

Starehe za Kisemvule

Shughuli! Ni moja ya starehe za Kisemvule hasa kwa akina mama.

KISE KIDS WAANZA MAZOEZI

Klabu ya Soka ya Kise Kids ya Kisemvule wilaya ya Mkuranga imeanza mazoezi makali katika kiwanja cha shule ya msingi Kisemvule chini ya mwalimu wao Abdallah Pembe

Selian KARIBU & KWAHERI!

Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Selian kilichopo mkoani Arusha kanda ya Kaskazini kina utamaduni mzuri wa kuwakaribisha wafanyakazi wapya na kuwaaga wale waliostaafu.Mkurugenzi wa Kanda wa Utafiti Dr. Lucas Mboyi Mugendi akiwapa mkono 'in style' angalia bahasha aliyoshika!
Karibuni Selian watafiti wapya.
Kwa heri Mr. Myovella gwiji la Karakana!
Kwaheri mama Juliana Luziga mahiri wa kumbukumbu za ofisi! (Picha zote kwa hisani ya Bw. Livingstone Mwedipando wa ARI-Selian, Arusha).

Mario Balotelli anapocheka hahaa!

Ni nadra sana kuiona picha ya Mario Balotelli akiwa na furaha kama hii. Balotelli ni mmoja wa wachezaji wenye rangi nyeusi wanaotikisa soka la Uingereza. Yeye ni mchezaji wa timu ya Manchester City.

Ziara ya Mkuu wa Mkoa kituoni Selian

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Magessa Mulongo alipotembelea kituo cha Utafiti wa Kilimo Selian, Arusha ambacho ndicho makao makuu ya Kanda ya Kaskazini
Dkt Fridah Mgonja(Mwenye vazi rangi nyekundu) wa kituo cha Utafiti wa Kilimo Selian akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa Mhe. Magessa Mulongo (wa kwanza kulia). (Picha zote kwa hisani ya Bw. Livingstone Mwedipando wa ARI-Selian, Arusha).

Thursday, December 20, 2012

Siielewi Cartoon hii ya KIPANYA

Ninachoona ni mayai, vibomu vidogo, jogoo anavuta gunia la ajira. Bado siielewi cartoon hii ya Kipanya iliyoko kwenye gazeti la Mwananchi la tarehe 20/12/2012.

Dkt. Eliab Luvanda-Matunda ya NJOSS

Mwaka 1974 pale Njombe Secondary School (NJOSS)nilikutana na kijana mpole Eliab Luvanda akiwa kidato cha pili nami nikiwa kidato cha kwanza. Eliab tulikuwa tukiishi bweni moja la sita, ghorofa ya pili na kwenye cubicle moja. Nilimfahamu Eliab kwa kuwa yeye alikuwa ni mpenzi sana wa Dar Young Africans na mimi shabiki mkubwa wa Simba Sports Club a.k.a Wekundu wa Msimbazi. Mwaka 1976 Eliab alimaliza kidato cha nne na kufaulu vizuri nafahamu alikwenda form v lakini sikumbuki shule gani na combination gani. Ninachofahamu kwa Eliab alikuwa ni mweledi sana alikuwa na uwezo wa kuelewa masomo kwa haraka sana na hakutumia muda mwingi kekesha ili kuelewa mambo alilala mapema na kuamka mapema. Ninachofahamu, Eliab kila siku asubuhi aliamka mapema sana kabla sisi hatujaamka na kujiandaa kwa masomo.Miaka 38 sasa, huyu hapa Dkt.Eliab Luvanda ), Mhadhiri (Mchumi)wa Chuo Kikuu Dar Es Salaam akitoa mafunzo ya kuongeza uwezo wa kuchambua takwimu za hali ya umaskini nchini.Hili ni moja kati ya matunda mazuri ya NJOSS.(Picha kwa hisani ya gazeti la Mwananchi 20/12/2012)

Sindano ya kushonea ya mkono

Kila kitu kinajieleza. Jamani sindano! Tanzania tunatengenza sindano zetu wenyewe au tunaagiza kutoka nchi nyingine? Nipe jibu.(Picha kwa hisani ya gazeti la mwananchi tarehe 20/12/2012).

Christopher Katongo wa Chipolopolo

Huyu ndiye Christopher Katongo captain wa timu ya Taifa ya soka ya Zambaia a.k.a Chipolopolo akihojiwa na waandishi wa habari maru tu baada ya kushuka kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana tarehe 19/12/2012. Zambia itacheza na Taifa Stars siku ya Jumamosi tarehe 22/12/2012 uwanja Taifa.

Tuesday, December 18, 2012

Wanawake na Wanaume wachangia hoja Vikindu

Mabadiliko makubwa yanayoleta maendeleo katika mkoa wa Pwani yameanza kuonekana. Wanawake na wanaume wanashiriki kwa pamoja katika kuleta maendeleo. Katika mkutano wa wazazi na Bodi ya Shule ya Sekondari Vikindu ya Mkuranga, mkoa wa Pwani uliofanyika tarehe 24/12/2012 shuleni hapo,wazazi walichangia hoja chanya za kusaidia kuboresha elimu inayotolewa kwa watoto wao. Waliongelea kuhusu miundo mbinu ya shule, nidhamu na taaluma.
Wanawake kwa waume walichangia hoja.

Kisemvule kimeshatoa matofali 200

Kijiji cha Kisemvule kilichoko kata ya Vikindu tayari kimeshawasilisiha jumal yan matofali 200 na mifuko miwili ya sementi kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya shule ya Sekondari Vikindu kwa kuzingatia makubaliano yaliyofanyika kwenye kikao cha Kata ya Vikindu.

Wazazi wajionea hali halisi ya vyoo

Kabla ya mkutano na Bodi. Wazazi walitembezwa kujionea wenyewe hali halisi ya vyoo wanavyotumia watoto wao wawapo hapo shuleni Vikindu Sekondari.

Hali ya vyoo vinavyotumika shueni Vikindu

Hii ndiyo hali halisi ya vyoo vinavyotumika kwa sasa shule ya Sekondari Vikindu.