Thursday, December 20, 2012

Dkt. Eliab Luvanda-Matunda ya NJOSS

Mwaka 1974 pale Njombe Secondary School (NJOSS)nilikutana na kijana mpole Eliab Luvanda akiwa kidato cha pili nami nikiwa kidato cha kwanza. Eliab tulikuwa tukiishi bweni moja la sita, ghorofa ya pili na kwenye cubicle moja. Nilimfahamu Eliab kwa kuwa yeye alikuwa ni mpenzi sana wa Dar Young Africans na mimi shabiki mkubwa wa Simba Sports Club a.k.a Wekundu wa Msimbazi. Mwaka 1976 Eliab alimaliza kidato cha nne na kufaulu vizuri nafahamu alikwenda form v lakini sikumbuki shule gani na combination gani. Ninachofahamu kwa Eliab alikuwa ni mweledi sana alikuwa na uwezo wa kuelewa masomo kwa haraka sana na hakutumia muda mwingi kekesha ili kuelewa mambo alilala mapema na kuamka mapema. Ninachofahamu, Eliab kila siku asubuhi aliamka mapema sana kabla sisi hatujaamka na kujiandaa kwa masomo.Miaka 38 sasa, huyu hapa Dkt.Eliab Luvanda ), Mhadhiri (Mchumi)wa Chuo Kikuu Dar Es Salaam akitoa mafunzo ya kuongeza uwezo wa kuchambua takwimu za hali ya umaskini nchini.Hili ni moja kati ya matunda mazuri ya NJOSS.(Picha kwa hisani ya gazeti la Mwananchi 20/12/2012)

2 comments:

Pansullah Chavichavi said...
This comment has been removed by the author.
Pansullah Chavichavi said...

NIMESOMA NJOSS ADVANCED LEVEL,NA NIMESTAAJABU MAANA AMENIFUNDISHA ECONOMETRICS NLIPOKUWA NASOMA SHAHADA YA UCHUMI.HAKIKA HULKA YAKE HAIJABADILIKA NA BADO ANA UELEWA MKUBWA SANA MAANA HILO SOMO NI GUMU LAKINI ALIKUWA ANATUFUNDISHA VYEMA.NAJIVUNIA KUSOMA NJOSS