Monday, December 17, 2012

Za Mchina feki zetu ziko wapi?

Waafrika tukiwemo sisi Watanzania tumezoea kulalamika na kudharau vitu vya wengine hali hilal wenyewe hatuna tunachotengeneza. Wengi nimekuwa nikiwasikia wakisema simu ya China hovyo, pikipiki za mchana hazifai, mabasi ya Mchina hayafai. Lakini sijaona simu ya iliyotengenezwa kutoka Tanzania au Kenya ambayo haifai. Viko wapi vya kwetu? Kama hutaki simu ya Mchina feki kuna Nokia nenda kanunue? Mchina amefanya utafiti na kugundua soko la kuuza bidhaa zake kwa bei nafuu nasi tunazinunua kwahiyo tusilalamike. Kama tunataka vizuri tutengeneze vya kwetu halafu tulinganishe na vya Mchina. Isitoshe pikipiki itakuwaje imara kama inabeba watu zaidi ya mmoja au mzigo mzito? Hata kama Yamaha ya Mjapan haiwezi, itaharibika tu.

No comments: