Sunday, November 27, 2011

Chodo na kabati limeanguka

Hebu fikiria unapoitwa urudi nyumbani kwa sababu kabati limeanguka! Sidhani kama utadharau. Lakini hiyo ni stahili ya uswahili ya kuitana wakati wa kula chakula la sivyo wote watakuja na chakula hakitatosha!

Huyu naye anafyonza 'umande wa mlimani'

Watoto hupenda soda huyu hupenda 'Mountain Dew' - umande wa mlimani!

Wapenzi wa Soka Kisemvule

Wakazi wa kijiji cha Kisemvule wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani ni wapenzi wa mchezo wa soka. Mwaka wa jana Serikali ya Kijiji iliandaa mashindano yaliyojulikana kwa jina la KISE CUP. Mwaka huu je?

Saturday, November 26, 2011

Ndani ya CCM-NEC

Kujenga au kubomoa.Busara itumike. (Picha kwa hisani ya CITIZEN ON saturday 26/11/2011)

Lagos-Traffic Jam

Ukisikia traffic jam ndiyo hii. Na hapa ni Lagos Nigeria. Miji mingi ya Afrika matatizo yake yanafanana! (Picha kwa hisani ya gazei la Citizen on Saturday 26/11/2011)

Tumsome Mshindo Msolla


Dr. Mshindo Msolla ni mmoja ya watu waliojaliwa vipaji hapa duniani. Yeye mtaalamu bingwa kwenye raslimali ya udongo. Aidha Msolla ni kocha mahiri wa mchezo wa mpira wa miguu (Soccer). Ameshawahi kufundisha timu ya Taifa mara nyingi katika vipindi tofauti. Kwa mapenzi aliyonayo kwenye soccer, Msolla ana mraba wake katika gazeti la 'The Citizen' kila Jumamosi. Mraba wake unaitwa 'Looking at Sports with a bird's eye' ndani ya mraba huo Msolla huchambua masuala mbalimbali yanayohusu michezo hapa nchini na duniani kwa jumla.Katika mraba wa leo, Msolla anakuja na rai ya vilabu vikubwa vya soka hapa nchini kukuza vipaji vya wanasoka vijana kwa kuwasajili katika ligi kuu badala ya kupoteza fedha nyingi kusajili wachezaji wazee waliokwisha kutoka nje. Swadakta! Dr. MSOLLA.

Chodo na yai

Mwalimu amewaagiza wanafunzi kila mmoja alete yai. Chodo anajibu vingine kabisa. Hebu soma sababu aliyoitoa.

Watoto wetu wa Kisemvule Pr.School

Hawa ndiyo watoto wetu wa shule ya Msingi Kisemvule wakisheherekea mahafali ya wahitimu wa darasa la saba 2011.

Inakuwaje unaposindikizwa?

Unapomtembelea ndugu yako, rafiki yako au yeyote yule. Ukiona unasindikizwa na familia nzima huku hawataki uondoke na kukusindikiza hadi kituoni ujue wamefurahia ujio wako!

Hapa ndipo SUASA

Hii ndiyo Canteen maarufu Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine. Inaitwa SUASA.

Natoa Vyeti

Mwezi wa Kumi mwaka huu wanafunzi Wakristo wa Bright Angels Secondary School walinialika kuwa mgeni rasmi katika mahafali ya wanachama wa vyama vyao vya kidini hapo chuo waliohitimu kidato cha Nne. Lazima nikiri kuwa hiyo ni mara yangu ya kwanza kutunuku vyeti kwa wahitimu ni heshima iliyoje! Shukrani

Mbwa ukimchezea atakunga'ta!

Mbwa ni mnyama mlinzi wa binadamu lakini ukimchezea atakudhuru!

Friday, November 25, 2011

Chodo na mbinu za Dar

Ni kweli Chodo ukichacha Mangi atakusevu- Mimi nina rafiki yangu Mchagga anaitwa Makishe nikichacha huwa ananikopesha nyepesi nyepesi!

Thursday, November 24, 2011

Simbakalia alipotembelea ARI-Naliendele

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Mstaafu Mh.Joseph Simbakalia alipotembelea Kituo cha Utafiti wa Kilimo - Naliendele, Mtwara alikuwa na hitimisho hili:-
1)Bado kilimo ni msingi wa maendeleo na kwa Mtwara upatikanaji wa gesi asilia (na huenda mafuta) kutasababisha wageni kuingia kwa wingi na hivyo mahitaji ya chakula yataongezeka. Mkoa unatakiwa kujipanga kukabiliana na changamoto hii, na kituo cha Utafiti kinaweza kutoa mchango mkubwa wa namna ya kuongeza chakula kutokana na majukumu yake.
2)Kituo cha Utafiti wa Kilimo Naliendele ambacho ni cha daraja la kwanza duniani (first class worldwide) katika utafiti wa zao la korosho. Hata hivyo, bado kilimo cha zao hilo hakijafikia hatua au kiwango ambacho taifa lingependa kuona. Bado kuna matatizo katika uzalishaji wa zao hilo ambayo hatuna majibu aidha kama wataalamu au kama serikali.

Mkuu wa Mkoa anapochukua fursa ya siku nzima kuona shughuli za watafiti na kuzungumza nao, unapita picha ya jinsi gani anavyotoa kipaumbele kwa masuala ya teknolojia katika maendeleo ya nchi.

Kilimanjaro Stars mazoezi ya kufa mtu


Zikiwa zimesalia takribani siku mbili mashindano ya CECAFA Challenge Cup kuanza siku ya Jumamosi jijini Dar. Wachezaji wa Kili Stars waliendelea kujifua kwenye uwanja wa Karume. Pichani chini Erasto Nyoni, Kushoto-Mbwana Samatta na kulia ni Said Morad (picha kwa hisani ya gazeti la Mwananchi tar 24/11/2011)

Napata picha

Wngine hawaamani, wengine wanashangaa, wengine wanaona kama kejeli vile!Wengine kama hakuna kilichotokea. (Picha kwa hisani ya gazeti la Mwananchi tarehe 24/11/2011

Samaki mkunje angali mbichi


Mtoto Vanesa Himili Mbawala anapoamka asubuhi huchukua kikombe na mswaki tayari kwa kusafisha meno yake.Uncle Vanesa pamoja na mama yake walitutembelea Kisemvule wakitokea Arusha wanakoishi. Tabia nzuri sana. Samaki mkunje angali mbichi!

To graduate on 3rd December 2011

Maria John Banzi will 'graduate' from Nursery School education on 3rd December 2011 at St Vicnet Vikindu Nursery School Mkuranga.

Samaki samaki

Sijafika huko kwenye klabu ya samaki samaki. Lakini ubunifu wa kofia zao za samaki samaki niliwaomba wanitengenezee ya rangi nyekundu (simba!). Banzi wa Moro nimetulia utanitaka?

Chodo na Elimu ya Afya

Kweli Chodo hata wasomi wetu kwenye hili jambo wako nyuma sana. Tembelea mashuleni, ofisini ni uchafu, uchafu, uchafu lo. Vyoo vichafu, vyumba vichafu, mifereji michafu viwanja navyo ni vichafu. Kwa hiyo kujifunza tu elimu ya afya hakutoshelezi inatakiwa kujifunza kwa vitendo.

Wednesday, November 23, 2011

Watoto-Bembea


Kila mchezo na wakati wake na kundi lake. Watoto hupenda kubembea

Kila mtu hupenda usalama wa chombo chake

Gari la uncle Jordan likiwa lime park ndani ya Sitting room!

Kula ukipendacho

Fredy na mdogo wake Athony wakichagua msosi!
Dada Ghana akimwambia kaka yake Fredy anza wewe
Dada Eddy-msosi mtamu sana!
Christian Mkoba a.k.a Rizik, nyumba hujengwa kwa matofali!
Dada Esther msosi 'gumala'Tukikutana Africana. Tunajadiliana na maamuzi yenye manufaa ya kikundi hutolewa (mengine magumu) lakini hatukosi msosi wa pamoja. Jumapili tulikuwa Chang'ombe nyumbani kwa familia ya Japhet Kirita (Baba Jordan). Asanteni sana kwa maandalizi mazuri. Jumapili ya tarehe 11/12/2011 Africana watakutana nyumbani kwa Bw. Christian Mkoba a.k.a. Rizikiel au Matombo maarufu kama Baba Mbiki- huko Mikocheni saa 6.00 juu ya alama.

Chodo na Kuvunja vyombo

Kuvunja vyombo hakuna mkubwa wala mtoto.Tena mara nyingi wale walio na wafanyakazi wa nyumbani wakivunja vyombo hukatwa kwenye mishahara yao, wahudumu wa Bar wakivunja glass hukatwa kwenye posho zao! Kwa kweli kuvunja vyomba mara nyingi ni bahati mbaya na siyo makusudi.Hebu angalia yaliyomkuta baba Chodo.

Birthday ya Kisa!

Kisa anakata keki
Kisa anazima mishumaa
Kisa chai ya miaka 30
Tukiwa mafunzoni Dodoma, Kisa Tulibonywa Mwaisoba-Socio-Economist kutoka kituo cha Utafiti wa Kilimo Uyole, Mbeya aliazimisha birthday yake ya 30. Hongera dada Kisa una miaka zaidi ya 30 ya kufanya kazi ya utafiti!

Generator inafanya kazi!


Haina make wala model.Generator hii iliyopo Dear Mama Hotel Dodoma inafanya kazi vizuri sana. Wakati Hotel au Guest Houses nyingine inapowashwa generator hakuna kuwasha TV wala AC. Dear Mama ruhusa!

Dodoma Kondoa barabara isiyo na msongamano

Si kama Dar Es Salaam. Barabara nyingi za Dodoma hazina msongamano. Hivi ndivyo alivyokuta Banzi wa Moro alipokuwa Dodoma hivi karibuni.

UDOM ni mji ndani ya mji

Chuo Kikuu cha Dodoma kwa mpangilio wake kiko safi sana kina eneo kubwa na kimejengwa mahali pazuri kilimani! Mpangilio wake ni kwa Colleges na huko kuna miundombinu yote. Kama alivyosema Maamud inatakiwa menejimenti nzuri na uwezeshaji wa hali ya juu kuiweka UDOM katika hali nzuri na kuiboresha zaidi




Tuesday, November 22, 2011

Hii ndiyo UDOM bwana!

Chuo Kikuu Dodoma au kwa kifupi UDOM. Ni chuo kilichojengwa kwa fedha zetu wenyewe. Chuo Kimejengwa katika mandhari mazuri zamani pakiitwa-Chimwaga-CCM.Ungana nami kesho nikupatie baadhi ya majengo ya UDOM.

Chodo na Kilo ya mawe


Filosofia za Chodo Bwana!

Tuesday, November 15, 2011

Watafiti wajiandaa kwa Kilimo Masoko

Mkurugenzi Msaidizi - Mifumo ya Kilimo na Uchumi Jamii Bw. Ninatubu Lema (wa pili kutoka kushoto)akiongoza mafunzo ya utafiti wa kilimo masoko yaliyoanza tarehe 14 Novemba 2011 mjini DodomaWachumi Kilimo kutoka Idara ya Utafiti na Maendeleo wakiwa katika mafunzo ya muda mfupi ya jinsi ya kuandaa tungo bora kwa ajili ya utafiti Kilimo Masoko. Lengo ni kuweza kuwa na taarifa za uhakika katika uwekezaji katika kilimo. Kwa mfano ni vyema mkulima akafahamu katika mazingira yake kama kulima mpunga kunalipa na kwa kiasi gani.

Dear Mama Hotel-Dodoma

Chumba cha asili kando ya hotel ya Dear Mama - Dodoma ndani ya 'kijiji cha Samunge'
Kijiji cha Samunge ndani ya Hotel

Mvua zinazonyesha sasa zinaashiria nini?

Licha ya kuleta madhara makubwa huko Mwanza, hata mkoa wa Pwani wilaya ya Mkuranga mvua ya kutosha imenyesha siku ya Jumamosi huko Kisemvule.Weusi unaoonekana kwenye picha siyo nyoka ni mkondo wa maji.
Hata kuku walijibanza kibandani