Friday, January 31, 2014

Ubwabwa ukipaliliwa mkaa

Hakika hutokosa matandu!

Kikundi cha Kuigiza Moro

Nikiwa Morogoro kwenye sherehe za harusi, mara nyingi  hukutana na kikundi hiki kinachoigiza muziki wa dansi uliokuwa ukipigwa na magwiji wa muziki huo mjini Moro ambao wote kwa sasa ni marehemu. Nao ni Mbaraka Mwinshehe Mwaruka, Juma Kilaza na Salum Abadallah. Kwa kweli ukiwaona waigizaji hao (pichani) utafurahi hasa kwa wale wenye umri wa miaka 50 na zaidi ya hapo kwani wanaweza kukumbuka enzi zao.

Namezea mate ndafu hii

Jinsi ilivyochomwa. Ndafu hii ilichomwa na mtaalamu kutoka Kilimanjaro anaitwa Joseph. Wachagga kwa kutengeneza ndafu ndo wenyewe. Na ni wakali pia katika kudhibiti matumizi ya fedha. Lakini wanajua jinsi ya kzitafuta. Hii ndafu ilitafumnwa siku ya Boxinga day ya  mwaka 2013 huko Mbezi Beach nyumbani kwa mjomba Dr. G.Mluge

Nyumbani kwa Dr. Gregory Mluge

Nyumbani kwa mjomba marehemu Dr. Gregory Mluge, Mbezi Beach, Dar Es Salaam.

Ustaarabu wa Pwani

Ni kuvua viatu. Pwani mchanga ni mwingi kwa hiyo mtu mstaarabu haingia ndani huku akiwa amevaa viatu. Ustaarabu wa watu wa Pwani.

Paka anaweza kuwa rafiki na adui pia



Dada zetu ukumbini Moro

Akina Kimbiki na watoto wao wakijimwaga wakati wa sherehe za kumpongeza kaka yao Richard Banzi mwishoni mwaka jana huko Morogoro

Thursday, January 30, 2014

Karibuni wageni wetu

Mwezi huu tulitembelewa  na wageni muhimu nyumbani kwetu. Bw. Paul Mbetwa na mtoto wake

Waliofanikisha harusi ya Richard Banzi

Kutoka kushoto Faustini Mizambwa, Mrs Mizambwa, Mrs. Kobelo, Mr. Aniani Kobelo (Mwl. Thomas). Anayetambulisha Mama P.Mloka wakati sherehe ya kumpongeza Bw. Richard Banzi kwa kufunga ndoa huko Morogoro Desemba, 2013. Kazi nzuri ndugu zangu HONGERENI.

Msosi unaandaliwa

Msosi wa nguvu unaandaliwa tena ni wa watu wengi. Hebu angalia miiko !

Watoto wanapenda kuogelea



Ametulia kwa picha

Jogoo huyu ametuli tuli kupigwa picha.

Yanga Kandambili

Yanga kandambili ndiyo hii!

Elfu kumi ya Bluu

Tuliwahi kwa na noti ya bluu yenye thamani ya Tshs 10,000/=  picha ya Rais ni ya Mwinyi.

Whisky inapogeuzwa maji ya kunawa

Kama starehe ndiyo hivi basi laana. Wakati wengine wanatafuta fedha ya chakula, huyu ananawa mikono yake kwa kutumia pombe kali - Whisky!

Kuna ubishi?


Uokovu wa kula nyasi

Inasemekana hawa wameokoka na wanasali kwa kula nyasi. Ukiangalia vizuri picha hii wote ni vijana. Hivi kuna nini kinaendelea? Je, ni kukata tamaa ya maisha?

Kitalu cha miche ya miembe


Tuesday, January 28, 2014

WAWATA DEKANIA YA KIGAMBONI

Tarehe 25/01/2014. WAWATA, Dekania ya Kigamboni iliendesha Misha ya Shukrani Parakiani Vikindu. Misa hiyo ilifana sana na Jumla ya shilingi milioni 5 zilichangiwa kutunisha mfuko wa Elimu ulioanzishwa na chama hicho cha Wanawake Wakatoliki Tanzania.

Maandamano kuelekea kanisani


Happy Birth Day Norbert !



Tarehe 26/01/2014 Norbert Macarios Banzi ametimiza mwaka mmoja. Happy birthday Norb. Je, atakuwa dereva?

Onyo

Baeleze, baeleze!

Ujasiri wa kuchezea nyoka

Wengine wanaogopa nyoka. Lakini kuna dada majasiri wa kucheza ngoma na nyoka hapa nchini Tanzania huu ni utamaduni wetu tuuenzi.

Mwanangu kujiunga na shule hii

Sababu kubwa ni mmiliki wa shule hii ni Simba mwenzangu. Akha! Charity begins at home babu!

Mama Kikwete hotuba kwa wake wa Mabalozi

Mama Salma Kikwete akitoa hotuba ya kuukaribisha mwaka mpya kwa wake wa Mabalozi nchini Tanzania hivi karibuni.

Mawaziri wa Fedha Tanzania

Mawaziri wa Fedha Tanzania. Watatu ni wa Muungano na mmoja  wa Zanzibar. Chungu kimoja

Kikwete na Ruto

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa   Ruto Makamu wa Rais wa Kenya hivi karibuni

Mnyama!

Usimchezee simba atakurarua. Kaa mbali naye!

John Pombe Magufuli kwenye eneo la Mafuriko

Waziri wa Ujenzi Mhe. John Magufuli akiwa katika eneo la mafuriko kwenye daraja la Dumila

Magufuli ndani ya mtambo kwenye eneo la darala la Dumila

Waziri wa Ujenzi Mhe. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya mtambo wa kujaza kifusi kwenye daraja lililoharibiwa na mafriko huko  Dumila, Kilosa, Morogoro.

Mafuriko kijiji cha Magore

Mafuriko kijiji cha Magore. Kikwete ashtukia takwimu zilizowasilishwa za wahanga wa mafuriko

Hivi ndivyo daraja la Dumila lilivyochimbika

Daraja lilichimbwa mwanzo na mwisho hivyo  kulifanya lisipitike baada ya mvua kubwa kunyesha wilayani Kilosa mkoani Morogoro hivi karibuni.

Ibrahimu Masoud akimhoji Sumaye

Mtangazaji maarufu wa michezo wa Clouds alipata fursa ya kumhoji Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Sumaye wakati alipotembelea studio za kituo hicho hivi karibuni. Masoud alimuuliza swali la kizushi Mhe. Sumaye mapenzi yake kwa Club ya Simba ya mtaa wa Msimbazi  maaelezo zaidi sina.

Kikwete ashangiliwa Switzerland

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akishangiliwa baada ya kutoa hotuba yake mjini Davoos, Switzerland.

Pokea hati ya kuboresha jeshi la Polisi

Waziri wa Mambo ya Ndani  Mhe. Mathias Chikawe akipokea hati ya kuboresha Jeshi la Polisi nchini Tanzania.

Huyu ni Flaviana Matata

'Modo' Flaviana Matata  mrembo kutoka Tanzania anayefanya vizuri katika masuala ya urembo

Nasikia 'Lulu' amepata mchumba

Huyu ndiye Elizabeth Michael a.k.a Lulu aliyepata kashikashi ya kifo cha Kanumba. Ni mcheza filamu maarufu hapa Tanzania. Tetesi ni kwamba Lulu amepata mchumba

Hiyo ndiyo bodaboda bwana

Waw! Bodaboda  abiria 8! Hata gari ndogo aina ya Toyota haiwezi kubebe abiria wengi kiasi hicho. Lakini abiria wameufurahia usafiri huo!

Bill ya utata

Je, umeshawahi kuandikiwa bill ya utata? Hii hapa. (Picha kwa hisani ya fb-George Mandepo)

Picha ya kuchora ya Bi.Kidude

Marehemu Bi. Kidude mwimbaji gwiji wa muziki wa taarabu hapa nchini

Yapo mahindi rangi nyeusi

Wengi tumezoea mahindi rangi nyeupe au manjano. Lakini ya rangi nyeusi yapo pia.

Aina nyingi za karoti

Kuna karoti za aina nyingi; nyeupe, njano,kijani,nyekundu........

Kuna aina nyingi za bilinganya

Kuna aina nyingi za bilinganya ambazo wengi hatuzifahamu na hatujazila.

Adha ya ujenzi wa barabara ya mabus yaendayo kasi DAR

Mpaka itakapokuwa imekamilika. Ujenzi wa barabara ya mabus yaendayo kasi jijini Dar utakuwa umewatesa wengi na kwa kweli wachumi tunaweza kukokotoa gharama ya matumizi ya mafuta na kuchelewa kazini wakati wote wa ujenzi wa barabara hiyo/hizo. Tutashangaa!