Wednesday, March 2, 2016

Wataalamu wa ERPP ofisini Mvomero

Mradi wa kuongeza uzalishaji wa Mpunga (ERPP) umeshaanza. Mradi huu utatekelezwa katika wilaya tatu za mkoa wa Morogoro (Mvomero,Kilosa na Kilombero). Skimu za umwagiliaji zitahusika nazo ni  Kigugu, Mbogo-Kamtonga, Mvumi, Njage na Msolwa. Pichani wataalamu wakielezea jinsi mradi huo utakavyotekelezwa ndani ya ofisi ya Mkurugenzi wa Maendeleo Halamshauri ya Mvomero (Haonekani).

Ifakara ya 2016 inang'ara

Hii ni moja nyumba ya kulala wageni iliyopo mjini Ifakara.m Miaka 10 iliyopita mji wa Ifakara ulikuwa na nyumba chache za kulala lakini hivi sasa nyumba za aina hii ni nyingi tu. Hebu fikiria pango la chumba kwa usiku mmoja ni Tsh 15,000/= huku ukila raha ya TV ya bapa!

Padri Abdoni Antipas Nzegesela akisoma Injili

Padri Abdoni Antipas Nzegesela ni Paroko wa Parokia ya Ilonga iliyoko Kilosa- Kanisa Katoliki jimbo la Morogoro. Pichani anaonekana akisoma Injili ndani ya Kanisa Katoliki Vikindu, Jimbo Kuu la Dar Es Salaam. Ndiye aliyefungisha ndoa ya Bw. Macarios Banzi na Bi. Martina Jeremias siku ya tarehe 6/02/2016

Bango bora la Shule ya Msingi Kisemvule

Huenda likawa bango bora kabisa kwa shule za msingi za wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani. Ni shule ya msingi Kisemvule. Kila kitu kiko wazi.Huu ni ubunifu wa mwalimu mku wa shule hiyo ambaye amehamishiwa hapo shule hivi karibuni. Nilipouliza gharama ni Tshs 150,000/= na kiasi kikubwa cha fedha kimetolewa na Serikali ya Kijiji cha Kisemvule. Hongera Mwenyekiti na Kamati yako ya Kijiji. Kujitangaza ni maendeleo pia!

Skimu ya umwagiliaji ya Msolwa kuboreshwa

Wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakikagua skimu ya umwagiliaji ya Msolwa iliyoko wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro ambayo kupitia Mradi mpya wa " Expanded Rice Production Project" ulioanza kutekelezwa mwaka 2015/16  ni moja ya skimu zilizo kwenye mpango wa kuziboresha ili ziweze kuongeza uzalishaji wa mpunga nchini.

Samaki-Faida inayoweza kupatikana kwenye skimu za umwagiliaji

Hivi karibuni nilitembelea skimu ya umwagiliaji ya kijiji cha Msolwa kilichoko wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro. Nilishangaa kuwaona watoto hawa wakivua samaki kwenye skimu hiyo. Hii ina maana kuwa kwenye skimu za umwagiliaji, wakulima wanaweza kutenga sehemu na kuwa na mabwawa ya kufuga samaki  na kujipatia kitoweo pamoja na mapato kwa kuuza samaki hao.