Saturday, October 30, 2010

Tatizo Kuosha vyombo


Shughuli ni nzuri lakini tatizo ni pale shughuli inapokwisha na sasa inabidi vyombo vioshwe. Kasheshe!

Hata Moro ipo 'Kiduku'

Vijana wa Moro walitupatia show ya 'Kiduku'

Bia bwelele


Huwezi kuamini, kulikuwa hakuna kadi ya kuingia ukumbini lakini wageni walikula na kunywa. Hakika bia zilikuwa bweleleee!

Bro Omari Jakka wa Mikumi alikuwepo


Tuliondoka Mikumi saa 12 asubuhi kuelekea Morogoro kwa nia ya kushuhudia Komunio ya Kwanza ya Eric. Pichani Bro Omari Jakka wa Mikumi na Dada Irene Banzi wakilisakata ruhmba ukumbini Tushikamane.

Dogo Elvis naye alikuwepo


Kama kuna mwalikwa ambaye alifurahi sana wakati wa sherehe za kumpongeza Eric Mkoba pale Tushikamane-Morogoro basi ni Elvis G.Banzi (Pichani)

Mama alirushwa juu juu


Ndugu, marafiki na majamaa walimrusha juu kwa juu Mama Eric (Restituta) huku wakimpongeza kwa zawadi mbalimbali hasa khanga na vitenge.

Wakati wa kuburudika


Baada ya kushughulika sana wajomba mama mkubwa wanaburudika. Pichani kutoka kushoto Gaitan Banzi,Anthony Kunambi, Faustini Mizambwa na Mama Mkbwa Dr.Doreen Moshi wakiburudika kwa raha zao! kwenye tafrija ya kumpongeza Eric ukumbini Tushikamane-Kilakala, mjini Morogoro.

Wengi walilishwa Keki




Eric aliwalisha keki wazazi, ndugu na marafiki zake waliohudhuria sherehe hiyo.

ERIC ALIKATA KEKI YA KOMUNIO YA KWANZA

Kabla ya kupata chakula Eric alikata Keki ya Komunio ya Kwanza.

Friday, October 29, 2010

Wamekuja kumpongeza

Ndugu, jamaa na marafiki kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini walikuja kushuhudia na kumpongeza Eric Mkoba kwa kupata Komunio ya Kwanza.

Thursday, October 28, 2010

Safari imeanza


Baada ya kumaliza Ibada, safari lianza kurudi nyumbani ambako Eric alipokelewa kwa shangwe na vigelegele.

Kanisa la Kigurunyembe


Kanisa hili lipo kwenye eneo kilipo Chuo cha Ualimu Kigurunyembe. Chuo hiki kina historia muhimu ya nchi hii inayohusu Elimu. Walimu wengi wamepitia chuoni hapa. Kilichonishangaza kwenye chuo hiki ni uchakavu wa miundo mbinu yake. Licha ya kujengwa mahali pazuri na plan nzuri. Miundombinu ni chakavu kwelikweli. Kwa wale wanaoifahamu Kigurunyembe ya wakati huo walisikitika kuona kuwa chuo kimekwisha. Kuna haja ya kuanza kukikarabati chuo hicho na kurudia enzi zake za zamani.

Eric Mkoba amepata Komunio


Kwa Mkristo Mkatoliki Sakaramenti ya Komunio ni moja ya sakaramenti 7 muhimu katika kanisa hilo. Jumapili iliyopita Eric Mkoba wa Kilakala Morogoro alipata Komunio ya Kwanza kwenye Parokiani Kigurunyembe, Mkoani Morogoro baadaye tafrija ya nguvu ilifanyika katika ukumbi wa TUSHIKAMANE.

Friday, October 22, 2010

Kariakoo ni kila kitu


Ukitaka kununua kitu chochote jijini Dar Es Salaam, tembelea maduka yaliyopo Kariakoo. Hapa hakuna kinachokosekana. Pichani mteja anafanya kinachoitwa 'window shopping'

Wataalamu wa kilimo wajadili habari za udongo


Hivi karibuni wataalamu wa kilimo wapatao 15 wengi wakiwa ni watafiti walikutana jijini Dar Es Salaam kupata taarifa ya Mradi wa Afsis wenye lengo la kukusanya na kusambaza taarifa za udongo barani Afrika zitakazorahisisha kutoa maamuzi sahihi ya matumizi ya udongo katika kilimo ili kuongeza tija na kuongeza kipato cha wakulima.

Paroko wa Vikindu Fr.Tommy

Paroko wa Parokia ya Vikindu Fr. Tommy (pichani kushoto)akitoa maelekezo wakati wa utoaji wa sakramenti ya Kipaimara iliyotolewa tarehe 17/10/2010 hapo parokiani.

Mjue Askofu Libena


Askofu Salutaris Melchior Libena alizaliwa tarehe 23 Nov 1963 Itete,Mahenge,mkoani Morogoro, alipata daraja la upadri tarehe 29 June 1991 akiwa na umri wa miaka 27. Mwaka 2010 Januari, 28 aliteuliwa kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo la Dar es Salaam, Tanzania na alisimikwa rasmi daraja la Uaskofu tarehe 19/3/2010 ni mmoja kati ya Maaskofu vijana, Tanzania.

Thursday, October 21, 2010

Mwenyekiti wa Parokia alitoa Shukrani


Mwenyekiti wa Parokia ya Mt.Vincent wa Paulo, Vikindu alitoa shukrani kwa niaba ya waumini kwa Askofu Salutaris Libena kwa kufika Parokiani kwa mara ya kwanza na kutoa Sakramenti ya Kipaimara kwa waumini.

Walijipanga kumshika mkono Askofu Salutaris


Waumini wote wakiwemo masista baada ya misa walijipanga kumshika mkono Askofu Libena

Parokia ya Vikindu ilifurika


Jumapili ya tarehe 17/10/2010 iliandika historia nyingine kwa parokia ya Vikindu. Kanisa lilifurika kama inavyoonekana pichani.

Askofu Salutaris atoa Kipaimara Vikindu


Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki,Jimbo Kuu la Dar Es Salamu Mhashamu Askofu Salutaris Melchior Libena Jumapili ya tarehe 17/10/2010 alitoa sakramenti ya Kipaimara kwa waumini 75 katika Kanisa Katoliki Mt.Vincent wa Paulo,Parokia ya Vikindu. Libena aliwataka waumini hao kuishi Kikristu. Alitoa onyo kwa wale wanaosahau sakramenti ya Kitubio na kuwataka kuwa wakatoliki hai kwa kushiriki Ibada zinazoendeshwa na Kanisa.

Naongea na Dr. Assenga


Siku ya Chakula Duniani nilipata bahati ya kuongea na Dr. Assenga, DALDO wa Ilala.

Walijionea wenyewe


Mambo ya Kimbiji yalikuwa makubwa, wajasiriamali kutoka Halamashauri za Wilaya za Temeke, Ilala na Kinondoni walileta bidhaa mbalimbali za vyakula vilivyoongezwa samaki. Hata sambusa zilipatikana hapohapo!

Tulifika Kimbiji


Baada ya kusafiri umbali wa zaidi ya kilomita 60 hatimaye tulifika Kimbiji na kushiriki kwenye maonyesho ya Siku ya Chakula Duniani Kitaifa.

Wizara ya Mifugo na Uvuvi walikuja na Kamba kochi


Si wengi wanaofahamu samaki ajulikanaye kwa jina la kamba kochi. Anafanana sana na kamba lakini ni mkubwa zaidi ya kamba. Kutokana na maelezo ya wataalamu inasemekana kuwa samaki huyo ni mtamu sana na ana proteini nyingi. Wakati mwingine ukitaka kununua samaki ulizia kamba kochi. Pichani kulia ni kamba kochi aliyegandishwa.

Siku ya Chakula Duniani-Kimbiji


Siku ya Chakula Duniani 16 Oktoba iliadhimishwa kitaifa Kijijini Kimbiji,wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar Es Salaam. Maonyesho yaliyotawala siku hiyo ni usindikaji wa vyakula mbalimbali.

Hawa ndiyo wageni waalikwa kwenye send-off ya Joy




Wazazi, ndugu, marafiki na watoto walishiriki kikamilifu katika kumuaga Joy pale Estana.

Mziki wa nguvu na waalikwa waliserebuka




Dj alikuwa na muziki wa nguvu. Nyimbo za aina mbalimbali zilipigwa na watu waliserebuka. Kibao kilichotia fora ni wimbo wa injili uliojulikana kwa jina la 'Kiatu kivue'

Na keki ilikatwa


Hatimaye ulifika wakati wa kukata keki. Keki hii ilikuwa na mchanganyiko wa ngano na mbatata kutoka Makete na Magimbi kutoka Matombo! Utamu mpka kisogoni!

Mzee Luhungu alitoa nasaha kwa mwanawe Joy


Kama kuna siku ambayo mzee Charles Kyando Luhungu alifurahi basi ni usiku wa tarehe 12/10/2010 pale ukumbini Estana. Baba Joy alicheza tangu alipofika ukumbini na katika kipindi chote cha sherehe. Na baadaye alitoa nasaha ya maisha mapya kwa mwanawe wa kwanza Joyce Kyando.Pichani Mzee Luhungu akitoa nasaha kwa mbwembwe!

Send Off ya Nguvu kwa Joyce Kyando


Usiku wa tarehe 12/10/2010 ulikuwa wa hoihoi vifijo na nderemo nyingi wakati wazazi, ndugu na marafiki walipomuaga binti yao mpendwa Joyce Kyando katika ukumbi maarufu wa Estana uliopo barabara ya Ali Hassani Mwinyi karibu na kituo cha mafuta cha Victoria jijini Dar. Pichani Joyce (kulia) akiwa na matron wake.