Monday, April 30, 2012

Huko ndiko kuagwa

Ukiona sanduku, ujue safari imeiva. Pichani Bw. George Ng'atigwa, akimuaga dada yake Adela Nga'tigwa wakati alipowakabidhi rasmi ukoo wa Kavia (mume mtarajiwa) katika ukumbi wa Magadu ulipo ndani ya Kambi ya Jeshi la Wananchi-Mzinga siku ya tarehe 28/4/2012.

Bw na Bibi Ng'atigwa

Hawa siyo maharusi bali wazazi wa Bi Adela Ng'atigwa Bw. Na Bibi Ng'atigwa wakiwa pamoja kwenye sherehe ya kumuaga binti yao iliyofanyika katika ukumbi wa Magadu Leaders Club mjini Morogoro tarehe 28/4/2012
Baba na Mama Adela kutoka kulia kwenda kushoto wakifuatilia kwa makini sherehe ya binti yao

Adela akitoa utambulisho

Adela akitoa utamblisho kwa wageni waalikwa.

Dada Adela Ng'atigwa akiingia ukumbini

Dada Adela Nga'tigwa akiwa na mpambe wake Imaculata Banzi wakiingia ukumbini Magadu Leaders Club Morogoro siku ya Jumamosi tarehe 28/4/2012 tayari kwa sherehe ya sendoff.

Tuesday, April 24, 2012

Jirani wa Chuo cha Nelson Mandela -Arusha

Jirani huyu amejenga karibu kabisa na Chuo cha Nelson Mandela kilichopo Arusha.Ni nyumba nzuri na ya kisasa huenda atapata wateja!

Uanikaji nguo maghorofani

Ni tabia iliyozoeleka na baadhi yetu kuanika nguo ovyo ovyo. Juma la jana Banzi wa Moro alifanikiwa kunasa jengo hili likiwa na nguo zilizoanikwa barazani. Hili ni jengo la ghorofa, ni kubwa na zuri lililoko kati kati ya jiji la Dar Es Salaam. Hivi kweli hii ni tabia nzuri ya kuanika kila kitu nje? Huu nao ni uchafu.

Uvunaji wa maji ya mvua

Shule ya Msingi Kisemvule iliyoko wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani imebahatika kuwa na mradi wa uvunaji maji. Maji haya hutumika kwa shughuli mbalimbali yanafaa pia kwa kunywa ila inashauriwa kuwa ni vizuri kuyachemsha kabla ya kunywa.

Ukitaka kwenda Kigogo

Juzi nilitembelea maeneo ya Kigogo. Barabara ya Kigogo kwa sasa ni nzuri na mabus yanayotumia njia hiyo ni mazuri na makubwa. Pichani ni njiapanda ya Kigogo. Hapa ndipo unapoweza kuunganisha mabus ya kwenda Kigogo, Mburahati na hata Manzese.

Monday, April 23, 2012

New Kisemvule Butchery

Mwekezaji amewahi Kisemvule. Sasa tuna duka la nyama. Zamani ilitubidi kupata kitoweo pale Vikindu au Mbagala. Sasa hivi nyama wakati wowote. Haya ni maendeleo yanayokuja kwa kasi katika kijiji ninachoishi, Kisemvule-Mkuranga.

Friday, April 20, 2012

Doreen Nyanjura


Msichana Doreen Nyanjura wa Uganda hivi karibuni alitawala vyombo vya habari vya Uganda na Afrika Mashariki baada ya kukamatwa na kutiwa ndani kwa sababu ya kuandika kitabu kiitwacho "Is it The Fundamental Change?"

Doreen ana umri wa miaka 22 na ni mwanafunzi wa chuo kikuu. Sifahamu kilichoondikwa ndani ya kitabu hicho kwani sijakisoma. Lakini kutokana na makala ya Padri Privatus Karugendo (Raia Mwema Aprili 18- 24,2012 baadhi ya nukuu ambazo zimenisisimua kwenye kitabu hicho kama alivyonukuu Karugendo ni "Maisha yanaelekea mwishoni, siku tunapokaa kimya kwa mambo ya msingi" na "Dunia inateseka, si kwasababu ya vurugu na maasi ya watu wabaya, bali ni kwa sababu ya ukimya wa watu wema".

Nimesisimka kuona msichana wa miaka 22 kuandika ambacho kinaanza kuleta changamoto! Hongera sana Doreen Nyanjura na pole kwa kutiwa kolokoloni!

Tunawachia nini watoto hawa?


Hili ni swali la kujiuliza wote hasa sisi watu wazima. Je, tunawaachia nini watoto hawa? Elimu bora? Uchumi imara? Uongozi safi? Huduma bora na za uhakika (Afya,maji, umeme..) miundo mbinu (barabara).

Vituko vya Iddi Amin Dadah


Inasemekana kuwa aliyekuwa Rais wa Uganda Gen. Iddi Amin Dadah alikwenda kununua ndege ya rais akiwa na fedha taslimu mkobani! Kwa utaratibu huo Iddi Amin amekuwa mtu wakwanza kununua ndege kwa mtindo huo!

Wednesday, April 18, 2012

Ah, magogo tena!


Amini usiamini biashara ya magogo imerudi kwa mtindo wa aina yake. Magogo husafirishwa kwa kufunikwa turubai ili yasionekane. Lakini hutokea gari likapata ajali, magogo kutofunikwa vizuri (pichani) na siri kufichuka! Hakika, biashara ya magogo imerudi upya!

DARLIVE yetu


Mbagala tuna DAR LIVE.Ilala Je?
Dar Live imeongeza heshima ya watu wa Mbagala.
Imeongeza mzunguko wa fedha.
Barabara ya Kilwa iboreshwe!

Uchafu karibu na KTM ya zamani


Uchafu umekithiri kando kando ya barabara ya Kilwa. Karibu na kiwanda cha Nguo cha KTM (zamani)- Mbagala Mission, hali ni kama inavyoonekana kwenye picha.

Huu si ustaarabu


Madereva wengi wanapoona kuwa kuna traffic jam basi hupita tutani. Camera ya Banzi wa Moro iliinyaka gari unaloliona pichani kwenye barabara ya Kilwa leo asubuhi. Je, hili ni suluhisho la kukwepa traffic jam? Huu ni ustaarabu?

Adha ya Traffic jam-Barabara ya Kilwa


Kwa wale tunaotumia barabara ya Kilwa tumeanza kuonja adha ya 'Traffic jam' hasa nyakati za asubuhi. Kinachosababisha ni barabara mbovu.

Duka la viatu vya Bata


Wazee wetu bado wanaamini kuwa viatu vyenye jina la biashara 'Bata' ni imara. Kampuni ya viatu ya Bata ni ya Kenya. Jijini Dar wana maduka yanayouza bidhaa hizo. Pichani moja ya maduka katika ya jiji la Dar Es Salaam.

Thursday, April 12, 2012

Tukubali Dar chafu


Siku ya jana mvua kubwa ilinyesha jijini Dar. Nilishuhudia mafuriko katika mto Kizinga. Baadhi ya maeneo ya Tandika nyumba zilibomoka.Uchafu ulijitokeza waziwazi kwenye mitaa ya Tandika, Temeke na Mbagala. Mifereji imeziba maji hayatiririki kwenye mitaro iliyojengwa. Kila aina ya uchafu ulisambaa kirahisi kabisa. Mifuko ya plastiki, chupa, matambara, miwa, matunda, matairi chakavu na vingi vingi. Ni uchafu ambao umekuweko kwenye mitaa yetu kwa siku nyingi bila kushughulikiwa. Nina imani kuwa kuna kampuni za usafi zinazolipwa na jiji au Manispaa husika. Hizi zinafanya kazi gani je zinapata malipo bila kazi? Manispaa kwanini zimeshindwa kusimamia usafi? Mbona Moshi wameweza. Hakika ukifika Moshi utadhani ndiyo makao makuu ya Tanzania kwa jinsi maeneo yalivyo safi. Moshi kila mmoja ni askari wa usafi. Tukubali Dar Chafu!

Tuesday, April 3, 2012

Mawasiliano na Banzi wa Moro


Kuanzia sasa unaweza kuwasiliana na Banzi wa Moro kwa kutumia email addresses zifuatazo:- banzi.john@yahoo.com;jlsbanzi@gmail.com

kuna wasomaji wangu wengi walikuwa wakiuliza mbona siwajibu wakinitumia msg kwa email ya jbanzi@hotmail Ndugu zangu hii ilishibiwa na wajanja siku nyingi kwa hiyo nilikuwa siitumii lakini ilikuwa inaonekana kwenye blog yangu ingawa mimi nilikuwa natumia hiyo ya gmail.Leo nimempata mtaalamu wa IT hapa Mananga Centre na kunirekebishia mamboos.Vitu sasa safi kabisaa.Byebye hotmail.Na pole sana aliyeningilia hata kama hajui Kiswahili habari ndiyo hiyo!

Nauli za mabus Tanzania hizi hapa

Bango linaonyesha taarifa ya nauli za mabus kutoka Dar Es Salaam kwenda mikoani.(Nashindwa kufahamu kama Abood Bus ni kawaida,luxury au semi luxury).Jamani, Mkuranga nayo ni mkoani kama ilivyo Kibaha mbona haipo bangoni. (Picha kwa hisani ya Michuzi Blog).

Heshimu lugha ya mwenzako

Hebu soma bango hilo pichani. Bango hili ni moja ya mabango mengi yaliyotundikwa chuoni Mananga, Swaziland.Tafsiri kutoka Kiswati kwenda kiingereza inaeleweka.Je? Bango hilo lingeruhusiwa kutundikwa Tanzania?(Picha kwa hisani ya Leonard Mabuga, masomoni Mananga, Swaziland)

Mambo ya mpakani

Si mpakani mwa Swaziland wala Msumbiji ubadilishaji wa fedha kwa magendo unaendelea waziwazi. Hao wanaoenekana pichani wote wanafanya biashara ya kubadilisha fedha.

Squarters za Maputo

Maputo ni jiji kubwa ukilinganisha na Mbabane, Swaziland lakini unapoanza kuingia jijini Maputo ukitokea Swaziland habari ndiyo hiyo!

Jinsia inazingatiwa chuoni Mananga

Wimbi la kujiendeleza kitaalamu haliangalii jinsi ya mtu. Hapa chuoni Mananga idadi ya wanachuo ukizingatia jinsi ni asilimia 50 wanawake na asilimia 50 wanaume. Wanawake wana nafasi sawa na wanaume na kwa hakika wanawake wanapewa kipaumbele zaidi. Hata waajiri wameshaliona hilo ndiyo maana hali ni kama nilivyoieleza.

Msafiri Kafiri!

Msafiri kafiri.Ndiyo methali tuliyoizoea nyumbani Tanzania. Nikiwa Maputo Msumbiji hivi karibuni nilithibitisha uhalisia wa methali hiyo. Tukitokea Swaziland (nyumbani kwetu) tulijiandaa kwa vitafunnwa na vinywaji. Tulipofika Maputo tulipata kifungua ndani ya gari letu tulilosafiria. Mimi nilipata kipande cha kuku sehemu ambayo huwa siipendi!Tuko ugenini, safarini-Kweli Msafiri Kafiri.

Madafu- Maputo kama Dar!

Madafu bwelele jijini Maputo, Msumbiji. Vijana hao (nje ya uzio) walipotuona walitukimbilia na mkokoteni wao wakitaka kutuuzia madafu lakini kwa kuwa lugha gongana tulishindwa kunywa maji ya dafu ( Wao Wareno sisi Waingereza!).Kwa hiyo hata bei ya dafu jijini Maputo siijui!

Monday, April 2, 2012

Kila mlo - Juice

Kuna Juice za aina nyingi kutoka matunda mbalimbali.Hapa Mananga kila mlo lazima upate juice.Kuna juice ya maembe, mapera,machungwa,passion fruit....Unajua mimi napenda juice gani? (Hiyo yenye rangi nyekundu!)

Inawezekana

Essau Banda (katikati) ni Mhasibu - Benki Kuu Malawi na pia ni Mchungaji(Pastor).Tupo naye Swaziland hapa chuoni Mananga. Juzi tulisafiri naye kwenda Maputo Msumbiji. Kabla ya kuanza safari yetu tuliomba mmoja wetu aombe kwa sala ili Mungu aibariki safari yetu. Banda alijitokeza na kuomba sala fupi na nzuri.Kwenye bus nilikaa karibu naye pembeni yake kulikuwa na kitabu. Nilimuomba kukisoma ndipo nipogundua kuwa Banda ni mchungaji baada ya kusoma ukurasa wa kwanza ulioandikwa Pastor Essau Banda! Ona, Banda hajawahi kujionyesha kuwa ni mchungaji au mlokole. Na pia sikutegemea kuwa na mchungaji akisoma mambo ya dunia hapa Mananga, kumbe yote inawezekana!

Sunday, April 1, 2012

Na hapa ni Lomahasha border post ya Swaziland

Lomahasha kituo cha uhamiaji cha Swaziland.

Mpakani Namaacha-Msumbiji

Jana tarehe 31/03/2012, Mwenyekiti wa 'Africana Group' akiwa mpakani mwa Msumbiji na Swaziland.

Shamba la Miwa la Simunye-Swaziland


Shamba la miwa la Simunye nchini Swaziland

Bus linapovuta trailer la mizigo

Lori kufungwa trailer ni kitu cha kawaida nchini Tanzania lakini kwa bus hasa la abiria sijaona. Jana tarehe 31/3/2012 akiwa ziarani jijini Maputo nchini Msumbiji,Banzi wa Moro alishuhudia bus hili likivuta trailer lenye mizigo ya abiria.Usalama wa mizigo ya abiria!(sina jibu)

Ushuru wa barabara-Maputo

Unapoingia au kutoka Msumbiji kwa gari ni lazima ulipie ushuru.Pichani gari yetu ikisubiri kulipia ushuru jana tarehe 31/3/2012

Siyo photoshop

Leonard ndani ya Maputo akitokea Swaziland.Utamtaka!

Sina la kuwadanganya April 1

Banzi wa Moro Kando ya mti wa Yanga,Simunye-Swaziland!