Thursday, April 12, 2012

Tukubali Dar chafu


Siku ya jana mvua kubwa ilinyesha jijini Dar. Nilishuhudia mafuriko katika mto Kizinga. Baadhi ya maeneo ya Tandika nyumba zilibomoka.Uchafu ulijitokeza waziwazi kwenye mitaa ya Tandika, Temeke na Mbagala. Mifereji imeziba maji hayatiririki kwenye mitaro iliyojengwa. Kila aina ya uchafu ulisambaa kirahisi kabisa. Mifuko ya plastiki, chupa, matambara, miwa, matunda, matairi chakavu na vingi vingi. Ni uchafu ambao umekuweko kwenye mitaa yetu kwa siku nyingi bila kushughulikiwa. Nina imani kuwa kuna kampuni za usafi zinazolipwa na jiji au Manispaa husika. Hizi zinafanya kazi gani je zinapata malipo bila kazi? Manispaa kwanini zimeshindwa kusimamia usafi? Mbona Moshi wameweza. Hakika ukifika Moshi utadhani ndiyo makao makuu ya Tanzania kwa jinsi maeneo yalivyo safi. Moshi kila mmoja ni askari wa usafi. Tukubali Dar Chafu!

No comments: