Friday, April 20, 2012

Doreen Nyanjura


Msichana Doreen Nyanjura wa Uganda hivi karibuni alitawala vyombo vya habari vya Uganda na Afrika Mashariki baada ya kukamatwa na kutiwa ndani kwa sababu ya kuandika kitabu kiitwacho "Is it The Fundamental Change?"

Doreen ana umri wa miaka 22 na ni mwanafunzi wa chuo kikuu. Sifahamu kilichoondikwa ndani ya kitabu hicho kwani sijakisoma. Lakini kutokana na makala ya Padri Privatus Karugendo (Raia Mwema Aprili 18- 24,2012 baadhi ya nukuu ambazo zimenisisimua kwenye kitabu hicho kama alivyonukuu Karugendo ni "Maisha yanaelekea mwishoni, siku tunapokaa kimya kwa mambo ya msingi" na "Dunia inateseka, si kwasababu ya vurugu na maasi ya watu wabaya, bali ni kwa sababu ya ukimya wa watu wema".

Nimesisimka kuona msichana wa miaka 22 kuandika ambacho kinaanza kuleta changamoto! Hongera sana Doreen Nyanjura na pole kwa kutiwa kolokoloni!

No comments: