Monday, February 20, 2012

KATC wanahudumia skimu za umwagiliaji

Kilimanjaro Agricultural Training Centre (KATC)ni moja ya vyuo vya Kilimo chini ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika.Sifa kuu ya chuo hiki ni katika kutoa mafunzo ya kilimo bora cha mpunga kwa wakulima, afisa ugani na wadau wengine hasa katika teknolojia ya kilimo cha umwagiliaji.Chuo hiki ni maarufu sana kwenye skimu za umwagiliaji kama inavyoonekana kwenye picha.


Watoto wenye tabia njema

Leo jioni nikiwa kazini katika kijiji cha Mabogini, Moshi vijijini nilidondosha noti ya shilingi mia tano. Watoto hawa waliiona na kuikota kisha waliniita, "mzee umedondosha hela." Nikaitikia wito nikapokea noti hiyo kisha nikawarudishia na kuwaambia asante watoto wazuri.Jambo la maana nililojifunza kutoka kwa watoto hawa ni kwamba wana malezi mazuri kutoka kwa wazazi/walezi na walimu wao.Wangeweza kuificha noti hiyo kisha wakagawana.Hongera kwa wazazi na walimu wa watoto hawa.

Wakati mwingine mbuzi hupigana


Hata wanyama wakikorofishina hutuniana misuli. Ndivyo Banzi wa Moro alivyowakuta mbuzi hawa wanaofugwa KATC-Moshi wakipigana vichwa leo jioni.

Saturday, February 18, 2012

Wanahitaji miundo mbinu ya kisasa

Mkoa wa Pwani ni mmoja kati ya mikoa uliyajiliwa kuzalisha aina mbalimbali za matunda yakiwemo machungwa, mananasi, maembe,pasion, matikiti,matango. Aidha inazalisha kwa wingi nazi na korosho. Tatizo ni soko la uhakika kwa mazao hayo. Kwa kawaida kila zao lina msimu wake isipokuwa kwa nazi.Wakulima wakipata mbinu bora za uzalishaji na uhakika wa soko hakika uzalishaji utaongezeka na kipato cha wananchi kitaongezeka.

Wafanyabiashara hawa wadodowadogo wa matunda wanahitaji elimu,mbinu na miundombinu bora ya kisasa kuboresha soko la matunda yao. Hii ndiyo hali halisi kijijini Kisemvule kwenye soko doko la kituo cha bus.


Kuongezeka kwa pikipiki

Taifa limeshuhudia ongezeko kubwa la pikipiki mijini na vijijini. Je hii tafsiri yake ni nini? Ni kiashiria cha kukua kwa uchumi au imetokana na haja ya kukabiliana na tatizo kubwa la usafiri mijini na vijijini. Utafiti usio rasmi unaonyesha kubwa wamiliki wa wamiliki wa pikipiki hizi kwa asilimia kubwa ni vijana wa kiume huku wengine wakipata huduma za usafiri.Licha ya kusababisha ajali nyingi, ongezeko la pikipiki kwa kiasi kikubwa limesaidia kurahisha usafiri hasa vijijini. Pengine ni kiashiria cha kukua kwa uchumi nchini.

Makazi yanaongezeka miti inakatwa

Makazi mapya yanaongezeka kwa kasi kubwa jijini Dar Es Salaam na sasa watu wanatafuta makazi mapya mkoa wa Pwani. Hivi sasa minazi na miembe inapungua kwa kasi ya kutisha mkoa wa Pwani kupisha makazi mapya. Pichani makazi mapya kijijini Kisemvule.

Tuanze kufuga bata

Bata ni aina ya ndege wafugwao wanafanana sana na kuku lakini watu wengi hasa Watanzania wanaamini kuwa nyama ya bata imepooza lakini ukijaliwa kutembelea nchi ya Uholanzi mgeni aliyeheshimiwa hukaribishwa nyama ya bata na bei yake ni aghali ukilinganisha na kuku. Ufugaji wa bata ni rahisi ukilinganisha na wa kuku kwani hawashanbuliwi sana na magonjwa na chakula chake hupatikana kirahisi pia wanawezwa kufugwa ndani ya ua au banda.
Ni vizuri sasa watanzania wakahamasika kufuga bata kwani kilishe hana tofauti na kuku. Bei ya bata hapa Dar es Salaam ni kati ya Tshs 15,000-20,000/=

Hivi ndivyo ilivyokuwa

Kwa mila na desturi za watu wa Pwani kwenye mihadhara wanaume na wanawake hawakai sehemu moja. Na ndivyo ilivyokuwa kwenye mkutano wa Kijiji cha Kisemvule kilichopo wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani.Pichani wanawake walio wengi walikaa peke yao tena chini ya majamvi na mikeka wengi walikuwa wasikilizaji huku wanaume wakikalia viti na wakitawala mahajadiliano!

Monday, February 6, 2012

Kijiji kiliandaa mashine ya kurushia sauti

Kwa kuboresha mawasiliano siku ya Mkutano wa kijiji uongozi ulikodisha mashine ya kurushia sauti. Ile ilisaidia kusikilizana kwa ufasaha na kuelewana.Pichani kijana akiendesha mashine ya kurushia sauti.

Mzee Begeya wa Kisemvule


Mzee Begeya (wa pili kutoka kulia mwenye bargashia ya maua na kanzu ya draft)ni mmoja kati ya wazee wanaoheshimika kijijini Kisemvule. Sifa yake kuu ni kuhudhuria mikutano iwe ya kijiji ya wazazi hakosekani labada kwa udhuru. Na awapo kikaoni huwa na nguvu ya hoja.Wakati nilipopiga picha hii alinihoji je ina maslahi kwake?

Na hawa je?


Wakati kikao kinaendelea vijana waliokuwa ndani ya banda hili waliendelea na mchezo wa 'draft' bila kujali, kama vile wao si wanakijiji. Hawa ndiyo vijana wetu. Watanzania wa kesho, wanakisemvule wa kesho. Hivi kweli maendeleo yanaweza kupatikana katika mtazamo huu? Hivi kweli mkutano wa kijiji ni wa wazee tu? Yakiptishwa maamuzi, vijana wanalalamika wamesahaulika. Utakumbukwaje kama huhudhurii vikao na kutoa hoja au kero kwa maendeleo ya kijiji na taifa kwa ujumla?

Vijana wataka kiwanja cha michezo


Vijana wachache walihudhuria Mkutano Mkuu wa Kijiji cha Kisemvule huku wakitaka kufahamu ni lini kijiji cha Kisemvule kitamiliki Kiwanja chake cha michezo? Kwani kilichopo sasa ni cha mtu binafasi wakati wowote anaweza kuamua matumizi mbadala wa kiwanja hicho. Kijiji inafanyia kazi hoja hiyo.

Mdau wa Kijiji cha Kisemvule


Mmoja wa wadau waliokaribishwa katika mkutano wa Kijiji cha Kisemvule ni Mkurugenzi wa Taasisi za Elimu (Shule ya Msingi White Angels & Sekondari ya Bright Angels)Bw. Mwambeleko, (mwenye mic) alipewa fursa ya kutoa nasaha zake kwa kijiji.

Mkutano wa Kijiji cha Kisemvule 5 Februari 2012

Mkutano wa Mwaka wa Kijiji cha Kisemvule ulifanyika jana tarehe 5/2/2012 kijijini Kisemvule. Hapo yalizungumzwa mambo mengi ya msingi. Nikiwa mwanakijiji wa Kisemvule nilifurahishwa na kiwango cha uaandaji wa taarifa za kijiji. Uongozi ulitoa taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2011 na kuwasilisha Bajeti ya mwaka 2012 itakayoishia mwezi Desemba kipaumbele namba moja kikiwa ni kujenga zahanati ya kijiji ambayo itagharimu takribani tshs 21,000,000/=. Kwenye kikao hicho wanakijiji wengi walihudhuria wakiwemo wake kwa waume, vijana na wadau mbalimbali wa maendeleo kati yao ni wakuu wa shule za msingi na sekondari, Bwanashamba wa Kijiji na Mganga Mkuu wa Dispensary ya St. Vicent Vikindu.

Wanakijiji walipata taarifa za mapato na matumizi ya kijiji kwa mwaka 2011 ambapo mapato yaliyopatikana ni kiasi cha Tshs 37 milioni.Takribani asilimia zaidi ya 70 ya mapato haya yalitumika kuimarisha ofisi ya kijiji kwa kujenga ukumbi wa mikutano, vyumba vya biashara na ukarabati. Ukumbi wa mikutano unatarajiwa kukamilika na kuanza kutumika mwaka huu. Nyingine zilitumika katika kuboresha miundo mbinu ya shule za msingi (Kisemvule) hasa kutengeneza madawati. Sekondari ya Vikindu aliyopo kijijini ambayo ni ya kata walipata fedha za kujenga bohari ya shule.

Changomoto kubwa iliyojitokeza suala la ulinzi wa kijiji kwa wakati huu ambao wahamiaji ni wengi na shughuli ni nyingi.Migogoro ya ardhi ni moja ya changamoto inayoikumba serikali ya kijiji yote haya yalijadiliwa na kupendekeza njia ya kuweza kukabiliana nazo.

Katika kuleta mabadiliko na kuboresha kipato cha wanakijiji ushauri ulitolewa kwa wanakijiji kujiunga katika vikundi vya maendeleo na kubuni na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya kilimo na ufugaji.
Kijiji cha Kisemvule kilichopo mkoani Pwani wilaya ya Mkuranga ni kijiji kinachokua kwa kasi ya haraka kutokana na wawekezaji kupendelea kuwekeza katika kijiji hicho kutokana mazingira mazuri yanayopatikana katika kijiji hiki kama vile ardhi,barabara nzuri, umeme na maji mengi na yenye ladha nzuri.
Mwenyekiti wa Kijiji Bw. Omari Makunge akifafanunua jambo.
Katibu Mtendaji wa Kijiji Bw. Mzome(wa kwanza kushoto)akisikiliza kwa makini hoja.
Vijana wakiwa mkutanoni
Mama Eric (mwenye khanga begani)mwanakijiji wa Kisemvule akiwa mkutanoni amechangia hoja nyingi zenye manufaa hasa za kilimo na ufugaji.
Akina mama nao walijumuika na wanakijiji wengine katika mkutano huo na kuchangia hoja mbalimbali hasa elimu.
Meza kuu ilikuwa makini na kujibu hoja kutoka kwa wanakijiji.
Kama kawaida idadi ya wanaume mkutanoni ilizidi ile ya wanawake hivyo hivyo kwa hoja.

Wednesday, February 1, 2012

Ukarimu wa Watanzania

Ukarimu wa Watanzania ni wa asili. Karibu makabila yote hapa nchini yanajua kukarimu vizuri. Mgeni anapptembelea nyumbani kwako jitahada zinafanywa kuhakikisha kuwa amekarimiwa vya kutosha hasa chakula. Hivi ndivyo ilivyokuwa nilipokuwa Arusha nilipopata nafasi ya kuwatembelea ndugu na jamaa.Mama Vanesa (Mrs Himili Mbawala)aliandaa chakula cha jioni
Mtoto Vanesa alishiriki pia lakini mvuto ulikuwa kwa chips kama ilivyo kawaida kwa watoto kupenda chips.
Gari ya familia ilitumika kunipeleka sehemu muhimu nilizopenda kuziona kama vile Taasisi ya Nelson Mandela.
Familia nzima pamoja na mgeni wanajumuika na kuongea pamoja baada ya chakula

Mhadhiri Sheila Mziray

Mama Sheila Mziray ni Mhadhiri Mwandamizi Chuoni ESAMI ni mtalaamu wa Raslimali Watu na masuala ya Menejimenti. Unauzoefu wa miaka mingi kwa kufanya kazi katika taasisi mbalimbali moja wapo ikiwa 'World Vision'. Kazi nyingi za kitaalamu amezifanya ndani na nje ya nchi kama vile Malawi na Zambia. Huyu ni mmoja kati ya wahadhiri waliotupatia utaalamu,mbimnu na uzoefu katika masuala ya JINSIA kwa muda wa wiki mbili za mafunzo pale ESAMI.Tanzania tuna wataalamu ambao wanakubalika ndani na nje ya nchi lakini hatuwatumii ipasavyo. Jirani zetu wanafaidika na wataalamu wetu sisi tunapiga usingizi au tunawadharau! Pichani Mhadhiri Mziray akiwa darasani na pia wakati wa chakula cha pamoja (special lunch)siku ya kuhitimu mafunzo yetu