Saturday, August 31, 2013

Mashine ya kubangua karanga

Mashine hii ya kubangua karanga iliyoletwa kwenye maonyesho ya wakulima 2013 huko Dodoma katika banda la Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika idara ya utafiti Utafiti

Friday, August 30, 2013

Furaha ya kikombe cha kinywaji cha kishona nguo cha RESEWO

Wadau na wanachama wa RESEWO wakifurahia kikombe cha kinywaji cha Kishona nguo inayotengenezwa na RESEWO.

Chai ya Kishona nguo iliyotengenezwa na RESEWO

Chai kutoka mmea wa kishona nguo (Black jack)iliyotengenezwa na akina mama wa RESEWO wa Kijitonyama.Kishona nguo kina dawa muhimu za kulinda afya zetu na kuwezesha jamii kupunguza gharama kubwa za hospitali kwa kutumia mboga ya kishona nguo, au chai yake hupunguza kasi ya malaria,huongeza damu mwilini,hutuliza maumivu ya meno,huimarisha afya ya macho na pia huponyesha baadhi ya vidonda -vikiwemo vinavyowathiri walio na virusi vya Ukimwi.

Delega-Mboga ya asili

Delega ni moja ya mboga za asili zinazostawishwa kwenye bustani ya RESEWO pale Kijitonyama-Kijiji cha Makumbusho.Mboga hii inanikumbusha nyumbani kwetu Morogoro.Bibi zangu walikuwa wanaipika kwa kuchanganya na ufuta na nyanya chungu. Huenda delega ni zaidi ya mboga!

Unapoomba kupitia mzimu

Banzi wa Moro ilimnasa kijana huyu akiwa ndani ya kijiji cha Makumbusho Kijitonyama akiomba chini ya kibanda cha mzimu. Sijui, lakini kwa kuwa nilimkuta akiwa na makabrasha huenda anaoomba apate fursa ya kusomea shahada ya PhD!

Wanachama wa RESEWO

Tarehe 29/08/2013 Kikundi cha wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo chakula na Ushirika walioko kwenye mafunzo ya juma moja yanayohusu jinsia katika shughuli za kilimo kilitembelea kikundi cha wajasiriamali kiitwacho RESEWO (Regent Estate Senior Women Group)kinachoundwa na akinamama wapatao 22 wengi wao wakiwa wastaafu waliojikita katika uzalishaji wa mboga za asili kama vile mnavu,mchicha maua,delega na mazao mengine.Kikundi hiki kinafanya mambo mengi na wanayo mengi ya kueleza kuhusu mboga na mimea ya asili tuliyonayo ambayo wengi hutafahamu. Wanapatikana katika Kijiji cha Makumbusho, kando ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi, katika Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar Es Salaam.Watemblee.

RESEWO wa Kijitonyama

Regent Estate Senior Women Group (RESEWO) kinatoa huduma ya chakula cha asili zikiwemo mbogamboga pia inastawisha mimea aina mbalimbali ya asili inayoweza kutibu baadhi ya magonjwa yanayowasumbua binadamu kama vile kisukari,malaria,kuvimbiwa. Kikundi hiki cha akina mama kinafanya shughuli zake katika kijiji cha Makumbusho,Kijitonyama-Dar Es Salaam.

Wednesday, August 28, 2013

Zabibu kutoka Makutopora

Zabibu aina ya Makutopora kutoka kituo cha Utafiti-Makutupora, Dodoma ni moja ya matunda ya watafiti wetu wa Tanzania. Zabibu hizi zinafaa kutengenezwa mvinyo mweupe na hasa champaigne ni tamu pia zikitafunwa. Kinachotakiwa kwa sasa ni kusambaza aina hii ya mbegu kwa wakulima wa zabibu na pia kuboresha viwanda vyetu vya kuzalisha mvinyo. Kwanini tuagize champaigne kutoka nje? Aina hii ya zabibu inapaswa kupigiwa debe. Watanzania tupende vya kwetu!

Mashine ya Kupandikiza mpunga

Moja ya kazi ngumu katika kilimo cha mpunga ni kupandikiza (transplanting). Kazi hii mara nyingi hapa Tanzania hufanywa na wanawake. Mashine hii (rice transplanter) iliyoletwa kwenye maonyesho ya wakulima viwanja vya Nzuguni, Dodoma ilivutia wadau wengi wakiwemo wanafunzi ambao ni vijana.Mashine zinapotumika kwenye kilimo zinavutia vijana kukipenda kilimo hivyo kushiriki kwenye uzalishaji.

Watafiti vijana na teknolojia za kilimo

Watafiti vijana Dorah Bivugile (kushoto) na Athumani Mahinda kutoka kituo cha Utafiti wa Kilimo, Makutupora,Dodoma wakionyesha teknolojia mbalimbali za kilimo zilizobuniwa na watafiti katika maonyesho ya wakulima kitaifa yaliyofanyika mjini Dodoma Agosti 2013.Ni vizuri kuwajengea uwezo watafiti vijana.

Mabus ya kwenda kasi (DART) yatakavyokuwa

Haya ni moja ya aina ya mabus yanayokwenda kasi (DART) yatakayotumika jijini DAR yatakavyokuwa.Model hii ilionyeshwa huko Dodoma kwenye viwanja vya Nanenane,Nzuguni.

Mabus ya kwenda kasi (DART) maonyeshoni Dodoma

Nilishangaa kukuta banda la mabus ya kwenda kasi (DART) yatakayotumika jijini DAR kwenye maonyesho ya wakulima mjini dodoma mwaka huu (2013).Kweli kuna uhusiano kati ya wakulima na wanaoishi mjini. Mabus ya kwenda kasi si kwa Dar Es Salaam tu ni kwa watanzania wote wakiwemo wakulima inabidi wote tufahamu jinsi mradi huo utakavyokuwa na hatua ambayo imeshafikiwa.

Idara ya Kilimo banda la Chamwino

Hakika, banda la Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino lilikuwa banda bora kwenye maonyesho ya wakulima mwaka 2013 kule Dodoma. Angalia jinsi idara ya kilimo ilivyojipanga.

Bidhaa za wajasiriamali wetu

Nilifurahi nilipoona wajasiriamali wengi waliojitokeza kwenye maonyesho ya wakulima yaliyofanyika kitaifa kule Dodoma mapema mwezi agosti 2013.Wanawake walikuwa mstari wa mbele kuonyesha ubunifu wao. Kwenye banda hili Banzi wa Moro aliweza kununua mkoba mdogo wa kuweka vifaa vya wanafunzi kwa bei ya Tshs 10,000/=. Hakika mkoba huo sasa anautumia mmoja wa mabinti zangu na anaupenda sana kuliko mikoba ya mtumba!

Mtambo wa kusafisha mafuta ya kula

Mtambo huu wa kusafisha mafuta ya kula (k.m.alizeti) umetengenezwa na wabunifu kutoka Iringa.Ni ubunifu huu ulionyeshwa kwenye banda la Wizara ya Viwanda na Biashara huko Nzuguni Dodoma wakati wa maonyesho ya wakulima(Nanenane 2013). Gharama yake ni Tshs 75,000,000/=. Ubunifu huu unapaswa kuendelezwa.

TIRDO - analysis ya mafuta ya Alizeti

TIRDO wamefanya uchunguzi wa mafuta ya alizeti yanayokamuliwa kienyeji (majumbani/sehemu zisizo rasmi)Ni vyema mafuta hayo yakafanyiwa double refining ili yaweze kuwa bora zaidi. Kwa kutumia mitambo iliyobuniwa huko Iringa. Mafuta haya yanawezwa kusafishwa na kuongezewa ubora wake.

Thursday, August 8, 2013

Zabibu za kutengeneza mvinyo

Ni wachache wanaofahamu kuwa Tanzania inazalisha zabibu na hasa mkoa wa Dodoma. Kwenye banda la Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Idara ya Utafiti na Maendeleo, maelezo ya ustawishaji wa zao hilo yalitolewa na watafiti kutoka kituo cha Utafiti Makutupora.Zabibu hutumika kutengeneza mvinyo au divai pia zinatumika kama kiburudisho (tunda) kwa kutafuna.

Nyanya Banda la Chamwino

Nyanya hizi zimewavutia wengi waliotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kwenye viwanja vya Nzuguni-Dodoma  maonyesho ya kilimo  Kitaifa 2013. Hizo ni nyanya aina ya Meru zilizotolewa na watafiti wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika-HORTI-Tengeru, Tanzania.

Wanaandaa mbegu za alizeti

Nikiwa katika maonyesho ya kilimo ya Taifa 2013 viwanja vya Nzuguni - Dodoma niliwakuta akina mama hawa wakiandaa mbegu za alizeti tayari kwa mauzo kwenye banda la Halmashauri ya Wilaya, Chamwino-Dodoma.

TANDAN FARMS maonyeshoni Dodoma

Nanenane Nzuguni.Hapa nakutana na wajasiriamali kutoka Tandan Farms kutoka Vikindu - Kisemvule, Mkuranga, Pwani. Hawa ni wajasiriamali wa mifugo na kuiongezea thamani ya mazao ya mifugo hasa nyama. Wako karibu kabisa na Kanisa Katoliki Vikindu, Jesus - Town.

Tuesday, August 6, 2013

Ubora wa Nyanya aina ya Meru

Mtaalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino akielezea ubora wa Nyanya aina ya Meru kwenye viwanja vya Maonyesho ya Kilimo - Nzuguni,Dodoma 2013

Monday, August 5, 2013

Kituo cha 'kuchimba dawa'-Mikese Morogoro

Kituo hiki kilichopo Mikese, Morogoro kinawasaidia abiria kuweza kujisaidia wakiwa safarini bila gharama yoyote.Uchafuzi wa mazingira sasa basi!

Msamvu Primary School bado ipo

Kwa wenyeji wa Morogoro hawawezi kuisahau Msamvu Primary School iliyopo Morogoro mjini. Shule hii ya msingi imelea watoto wengi. Nakumbuka miaka ya sabini shule hii pamoja na shule nyingine za Morogoro mjini zilikuwa zikitumika kama kambi za wanafunzi katika mashindano ya michezo iliyokuwa ikiendeshwa katika wilaya za Morogoro mjini na vijijini. Msamvu bado ipo.

Bango la Moro

Unapoingia mjini Morogooro unakaribishwa na bango hili. Je, Manispaa inapata chochote?

Maboga aina ya Kisasa kutoka Chamwino

Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, mkoa wa Dodoma inastawisha mazao mengi yakiwemo maboga haya ambayo yamekuwa kivutio kikubwa katika maonyesho wa wakulima maarufu-Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni - Dodoma

Ndizi aina ya Mtwike kutoka JKT

Ndizi aina ya mtwike katika banda la maonyesho ya kilimo JKT viwanja vya Nzuguni, Dodoma 2013.

Sunday, August 4, 2013

Miaka 16 ya kubariki ndoa yetu

Tarehe 2/8/2013 mimi na mke wangu Nancy Mbawala tumetimiza miaka 16 ya kubariki ndoa yetu. Suti yangu,viatu pamoja na shati bado vipo, ila suruali kwa sasa inabana pamoja na viatu pia. Shela ya mama tuliazima! TUNAMSHUKURU MUNGU.

Nancy anakata Keki ya miaka 16 ya harusi yetu

Nilishangaa kukuta keki ya miaka 16 ya harusi yetu!

Familia yetu

Tulipofunga ndoa tulikuwa na hao jamaa wawili Sisty na Ude miaka 16 baadaye wameongezeka Catherine na Maria kweli familia imeongezeka!

Ka bia kangu cha miaka 16 ya harusi yetu

Raha jipe mwenyewe na ka bia. Sijamwalika mtu,nasherehekea miaka 16 ya harusi yetu mimi na mke wangu mpenzi Nancy Mbawala tukiwa nyumbani kwetu Vikindu, Kisemvule, wilayani Mkuranga!

Miaka 16 ya harusi yetu-Kiatu changu bado kinadai!

Tumetimiza miaka 16 ya sherehe ya harusi yetu tarehe 2/8/2013. Bado navikumbuka viatu vyangu vya siku tulipofunga ndoa na mke wangu mpendwa Nancy.