Friday, January 3, 2014
Mwaka 2014 nimeanza na matunda
Wengi wetu hupenda matunda. Tunaambiwa matunda yana vitamin aina nyingi ambayo huipa miili yetu kinga. Kwenye picha kuna ndizi,mananasi,machungwa, zabibu,peyas na pichis. Tanzania tumebahatika ya kuwa na matunda ya tropiki na matunda ya kutoka sehemu za baridi kama Mgeta mkoani Morogoro, Njombe, Tukuyu, Lushoto na sehemu nyingine. Lakini matunda kama vile ndizi, mananasi na machungwa hupatikana kwa wingi kijijini kwangu Matombo mkoa wa Morogoro. Kilimo cha matunda ni Biashara. Kwenye mazingira yanakostawi matunda tujikite na kilimo hicho na tufuate ushauri kutoka kwa wataalamu tulime kwa faida. Wakulima tubadilike. Fedha ziku shambani.Karibu Morogoro tule matunda!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment