Tuesday, November 1, 2011

SIKUKUU YA WATAKATIFU WOTE


Leo tarehe 1 Novemba, Kanisa Katoliki linakumbuka watakatifu wake wakiwemo marehemu wote. Nilibahatika kuhudhuria ibada fupi Parokiani kwangu Vikindu huku nikiwakumbuka wazazi wangu ndugu zangu marafiki majirani na wengine ambao wameaga dunia. Nachukua fursa hii kwa kumbukumbu ya mpenzi Bibi yetu Sr. Maria Magdalena aliyefariki mwaka mmoja uliopita. Tuongozane kwenye kumbukumbu ya hali ilivyokuwa siku ya mazishi yake huko Mgolole Conventry-Morogoro.

No comments: