Wednesday, November 2, 2011

Nilipata nafasi ya kuiwakilisha familia


Ninasimuliwa kuwa Marehemu Bibi yangu Sister Maria Magdalena wakati nikiwa mdogo na kuugua malaria kali alinishughulikia sana kupata matibabu katika hospitali ya masista pale Mgolole Conventry na kuwa hai hadi sasa. Ndiye aliyenifanya kuifahamu Mgolole. Akiwa hai alikuwa akinikumbusha nyimbo niliyokuwa nikimwimbia wakati huo akiwa Sister kijana kabisa. Wimbo ulikua hivi. Lo lo lo kipenzi changu, lo lo lo kipenzi changu, umenitia kishindoX2. Moyo wahangaika.. Sijui alinifundisha nani? Hata yeye alikuwa akishangaa kabisa. Kwahiyo mara nyingi nikikutana na bibi nilikuwa namwimbia nyimbo hiyo.

Bahati niliyoipata kwa marehemu Bibi ni kutoa neno la shukrani kwa niaba ya familia siku ya mazishi yake. Haikuwa kitu rahisi! Binti Makeya imekuwa historia. Lakini tutamkumbuka kwa mengi aliyoitendea familia na watu wote wakati wa uhai wake. Kwetu sisi wanafamilia alikuwa ni kiungo kizuri cha familia. Huyo ndiye aliyekuwa Bibi Mzuanda amezaliwa wa mwisho na kufa wa mwisho. Mungu uilaze mahali peponi roho ya marehemu Sister Maria Magdalena. AMINA

No comments: