Tuesday, November 1, 2011

Rafiki yangu Mwaseba


Kwa sasa anajulikana kama Dr. Dismas Lyegendili Mwaseba. Ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA). Niseme kuwa Dis tumetoka naye mbali sana. Kwa mara ya kwanza nilikutana naye Tosamaganga High School mwaka 1978 tukiwa Form V-CBG (cabbage). Wote tukitokea Dar Es Salaam-Magomeni. Mwenzangu akitokea Mwembechai na mimi Kota.(Inayovunjwa sasa). Tuliishi chumba kimoja pale Tosa. Sasa mwenzangu ni Sociologist pale SUA na mimi Economist -MAFC. Pichani akiwa ofisini kwake SUA.

No comments: