Wednesday, September 10, 2014

'Morogoro mji kasoro bahari' alisema J.K.Nyerere

Bwawa la Mindu
Ha! Kumbe jina la utani la ''Moro mji kasoro bahari' lilianzishwa na Baba wa Taifa Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere. Akiusifia mji wa Morogoro ulivyo mzuri ila kasoro hauna bahari. Hii ilikuwa ni katika harakati za Uhuru wa Tanganyika akiwa katika kampeni ya kugombea ubunge jimbo la Morogoro. Nyerere aliahidi katika kampeni hizo kuwa akifanikiwa kupata ubunge ataileta bahari Morogoro. Na kweli alitimiza ahadi yake kwa kuchimba bwawa la Mindu. Lakini kwa bahati mbaya maji yake hayana chumvi kama ya bahari. Alipoulizwa mbona maji hayana chumvi kwa utani alisema ataleta viroba vya chumvi na kuvimimina ndani ya bwawa hilo!

No comments: