Monday, September 8, 2014

Ndizi -Simba?

Ndizi rangi nyekundu unaweza kuiita ndizi ya simba sports club. La hasha, kwetu Matombo Morogoro ndizi hii inaitwa mzungu. Kabla ya kukomaa ndizi zake huwa rangi ya kijani, zinapokomaa na kuiva huwa na rangi nyekundu. Kwanini wanaiita mzungu na isiwe nyekundu mimi sina maelezo ya zaida. Ndizi hizi kwa sasa zimeanza kupotea. Watafiti wa kilimo wanakazi ya kutunza nasaba ya ndizi ya aina hii.

No comments: