Thursday, May 31, 2012
Mradi wa Ufugaji wa Kuku wa asili-Msosa
Moja ya vijiji vinavyopiga hatua ya kasi katika kilimo ni kijiji cha Msosa kilichoko wilaya ya Kilolo, mkoa Iringa. Kijiji hiki kiko karibu sana na barabara kuu ya Tanzania - Zambia sehemu maarufu ya Ruaha Mbuyuni. Licha ya wakazi wake kujikita katika kilimo cha vitunguu, sasa wameanzisha mradi mwingine wa ufugaji wa kuku wa asili. Mwaka 2010 kikundi kijulikacha JIPE MOYO kiliwezeshwa jumla ya shilingi 1,900,000 ambazo ziliwezesha kikundi kujenga banda la kuku na kuku wa kufuga na wanakikundi walichangia jumla ya shilingi 180,000/=. Kikundi kina jumla ya wanachama 21 wengi wao ni wanawake (17). Mradi huu kwa sasa hutumika kama shamba darasa la ufugaji bora wa kuku. Lengo ni kuboresha kuku wa asili. Wakulima hufundishwa lishe ya kuku, tiba, ujenzi wa banda bora na jinsi kuweka kumbukumbu za ufugaji ili kuweza kufuga kwa faida.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment