Sunday, May 13, 2012
Kilimo kinavyobadili maisha ya wakulima
Niko kikazi mikoa ya Iringa na Mbeya kwa madhumuni ya kukagua miradi inayotekelezwa na Programu ya kuendeleza Sekta ya Kilimo Tanzania (ASDP).Mpaka sasa nilichokiona kinatia moyo pale miradi ilipotekelezwa vizuri.Vijiji ambavyo havikutekeleza vizuri mambo ni 'business as usual' Wakulima wetu wanafanya kazi katika mazingira magumu. Wanazalisha ili kutulisha sisi. Kuna wengine kilimo kimebadilisha maisha yao. Kwa mfano wakulima wa kijiji cha Magozi Iringa vijijini kutokana na kilimo cha mpunga sasa wana uhakika wa chakula mwaka mzima, wengi wameweza kujenga nyumba bora pia wamejinunulia jenereta ya kufua umeme!
Mpunga ndani ya viroba
'Satelitte dish' kijijini Magozi wilaya ya Iringa Vijijini
Nyumba bora za kisasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment