Tuesday, December 30, 2014

Shule ya Msingi Matombo





Hii ni sehemu ya shule ya msingi Matombo nilikosoma darasa la tatu na la nne miaka ya 1970. Enzi hizo ilikuwa moja ya shule bora kabisa (lower school) ukifaulu mtihani wa darasa la nne (ambao nilifaulu) ndipo unapokwenda darasa la tano (middle school). Hali ya shule hii si nzuri kwa sasa angalia madawati yalivyo machache na ni ya zamani sana. Wakati napiga picha hizi nilibahatika kukutana na Mwl. Mkuu wa shule hii (mwanamama) ambaye kwa kifupi alinielezea matatizo ya madawati na kuniomba tukumbuke kuisaidia shule yetu. Nawaomba wote tuliosoma Matombo Primary School tusaidie shule yetu hali si nzuri hapa na pengine hii ikiwa moja ya sababu ya wanafunzi kutofaulu vizuri mitahani yao ya darasa la saba.

No comments: