Tuesday, December 30, 2014

Nakutana na Familia ya Michael Luanda


Nikiwa Matombo nilikutana na Bw na Bibi Michael Luanda ambao nao walikuwa kwenye mapumziko ya Christamass. Familia hii ni marafiki wa siku nyingi na familia yangu. Michael tumesoma wote Primary School Matombo, tukafaulu tukaenda Njombe Secondary School mwaka 1974. Tumeishi wote Dar kwa muda mrefu tukisaidiana kwa shida na raha nimeshiriki kwenye harusi yao nao wameshiriki kwenye harusi yetu. Michael nyumba yake ya kijijini Matombo amejengea Mtamba nilifika kwao nifahamu alipojengea nimefurahia jiwe hilo ambalo lipo kando ya nyumba yao. Niliwatania kuwa tayari wameshaanaza kujenga uzio imara. Kweli sehemu hii inapendeza.

No comments: