Tuesday, December 30, 2014

Makaburi ya Dr. Mluge na Balozi Mloka


Haya ni makaburi ya marehemu Dr. Gregory P.Mluge na Balozi  Daniel N.Mloka. Hawa ni baadhi ya waluguru wasomi wa mwanzo kutoka Matombo (bila kumsahau marehemu Chief Kunambi) hawa wamesoma shule ya msingi Matombo   na  hatimaye  Makerere University College, Uganda. Mluge alichukua masomo ya science na kuwa Daktari (Tabibu) wakati Balozi Mloka alisoma masomo ya Arts na kujikita kwenye masuala ya uchumi na siasa ambazo zilimuwezesha kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu kwenye wizara mbalimbali na pia Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani na Sweden. Wote wawili wamezikwa kwenye makaburi ya misheni kijijini Kiswira, Parokia ya Matombo, Morogoro.

No comments: