Tuesday, December 23, 2014

Naelekea Matombo-Nawatakia Christmass njema

Ndugu zangu, nawatakia Christmass njema. Banzi wa Moro atakuwa kijijini Matombo, Morogoro kusheherekea Sikukuu ya Christmass. Nitaimba Gloria ndani ya Kanisa Kongwe la Katoliki - Mt.Petri na Paul. Nitakuwa na Babu na Bibi zangu,mama,baba,shangazi,wajomba,kaka,dada,wadogo na watoto wangu, marafiki zangu tuliokua na kusoma nao pamoja hasa shule za msingi Matombo na Gozo. Nitapata fursa ya kuongea Kiluguru nipendavyo. Merry Xmass!

No comments: