Friday, December 5, 2014

Tulifika na Tandahimba pia


Afisa Ugani wa Kilimo-Wilaya ya Tandahimba-James Chitumi



Katika zoezi letu la kuperemba teknolojia za kilimo zilizopelekwa kwa wakulima mkoani Mtwara kupitia Mradi wa EAAPP tulifika pia wilayani Tandahimba. Huko tulikutana na Wataalamu wa Kilimo na watendaji wa Wilaya pamoja na wakulima. Tulizungumza nao kuona kama wanaufahamu mradi wa EAAPP pia kupata mawazo yao katika kuendeleza zao la muhogo wilayani humo. Kwa wakulima tulitembelea mashamba ya mfano ya muhogo yanayotekelezwa na kusimamiwa na vikundi vya wakulima. Kuna vikundi vinavyofanya vizuri na kuna vile vinavyosuasua. Tulichojifunza, wakulima wa Tandahimba wako tayari kupokea teknolojia mpya za kilimo zile zenye manufaa kwao. Mfano halisi ni kwa zao la korosho. Korosho kwa Tandahimba ni kila kitu kwao ndiyo 'engine' ya Halmashauri. Wakulima wanahudumia zao la korosho vizuri vizuri sana. Wilaya ya korosho inapiga hatua ya kasi zaidi kwa maendeleo. Sehemu chache tulizotembelea tumekuta  nyumba bora za kisasa vijijini na zilizojengwa kwa mpangilio mzuri. Shule zao za msingi na sekondari ni nzuri. Ukidodosa utaambiwa ni kwa sababu ya pato kutoka zao la korosho.

No comments: