Tuesday, December 30, 2014

Niliweza kufunga magoli nikitokea wingi ya kulia

Hiki ni kiwanja cha mpira wa miguu cha Matombo Secondary School. Wakati nasoma shule ya msingi Matombo (sasa sekondari) niliweza kufunga magoli mengi kupitia goli hili nikitokea winga ya kulia. Wakati mwingine pia nilikaa katikati ya goli kama golikipa na kunyaka mikwaju ya pembeni. Hata hivyo kutokana na ufupi wangu wachezaji mahiri walitumia udhaifu huo kunifunga kirahisi kwa mipira ya juu. Kiwanja hiki ndicho kilichonifanya niipende soka hadi hii leo. Namkumbuka mchezaji bora kabisa wa zama hizo Fransic  Kidondile (No.10) huyu ndiye alieyekuwa 'Pele' wa Matombo.

No comments: